Umesoma hio link ?
Isome uielewe, mifano ya hizo nch ndio kinachofanyika saiz Tz,
Basic huduma zinatolewa na serikali wakati bizness ni free market, kila mbuzi ale kwa kamba,
In short ili jamii iendelee kiuchumi ubepari is the way
Tatizo hujafika na kuishi kwenye usoshalisti kujua na ku-experience falsafa na maisha ya jamii ya kisoshalisti ikoje.
Fika Kenya, fika South Afrika na fika Marekani kwenye jamii za kibepari ambazo ni purely capitalist, Kenya, South Afrika hata Marekeni, masikini wanabakia kuwa masikini.
Marekani imewachukua muda mrefu masikini kuwa na mfumo wa bima ya afya, ilimhitaji Obama kuja na inclusive medCare (Obama care).
Watanzania huwa mnalaumu bila kujua misingi, tatizo sio usoshalist, ila misingi na falsafa yake inaigusa vip jamii.
Mfano, elimu ya bora na ya bure ni falsafa ya usoshalist. Karibu nchi zote za Nordic wana elimu bora kabisa; zinagharimiwa na kodi za wananchi.
Nchi kama hizi ambazo hujui kuna ubepari uchwara au usoshalist, unakuta waziri mwanae anasoma shule ya kibepari na ataiba hela tu ili mwanae asome huko, akijua shule za umma hakuna elimu bora.
Nyerere kaacha misingi ya shule za umma mpaka vyuo vya umma ndiko kulikuwa na uhakika wa elimu bora na jumuishi. Kutokae shule ya msingi mpaka chuo kikuu. Dhana ya wasio na uwezo wa kifedha kukopeshwa kwa dhamana ya serikali (umma) ni usoshalist.
Kwenye ubepari, ukiwa masikini, serikali ni ya matajiri na kwenye emerging economies matajiri wengi ni majizi na wapiga ma-deal na mifano ipo.
Usiwe mvivu, tembea, kaishi kwenye jamii za usoshalist; utaelewa exactly falsafa na misingi yao. Huwezi kukuta tajiri mkubwa kama Bill Gates Norway/Sweden, ila kuna utajiri uko shared na masikini hawapo na wachache sana. Nenda US, kuna Elon Musk na kuna watu wanalala barabarani, hawana uhakika wa kula na wamezaliwa na kukulia Marekani.