Tanzania Tulikuwa salama zaidi Mikononi mwa Ujamaa kuliko Tulivyo sasa Mikononi mwa Ubepari/Ubeberu

Tanzania Tulikuwa salama zaidi Mikononi mwa Ujamaa kuliko Tulivyo sasa Mikononi mwa Ubepari/Ubeberu

Japan ni wajamaa?
Kina Toshiba na Toyota ni wajamaa? Kina Rakuten?

Ujerumani ipi ya wajamaa? Hii hii ya kina Volkswagen? Sweden ya kina Volvo ndo unasema wajamaa?! Acha uongo wewe
Kwani ujamaa unazuia umiliki binafsi wa mali ?
 
Mkuu 'Proved', wewe mwenyewe bila shaka umegundua mleta mada kaweka mada ya kichokonozi kuamsha hisia za watu tu kwa jinsi alivyo iwasilisha.

Tuondoke huko kwenye 'dogma' za kizamani enzi za "Vita Baridi". Hizi ni enzi tofauti kabisa nasi tunatakiwa kuangalia maslahi ya nchi yetu katika mazingira haya ya leo, siyo yale ya juzi.

Mleta mada analaumu akina Mwinyi na wengineo; lakini anasahau kwamba tayari tulikuwa kwenye matatizo makubwa kama nchi siyo kwa sababu ya Ujamaa, bali haliya uchumi wa duniaani kote ilikuwa na mtikisiko; na kwa bahati mbaya sana kwetu tukawa na majanga mfululizo wakati huo huo. Vita Kagera, ukame uliosababisha ukosefu wa chakula, n.k.

Ni wapi katika ukanda huu ambapo hapakutokea mtikisiko wakati huo, iwe wana siasa za kibepari au za kijamaa Hapo jirani enzi za Moi huwezi kusema uchumi wao ulikuwa mzuri, ukiacha tu hizi propaganda zisizokuwa na miguu.

Kuna mambo ninayokubaliana na mkuu 'Burkinabe' katika mada yake, ikiwa ni pamoja na upotofu wa msimamo wa serikali zetu tukea enzi za Ruksa, Mkapa na Kikwete.

Matatizo yetu sasa yatakayotuchelewesha kusonga mbele kimaendeleo sasa hivi, siyo sababu ya siasa za kijamaa au kibepari. Tumekwishaona kwamba, hata katika ujamaa maendeleo yanawezekana, kama ilivyo katika ubepari. China katufundisha kuwa 'Socialist Economy" inao uwezo wa kuliondoa taifa katika rindi la umaskini.

Na tunajua pia, kwamba hata katika ubepari, nchi inaweza kabisa isifanikiwe bila ya kuweka mkazo katika baadhi ya mambo muhimu, kama kubana ufisadi na kuweka mfumo mzuri wa kiutawala ili shughuli za wananchi ziende vizuri.

Hatuwezi kufanikiwa kwa kutegemea wawekezaji toka nje na huku sisi wenyewe tukipanga kupeleka manamba nchi za nje.

Hali kadhalika, hatuwezi kuendelea kama serikali haiweki mipango madhubuti kujenga uwezo wetu wenyewe kujenga taifa letu

Kamwe hatuwezi kuendelea kama tunayo serikali isiyokuwa na uwezo wa kuwabana mabepari na mijizi ili raslimali zetu zisaidie ujenzi wa taifa letu.

Ukitaka kufungua nchi, hakikisha umejijengea uwezo wa kuhakikisha kuwa hukujisahau na kuruhusu kuliwa hata usikotaka uliwe.

Socialist economy
Duniani hapa twende na mixed economy, serikali ibaki kutoa basic huduma kama umeme, elimu, Afya na maji,
Masuala ya serikali kuuza sukari ni upuuzi mtupu duniani siku hizi
 
Why una focus kwenye unafuu? Sisi tunaongelea UFANISI. Cheap is not always efficient or effective. Having said that, nakupa mfano TRA inapaswa ku audit MNCs zaidi ya 300 kwenye eneo la transfer pricing CAG anasema ni 10% ya MNCs hukaguliwa. Cha ajabu private sector kampuni kama KPMG au Deloitte n.k zinaweza audit hizo kampuni zote!! Ndio unajiuliza why waweze ila TRA ishindwe? Kwanini? Sababu serikali hawana profit incentive wala shareholders wa kuwashika koo!!

Kuhusu Nishati bado haijawahi kuwa supplied na kampuni binafsi otherwise mgao ungebaki historia maana competition ingekua kubwa so kampuni A ikifeli kwenye distribution watu wanahamia kampuni B.
Yeah zipo kampuni mbovu hata sekta binafsi ila sio nyingi as compared to sekta ya umma zilizo mbovu. Katika kampuni zaidi ya 100 za serikali zinazo underperform ni zaidi ya 80!! Na hili hata JPM alisema hazikuwahi toa gawio tokea zianzishwe.
Una niuliza kwa nini nafocus kwenye unanafuu kwani msingi mkuu wa utoaji wa huduma za kijamii ni nini kama sio ubora na unafuu ?

Kwamba unataka huduma za kijamii ziwe katika hali ya gharama kubwa ? Una hakika makundi mangapi yatapokea huduma hizo na makundi mangapi yatakosa huduma hizo ? Kitu ambacho hakipaswi kuwa
 
Duniani hapa twende na mixed economy, serikali ibaki kutoa basic huduma kama umeme, elimu, Afya na maji,
Masuala ya serikali kuuza sukari ni upuuzi mtupu duniani siku hizi
Kiujumla ninakubaliana na wewe. Na kwa kweli sijui serikali inayouza sukari leo hii moja kwa moja; lakini kama unavyojua, hiyo ni bidhaa muhimu. Pamoja na kwamba watu binafsi wataendesha biashara hiyo; serikali haitaweza kujitoa na kuacha biashara iendeshwe kiholela.
Sote tunayo kumbukumbu jinsi tulivyokuwa tukiwaona akina Manji pale Dodoma Bungeni wakiwa na mabegi yaliyokuwa yamejazwa pesa za kuwalainisha wabunge waruhusu waliyotaka yaruhusiwe na hao wabunge.

Kwa hiyo serikali haiwezi kujiondoa moja kwa majoa katika swala lolote linalowahusu wananchi.
 
tu serikali katika eneo lolote, hata huko ku 'regulate' unakokusema wewe, tayari dhana nzima ya 'pure' imekwisha katika
Hujaelewa, ikibaki regulator means inaondoa kampuni zake kwenye ushindani mfano TTCL, NBC, NMB, ambazo in one way or the other zaweza haribu ushindani. Mfano TTCL ndio inaongoza mkonga wa taifa ila bado imefeli kusambaza hata internet tu majumbani. Imagine mkonga wa taifa ungekua chini ya vodacom?. Haya TPDC wana upstream company inayopewa tender huko kwenye kuchimba gesi ila wamefeli hata kuuza gesi ya magari imagine hiyo tender ingekua ya Lake Gas??
Hilo swala la serikali kujiondoa katika kila kitu, kwa kusema tu haiwezi kufanya chochote kwa ufanisi ni dhana nisiyokubaliana nayo kabisa
Hukubaliani na uhalisia? Hivi TRA isipo deliver kuna repercussions gani? Ila kampuni binafsi kama Ernst and Young ingepewa kazi ya kukusanya kodi ungeshangaa inafika ufanisi wa 90%. Sababu huko serikalini hakuna KPIs, mikataba ni ya kudumu, wanaajiri bila kuangalia competence ni interview tu ya mtihani, haya uwajibishaji ni zero maana sijawahi sikia mtu kafukuzwa kwa kushindwa kudeliver zaidi ni utovu wa nidhamu ndio pekee inaweza kukufukuzisha ila private sector mfano NIDA wangeambiwa ID 10,000 kwa siku ukishindwa unatimuliwa!!!
Kama maana ya serikali ni hiyo, basi ijiondoe kabisa hata katika maisha ya watu kabisa; jambo ambalo haliwezekani popote.
Wewe umesema tusikariri alafu hapa unasema "haliwezekani popote ". Why unajicontradict mwenyewe?. Na hapa ndio maana kuna ugatuzi kwamba kila eneo lijiendeshe lenyewe kulingana na context yake so kuna miji katika nchi moja ila ina mitazamo ya kiuchumi tofauti kabisa. So usikariri kwamba lazima centralization iwepo ndio nchi isonge, that's not the case.
Hizo unazo sema ni sera za CHADEMA; hujui kuwa hilo ni moja ya mambo yanayowafanya CHADEMA wasikubaliwe sana sehemu mbalimbali nchini? Sera hizo mara nyingi zimekuwa kama ni siri kubwa, hazielezwi kinagaubaga, matokeo yake yanakuwa kama ni hila za chama kuingiza maswala wasiyo yaelewa wananchi.
Hakuna mkutano wa chadema hatujasema hizi sera za majimbo, private sector n.k hata kampeni za 2020 Lissu alikua akitetea private sector na kupinga serikali kufanya biashara n.k na bado alikua ana pull crowds kubwa. Na ndio maana wapiga kura wengi wa chadema ni middle class na higher ups sababu wako more secured na sera zao kuliko under CCM ambayo ina protectionism kubwa. Kuhusu wananchi maskini hawa hupiga kura tu based on hype na hisia ila informed voters ambao pengine ni 30% pekee hii nchi basi be assured wanaipigia chadema kwa sababu ya sera za mrengo wa kati kulia.
 
Una niuliza kwa nini nafocus kwenye unanafuu kwani msingi mkuu wa utoaji wa huduma za kijamii ni nini kama sio ubora na unafuu
Hapana unafuu pekee sio ufanisi na ndio hapa tunafeli, NIDA ni bure ila mpaka leo sina ID ila kingeuzwa na private sector kwa elfu 5 ningeshapata na hao wengine serikali ingewalipia kuliko kusema bure alafu hakuna ID na serikali inalipa mishahara na expenses zingine zaidi ya 20B huko NIDA per year.

Huduma za kijamii hospital zenye PPP huwa ni both affordable and EFFICIENT sababu serikali inatoa pesa ila management ni ya mtu binafsi. So hili ni funzo mfano Mkonga wa taifa serikali ingeuweka chini ya PPP na vodacom pengine kila nyumba ingekua na full broadband kwa bei nafuu kelele za MB zingeisha. Lakini mkonga wa taifa upo chini ya TTCL see how its a failure!! Its cheaper but hakuna huduma inatufikia sio network, line, speed, wala huduma nzuri. So tuache kufocus kwenye affordability ila Efficency. Otherwise regulators wapo wafanye price ceiling tu kama wanachofanya TMDA, TIRA, TCRA, PURA n.k bei haitopanda hata TANESCO ikiwa distribution ya umeme kupitia sekta binafsi
Kwamba unataka huduma za kijamii ziwe katika hali ya gharama kubwa ? Una hakika makundi mangapi yatapokea huduma hizo na makundi mangapi yatakosa huduma
Serikali igharamie tu kama sasa ila kupitia private sector. Yaani mfano badala ya kutoa billion 10 kuendesha TRA inaweza tumia pesa hiyo hiyo kulipa kampuni binafsi kama Deloitte kukusanya mapato na kuhakikisha zinapitia hazina na kwamba ikishindwa deliver tender inahamia kwingine, imagine that efficency. Same to hospitali za serikali ziendeshwe kwa PPP utaona mabadiliko makubwa. Hii dhana ya kuamini ikiwa chini ya serikali ndio cheaper ilihali inaweza kuwa cheaper kwa PPP kupitia ruzuku itakua better.

Mfano wa mwisho pesa za halmashauri mbona hazirudishwi? Ila CRDB ukikopa usirudishe mali zote zinataifishwa. Ndio sasa tunasema ufanisi ni mkubwa kupitia private sector, je serikali ikitoa hiyo mikopo kupitia CRDB unadhani kuna mtu atashindwa rejesha?
 
Hujaelewa, ikibaki regulator means inaondoa kampuni zake kwenye ushindani mfano TTCL, NBC, NMB, ambazo in one way or the other zaweza haribu ushindani. Mfano TTCL ndio inaongoza mkonga wa taifa ila bado imefeli kusambaza hata internet tu majumbani. Imagine mkonga wa taifa ungekua chini ya vodacom?. Haya T
zi kwamba kila eneo lijiendeshe lenyewe kulingana na context yake so kuna miji katika nchi moja ila ina mitazamo ya kiuchumi tofauti kabisa. So usikariri kwamba lazima centralization iwepo ndio nchi isonge, that's not the
Hivi kweli mistari uliyoninukuu hapo juu nimeeleza chochote kuhusu "lazima ya ku-centralize" au unataka kunilazimisha nikubali unayotaka wewe niyakubali?

PDC wana upstream company inayopewa tender huko kwenye kuchimba gesi ila wamefeli hata kuuza gesi ya magari imagine hiyo tender ingekua ya Lake Gas??
Ona sasa mifano unayotumia hapa kuhalalisha nadharia unayoing'ang'ania kama msahafu.
Kwa nini hao watu wa serikali uwategemee kwa kufeli tu na siyo kufanikiwa? Why? Kwa sababu ni kasumba iliyojengeka kuwa serikali haiwezi kufanikisha jambo lolote; lakini tunaiona mifano sasa, mashirika ya kichina yakiwa yameenea kila sehemu duniani yakifanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Sina tatizo na huku; ingawa najua hata wewe unafahamu kwamba ni uongo kudhani kuwa serikali haiwezi kusimamia na kuendesha huduma za mashirika kama hayo. China wametuonyesha mifano wazi kabisa.

Ninalokataa ni hili la kasumba ya kusema serikali haiwezi kufanya jambo, kama kusimamia uendeshaji wa shirika. Hii ni fallacy
 
Hapana unafuu pekee sio ufanisi na ndio hapa tunafeli, NIDA ni bure ila mpaka leo sina ID ila kingeuzwa na private sector kwa elfu 5 ningeshapata na hao wengine serikali ingewalipia kuliko kusema bure alafu hakuna ID na serikali inalipa mishahara na expenses zingine zaidi ya 20B huko NIDA per year.

Huduma za kijamii hospital zenye PPP huwa ni both affordable and EFFICIENT sababu serikali inatoa pesa ila management ni ya mtu binafsi. So hili ni funzo mfano Mkonga wa taifa serikali ingeuweka chini ya PPP na vodacom pengine kila nyumba ingekua na full broadband kwa bei nafuu kelele za MB zingeisha. Lakini mkonga wa taifa upo chini ya TTCL see how its a failure!! Its cheaper but hakuna huduma inatufikia sio network, line, speed, wala huduma nzuri. So tuache kufocus kwenye affordability ila Efficency. Otherwise regulators wapo wafanye price ceiling tu kama wanachofanya TMDA, TIRA, TCRA, PURA n.k bei haitopanda hata TANESCO ikiwa distribution ya umeme kupitia sekta binafsi
Serikali igharamie tu kama sasa ila kupitia private sector. Yaani mfano badala ya kutoa billion 10 kuendesha TRA inaweza tumia pesa hiyo hiyo kulipa kampuni binafsi kama Deloitte kukusanya mapato na kuhakikisha zinapitia hazina na kwamba ikishindwa deliver tender inahamia kwingine, imagine that efficency. Same to hospitali za serikali ziendeshwe kwa PPP utaona mabadiliko makubwa. Hii dhana ya kuamini ikiwa chini ya serikali ndio cheaper ilihali inaweza kuwa cheaper kwa PPP kupitia ruzuku itakua better.

Mfano wa mwisho pesa za halmashauri mbona hazirudishwi? Ila CRDB ukikopa usirudishe mali zote zinataifishwa. Ndio sasa tunasema ufanisi ni mkubwa kupitia private sector, je serikali ikitoa hiyo mikopo kupitia CRDB unadhani kuna mtu atashindwa rejesha?
Mifano yote unayotoa hapa ni mifano mibovu, kwa sababu imekuwa ni jadi hapa kwa mashirika ya umakutofanya vizuri kwa sababu mbalimbali, nyingi zikiwa ni hujuma toka kwa watendaji huko huko serikalini wakishirikiana na hizo kampuni binafsi.

Tunaona Ethiopian Airlines iking'ara kabisa na kuingiza faida, lakini mifano kama hiyo hutaki kuitazama.
 
Mfano wa mwisho pesa za halmashauri mbona hazirudishwi? Ila CRDB ukikopa usirudishe mali zote zinataifishwa. Ndio sasa tunasema ufanisi ni mkubwa kupitia private sector, je serikali ikitoa hiyo mikopo kupitia CRDB unadhani kuna mtu atashindwa rejesha?
haya, unanipa mfano kama huu, sijui unataka niseme nini; nikubali kwamba serikali haiwezi kufanya vizuri?

Tutegemee nyakati zote kutofanya vizuri?

Sasa hata huko unakotaka wakusimamie, ku-regulate' kwa mwendo wa namna hii watafanikisha kitu gani?

Kuna sababu zipi za kuwa na serikali, kama uwezo wao ni huo unaoueleza wewe hapa?
 
Democratic Socialist Countries 2023

Nimejua nikiandika usoshalist na sio communism.

Ukiweza kusoma hapo juu labda utaelewa dhana na jnsjcaturs za usoshalist.
Umesoma hio link ?
Isome uielewe, mifano ya hizo nch ndio kinachofanyika saiz Tz,
Basic huduma zinatolewa na serikali wakati bizness ni free market, kila mbuzi ale kwa kamba,

In short ili jamii iendelee kiuchumi ubepari is the way
 
Japan ni wajamaa?
Kina Toshiba na Toyota ni wajamaa? Kina Rakuten?

Ujerumani ipi ya wajamaa? Hii hii ya kina Volkswagen? Sweden ya kina Volvo ndo unasema wajamaa?! Acha uongo wewe
Kuna tofauti Kati ya socialism na communism. Nyerere alitumia jina “ujamaa” akadai kuwa halina tafsiri.

Wengi kwa makosa wanafikiri ujamaa ni socialism. Lakini ukweli sio socialism bali ni ukomunisti uliopewa vinasaba bandia vya demokrasia ili kufanana na socialism. Km, kwenye socialism hakuna kutaifisha mali bila fidia wala kuzuia umiliki binafsi wa mali na uwekezaji binafsi. Aliipenda zaidi modeli ya China ya Mao lakini pia alitaka kuendana na matakwa ya wasoshalisti wa Ulaya.

Hivyo usishangae hizo nchi ulizotaja kuitwa za kijamaa. zimekuwa na serikali za kisoshalisti (social democrats) mara kadhaa. Kiswahili zinaitwa za kijamaa hivyo hivyo pamoja na mkanganyiko alioacha Nyerere kuhusu maana halisi ya “ujamaa”. I hope nimeeleweka.
 
Umesoma hio link ?
Isome uielewe, mifano ya hizo nch ndio kinachofanyika saiz Tz,
Basic huduma zinatolewa na serikali wakati bizness ni free market, kila mbuzi ale kwa kamba,

In short ili jamii iendelee kiuchumi ubepari is the way
Tatizo hujafika na kuishi kwenye usoshalisti kujua na ku-experience falsafa na maisha ya jamii ya kisoshalisti ikoje.

Fika Kenya, fika South Afrika na fika Marekani kwenye jamii za kibepari ambazo ni purely capitalist, Kenya, South Afrika hata Marekeni, masikini wanabakia kuwa masikini.
Marekani imewachukua muda mrefu masikini kuwa na mfumo wa bima ya afya, ilimhitaji Obama kuja na inclusive medCare (Obama care).

Watanzania huwa mnalaumu bila kujua misingi, tatizo sio usoshalist, ila misingi na falsafa yake inaigusa vip jamii.
Mfano, elimu ya bora na ya bure ni falsafa ya usoshalist. Karibu nchi zote za Nordic wana elimu bora kabisa; zinagharimiwa na kodi za wananchi.
Nchi kama hizi ambazo hujui kuna ubepari uchwara au usoshalist, unakuta waziri mwanae anasoma shule ya kibepari na ataiba hela tu ili mwanae asome huko, akijua shule za umma hakuna elimu bora.
Nyerere kaacha misingi ya shule za umma mpaka vyuo vya umma ndiko kulikuwa na uhakika wa elimu bora na jumuishi. Kutokae shule ya msingi mpaka chuo kikuu. Dhana ya wasio na uwezo wa kifedha kukopeshwa kwa dhamana ya serikali (umma) ni usoshalist.

Kwenye ubepari, ukiwa masikini, serikali ni ya matajiri na kwenye emerging economies matajiri wengi ni majizi na wapiga ma-deal na mifano ipo.

Usiwe mvivu, tembea, kaishi kwenye jamii za usoshalist; utaelewa exactly falsafa na misingi yao. Huwezi kukuta tajiri mkubwa kama Bill Gates Norway/Sweden, ila kuna utajiri uko shared na masikini hawapo na wachache sana. Nenda US, kuna Elon Musk na kuna watu wanalala barabarani, hawana uhakika wa kula na wamezaliwa na kukulia Marekani.
 
Amani iwe nanyi nyote.
Kwa wale wazee wenzangu mtakubaliana na mimi kwamba Tanzania ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo endapo ingeendelea na mfumo wa Ujamaa chini ya chama kimoja kuliko ilivyo sasa.

Uchumi wetu ulianza kuyumba mara tu awamu ya pili chini ya Mzee Ruksa, Alhaji Ali Hassani Mwinyi ilipoingia madarakani na kuusaliti Ujamaa wa Hayati Mwl. JKN.

Hadi kufikia mwaka 1987, uchumi wa Tanzania ulikuwa unaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Hii ina maana uchumi wetu ulikuwa mkubwa kuliko hata wa Kenya ambayo ndiyo kinara kwa kuwa na uchumi mkubwa katika ukanda huu kwa sasa!

Miaka ya 1990 tulipokubaliana na mambo ya kipuuzi kama nchi, tukapoteana kabisa na hali yetu haijatengamaa mpaka kesho. Fedha yetu inazidi kuporomoka mwaka hadi mwaka huku kukiwa na pengo kubwa sana kati ya wenye nacho na wasionacho.

Hivyo ushauri wangu ni serikali kufanya kila linalowezekana kuturudisha katika mfumo wetu wa Ujamaa; Sera inayotutofautisha sisi na majirani zetu. Hii itasaidia kuleta ustawi kwa wote na kutuondolea kero ya kuwa na viongozi wezi na vibaka waliojificha kwa mavazi ya uongozi.
Asalaam Aleykum.
Kwani ujamaa ulifutwa lini Tanzania?
 
Huna akili!

Nadhani hata kuzaliwa utakuwa umezaliwa mwaka 1995.

Kama ulikuwa na akili miaka ya 1982- 1985 na ulishuhudia namna watu kwalivyokuwa wanavaa viraka na kuogea majani ya mipapai kama sabuni sidhani kama unaweza kuja kuandika huu upuuzi wako hapa.

Ujamaa ni laana.
Asaivi tuko wapii? Labda km unaishii DSm
 
Ona sasa mifano unayotumia hapa kuhalalisha nadharia unayoing'ang'ania kama msahafu.
Kwa nini hao watu wa serikali uwategemee kwa kufeli tu na siyo kufanikiwa? Why? Kwa sababu ni kasumba iliyojengeka kuwa serikali haiwezi kufanikisha jambo lolote; lakini tunaiona mifano sasa, mashirika ya kichina yakiwa yameenea kila sehemu duniani yakifanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Sina tatizo na huku; ingawa najua hata wewe unafahamu kwamba ni uongo kudhani kuwa serikali haiwezi kusimamia na kuendesha huduma za mashirika kama hayo. China wametuonyesha mifano wazi kabisa.

Ninalokataa ni hili la kasumba ya kusema serikali haiwezi kufanya jambo, kama kusimamia uendeshaji wa shirika. Hii ni fallacy
Ndio haiwezi maana serikali inaangalia zaidi social benefits kuliko economic benefits. So hakuna incentive ya kufanya kazi. Hapa naongelea context ya Tanzania sio China maana wao wana mfumo tofauti kidogo.

Hata huko China unapotolea mfano bado private sector ina dominate uchumi n.k so hakuna sehemu duniani ambapo serikali imeizidi private sector kwenye kuchochea uchumi.

Nasema hivi sababu serikali haina competition so why should It deliver? TRA ina competitor? JWTZ? they have nothing to prove. Ila huko US kuna mpaka private military organisations zinalipwa kulinda watu na mali zao parallel na uwepo wa polisi!! So lazima na jeshi lao liwe up to date maana likizembea mikataba watapewa Blackwater kupambana vitani.
 
nyingi zikiwa ni hujuma toka kwa watendaji huko huko serikalini wakishirikiana na hizo kampuni binafsi.
Hii ni moja ya excuses mbovu sana eti kuhujumiwa are you serious?. Incompetence na kuhujumiwa wapi na wapi? Mfano baraza la uwezeshaji kiuchumi linahujumiwa na nani? baraza la maendeleo, sijui NIDA inahujumiwa na nani? Maana hizo ni monopoly sasa zikihujumiwa huyo anayehujumu wa kutoka private sector anapata faida gani?

Acheni excuses, ni sababu huko serikalini hakuna profit incentive hakuna shareholders, no Key performance indicators, hakuna accountability kabisa. Ila private sector unapewa targets kuwa fikisha wateja elfu 5 kila mwaka huwezi unatumuliwa ila huko TTCL wana wateja laki 3 kwenye industry ya wateja million 25 ila sijawahi sikia marketing officer katimuliwa!? Sasa hujuma hapo inatoka wapi?

Serikalini kuna incompetence maana hakuna mwenye mali ila mtu binafsi akiweka mtaji wake MD hawezi survive.
 
Tunaona Ethiopian Airlines iking'ara kabisa na kuingiza faida, lakini mifano kama hiyo hutaki kuitazama.
Ethiopian Airlines unadhani inaendeshwa kwa model yetu huku? Wao wanatoa tender hadi kwa makampuni ya foreign kufanya shughuli kama handling, management, marketing, flight operations etc sio kwamba ni serikali purely inasimamia kila kitu!! Watu wameshahama huko wanarely kwenye private sector yaani sio kila kazi ifanywe na ofisi kuu. Mfano marketing unaipa kampuni A, cargo handling kampuni B, Recruitment kampuni C, Flight operations kampuni D, sijui sales and marketing kampuni E.
 
Back
Top Bottom