Tanzania tuna chuma lakini inashangaza tupo bize kukusanya skrepa

CCM imetuzuia kufikiri? Yaani nchi iliyojaliwa kuwa na madini ya chuma, lakini wananchi wake wapo bize kukusanya skrepa mitaani.

Yaani hawa waiba misalaba na Kengele za makanisani, au wang'oa vyuma vya madaraja na waokoto vyuma mitaani, kama madini ya chuma tuliyo nayo yangechimbwa wangeishi aina hii ya maisha!?
utakuwa umefeli intreview tra
 
Vyuma watachimba vizazi vinavyokuja, Kwa sasa ni kupita na bandari, ngorongoro na vile vinavyoonekana Kwa macho!
Kapewa mchina anataka kuchimba,kwa kasi ya uchimbaji madini ya wachina tza sidhani ndani ya miaka kumi ijayo tza itakuwa na madini yatasomwa kwenye historia.
Hawa jamaa Wanapiga kazi hatari kazi ya mwaka wanapiga kwa mwezi,wametumwa pesa aisee.
 
Mkataba maslahi ya Tanzania yamezingatiwaje?
 
Changamoto kubwa iliyopo ni watu wengi kuanzia wananchi hadi viongozi kuwa na fikra tegemezi (umasikini wa fikra).
Kila kitu wanategemewa wageni, wenyewe hatuwezi. Kuchimba making, gas, kuendesha bandari, kujenga barabara..... tuwape wachina, waarabu, wazungu...
Kizazi cha sasa hakijui maana ya Uhuru waliopigania wazee wetu.
Bahati mbaya hata wale wachache walioona harakati za Uhuru waliobaki wamejiunga kwenye huo upuuzi.
Mapinduzi ya fikra na hatimaye matendo ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi.
Nani alikuambia wazee wetu walipigania uhuru au walipigania maslai yao.
Walichojua ni kumuondoa mkoloni tu basi na sio baada ya mkoloni kuondoka tunafanyaje ndo maana miaka 60 Africa imekwama hatujui tuvae sketi au bukta tunaelea elea tu
 
chuma cha tanzania kina grade ya chini, ukilinganisha na urusi ukrane romania
Mbona mababu zetu waliweza kutengeneza mikuki imara kabisa ambayo ukikichoma kitoweo kinaanguka hapo hapo.
 
Na ilipo chuma yapo makaa ya mawe mzoga kapewa fisi ( mchina)anachekaje.
Kuyeyushia chuma ni rahisi sana kwa makaa ya mawe.
Wananchi eneo husika wajifunze kuyeyushia chuma kwa level ndogo ndogo wauze chuma viwandani makaa ya mawe si yapo.
Unaweza jenga vyungu vya udongo au matofari ya udongo kuyeyushia chuma Kwan wazee watu walifuaje chuma zamani kabla ya ujio wa wageni
 
chuma cha kutengeneza mkuki ni tofauti na chuma cha kutengenezea engene.
 
Engene ndiyo nini. Hata kama ulitaka kumaanisha "Engine" bado unatakiwa utuambie utofauti wake unatokana na nini?
 
hiyo ni shule ingine mkuu, sio kila chuma kinafaa kila mahala, inategemea na atomic tracture ya kila ferric compound
 
chuma cha kutengeneza mkuki ni tofauti na chuma cha kutengenezea engene.
Engine inamchanganyiko wa vyuma ina cast iron kwenye crank shaft aluminium kwenye pistons nk.

Hichi chuma chetu Engine block kinafaa.
 
hiyo ni shule ingine mkuu, sio kila chuma kinafaa kila mahala, inategemea na atomic tracture ya kila ferric compound
Sasa wewe unaijua *Structure" na hiyo "ferric compound" ya huko Liganga?
 
Na ilipo chuma yapo makaa ya mawe mzoga kapewa fisi ( mchina)anachekaje.
Kuyeyushia chuma ni rahisi sana kwa makaa ya mawe.
Wananchi eneo husika wajifunze kuyeyushia chuma kwa level ndogo ndogo wauze chuma viwandani makaa ya mawe si yapo.
Unaweza jenga vyungu vya udongo au matofari ya udongo kuyeyushia chuma Kwan wazee watu walifuaje chuma zamani kabla ya ujio wa wageni
Ndio maana Lissu aliwambia nyie watu wa Mbinga, babu zenu hawakwenda shule kama nyie lakini walikua akili kuwazidi.
Unapewa chuma unapewa makaa ya mawe tena karibu alaf unaomba msaada kwenye nchi za jangwani.
🤷🏿‍♂️
 
Wakaona wamdake!
 
Nani alikuambia wazee wetu walipigania uhuru au walipigania maslai yao.
Walichojua ni kumuondoa mkoloni tu basi na sio baada ya mkoloni kuondoka tunafanyaje ndo maana miaka 60 Africa imekwama hatujui tuvae sketi au bukta tunaelea elea tu
Baada ya Uhuru, maneno na vitendo vyao vilionesha kuunganisha na kuwaendeleza wananchi wote bila ubaguzi.
Zile fikra na matendo zingeendelezwa sasa hivi matokeo yangekuwa maturity sana.
Sasa hivi ubinafsi unaosababisha kujipeleka utumwani kwa wageni umekuwa sera.
 
Back
Top Bottom