Tanzania tuna chuma lakini inashangaza tupo bize kukusanya skrepa

Tanzania tuna chuma lakini inashangaza tupo bize kukusanya skrepa

Sasa wewe unataka kusema chakula kinacholiwa mezani na makombo ni sawa?

Skrepa unawezaje kuifananisha na chuma Cha kutoka mgodini? Wewe ndiyo unatakiwa ujishangae ni kwa nini unaona mgodi wa chuma na uokotaji wa skrepa mitaani ni mambo yanayofanana!
Inawezekana pia hujui unachokiongea.
 
CCM imetuzuia kufikiri? Yaani nchi iliyojaliwa kuwa na madini ya chuma, lakini wananchi wake wapo bize kukusanya skrepa mitaani.

Yaani hawa waiba misalaba na Kengele za makanisani, au wang'oa vyuma vya madaraja na waokoto vyuma mitaani, kama madini ya chuma tuliyo nayo yangechimbwa wangeishi aina hii ya maisha!?
Kwani kafulila na Kitila Mkumbo, madalali wakuu wa mali za nchi hii wanasemaje, mkuu 'Kilewela'?

Nchi imegeuzwa kuwa watu wategemezi au kufanyiwa, sisi wenyewe hakuna tunachoweza kukifanya!

CAG kila mwaka anatutangazia mabilioni ya shilingi ambayo matumizi yake hayajulikani; lakini hata mara moja hatuwezi kufikri kwamba ni pesa hizi hizi ambazo zingetuwezesha kujijengea uwezo katika mambo mengi sana badala ya kunadisha tu kila kitu.

Huo mradi wa chuma na makaa ya mawe ni kama zawadi toka kwa Mungu kutuwezesha kujenga viwanda vya kimkatati kwa ajili ya maendeleo yetu. Lakini ni kama Mungu naye alikosea kuweka vitu hivyo hapo kwa watu wasiokuwa na akili sawasawa vichwani mwao (soma viongozi).
Hivi vi-nchi, kama Uingereza viliweza kuinuka haraka sana kwa kuwa na mali ghafi kama hizo. Sisi leo hatujui maana yake, tunasubiri wachina waje kuvuna.

Inaudhi na kukera sana
 
Steel industry Ina siasa ya ajabu sn dunia hii, jichanganye km nchi kamwage pesa kwe mradi wa chuma uone, marekan mwenyew analia na faulo za china na Japan, c kwamba waafrica c ni wajinga hvyo ila waliotangulia washaweka mifumo ambayo inahitaji akili uvumilivu, siasa na mambo mengi sana kuiingia,
Sasa wakishaweka mifumo ndiyo nasi tuwe mazuzu?
Uko sahihi sana juu ya hao Marekani na China kuhusu zao hilo; lakini hiyo isiwe sababu ya sisi nasi kutumia vichwa kutafuta njia za kuendeleza mali ghafi zetu.
Kwa nini chuma itoke China kuja kujenga miundo mbinu ya usafiri Afrika nzima? Hata kama hatuwezi kushindana kwa kiasi cha hao wakubwa; kwa kiasi cha kati pia hatuwezi?
Kwa maana hiyo hiyo, unataka hata kuku wa nyama au mayai wafugaji wetu wasifanye, kwa vile Marekani anazalisha ziada na anaweza kutusambazia hapa kwetu kwa bei ya kutupa?
Hali iwe hivyo hivyo na Sato waliogandishwa toka uchina,wavuvi wetu hapa wasijishughulishe?

Tuachane na haya mambo ya kukaririshwa na hao hao wanaotaka sisi tuwe soko tu la kupokea takataka toka kwao.
 
CCM imetuzuia kufikiri? Yaani nchi iliyojaliwa kuwa na madini ya chuma, lakini wananchi wake wapo bize kukusanya skrepa mitaani.

Yaani hawa waiba misalaba na Kengele za makanisani, au wang'oa vyuma vya madaraja na waokoto vyuma mitaani, kama madini ya chuma tuliyo nayo yangechimbwa wangeishi aina hii ya maisha!?
Umesema kweli sana! Fisiemu ni laana kwa nchi hii!
 
chuma cha tanzania kina grade ya chini, ukilinganisha na urusi ukrane romania na iran, madini chuma yapo kila mahali hapa kwenye nyanya yapo tatizo ni kujua ukiprocess utapata faida?
Ungeweka tarakimu ingesaidia sana kulinganisha hizo 'grade', lakini naona ni maneno mengi tu bila ya ushadi mfupi tu wa kuonyesha unacho kizungumzia.
Wakusanya chuma chakavu na kutengeneza bidhaa zinazouzika kwa faida; lakini kupata bidhaa hiyo hiyo toka kwenye mali ghafi iliyopo ikawa ni hasara kubwa? Inahitaji maelezo makubwa zaidi ya hivyo vimistari ulivyo bandika hapo.
 
Sasa wakishaweka mifumo ndiyo nasi tuwe mazuzu?
Issue sio uzuzu, km tumejpanga sawa, haya mambo hayahitaji hasira. Tuko nyuma vitu vingi but why tuko nyuma? Hapa ndo nahis panatuchanganya Africa maana tunatumia sana hisia badala ya uhalisia
 
CCM imetuzuia kufikiri? Yaani nchi iliyojaliwa kuwa na madini ya chuma, lakini wananchi wake wapo bize kukusanya skrepa mitaani.

Yaani hawa waiba misalaba na Kengele za makanisani, au wang'oa vyuma vya madaraja na waokoto vyuma mitaani, kama madini ya chuma tuliyo nayo yangechimbwa wangeishi aina hii ya maisha!?
😀😀😀akili za kiafrika
 
Issue sio uzuzu, km tumejpanga sawa, haya mambo hayahitaji hasira. Tuko nyuma vitu vingi but why tuko nyuma? Hapa ndo nahis panatuchanganya Africa maana tunatumia sana hisia badala ya uhalisia
Na kwa njia hizi hizi kama maelezo yako yalivyokaa; ndipo tutakapotoka huko"nyuma" unakokuelezea wewe hapa.

Maajabu makubwa!
 
Back
Top Bottom