Tanzania tunajifunza nini kuhusu uchaguzi wa Kenya? Tubadilike

Tanzania tunajifunza nini kuhusu uchaguzi wa Kenya? Tubadilike

MWALLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2006
Posts
16,952
Reaction score
10,500
Naona vyombo vya habari vingi vinajifanya kama havina habari kabisa kuhusu uchaguzi wa kenya yaani wanachukulia kama vile uchaguzi wa kumchagua mjumbe nyumba 10 10.

Serikali y a CCM mnalo la kujifanza hapa msijifanye hampo na hamna habari, angalieni chaguzi ya Kenya inavyofanyika pamoja na mapungufu machache lkn unaweza ona jinsi uchaguzi ulivyokuwa umekubalika na wananchi wa kenya upo huru.

CCM jifunzeni kuendesha mambo kwa demokrasia wapeni uhuru wananchi wapeni uhuru vyama vya siasa vifanye shughuli zao kwa uhuru kanini mnakuwa waogamno kupitiliza?

Mnakuwa waoga mpaka mnakuwa kama wajinga. miaka 60 ya uhuru kweli mnaishi kwa style hii?

sasa jifunzeni kupitia uchaguzi huu wa kenya acheni kubana watanzania kujielezea kwa uhuru.

azamtv nimewaona wapo mjini nairobi hapa wakituhabarisha kwa uzuri sana

 
twajua KENYA wapo kwa kutekeleza Democracy. TZ kuna mechi gani hufanyika zaidi ya uchafuzi?
Ungekua ni mkenya unaezielewa siasa zao sawa ningekubali.............Afrika ni ile ile tofauti tu ni script ya movie nzima
 
CCM walisha zoea vya kunyonga, hawawezi zungumzia uchaguzi wa Kenya KWA jinsi unavyoendeshwa ndio changamoto haziwezi kukosa, wakenya wamepiga hatua kubwa Sana Katika ukanda huu.
 
Kenya ndio wanatakiwa wajifunze kutoka Tanzania namna tunavyobadilishana Madaraka bila ukabila wala kumwaga damu
 
Kenya ndio wanatakiwa wajifunze kutoka Tanzania namna tunavyobadilishana Madaraka bila ukabila wala kumwaga damu

Tanzania CCM inakaa madarakani kwa shuruti, bora hao wanaonadilishana kwa ukabila. Hapa Tanzania ni nchi ya makondoo watu wanaweza kutangazwa washindi kwa kura fake na watu wakakaa kimya.
 
CCM walisha zoea vya kunyonga,hawawezi zungumzia uchaguzi wa Kenya KWA jinsi unavyoendeshwa ndio changamoto haziwezi kukosa, wakenya wamepiga hatua kubwa Sana Katika ukanda huu
kwa jinsi hali ilivyo hivi tunashudia uchaguzi na sio uchafuzi wa kenya now .. hapa CCM wanautazama kwa jicho la pembeni wakidhani hatuwaoni wanavyouchungulia uchaguzi unavyoendeshwa kwa kufuata misingi ya ya demokrasi hili kwao ni aibu kubwa. hivyo tayari akili zao zinajishughulisha kuangalia ni njia gani watatumia chaguzi ijayo namna ya KUIBA TU mana wanajua kabisa wao kushinda kihalali huwa haiwezekani kwa maana watanzania pamoja na uzuzu wao wa kushindwa kujiamulia mambo yao lkn wanaweza kuitia aibu ccm angalao kwa kuijulisha kuwa hawaitaki hawaipendi.
 
Kenya ndio wanatakiwa wajifunze kutoka Tanzania namna tunavyobadilishana Madaraka bila ukabila wala kumwaga damu
kijana hivi huoni hat aibu kuongea hizi maneno.. lkn sio kosa lako mana umeshalishwa ujinga wa LUMUMBA kubadilika wewe ni shida kubwa
 
Ungekua ni mkenya unaezielewa siasa zao sawa ningekubali.............Afrika ni ile ile tofauti tu ni script ya movie nzima
Acha kupotosha.Kenya wapo dunia ingine katika mambo ya siasa na chaguzi.Ndiyo maana vyama hubadilishwa kwa sanduku la kura.
 
Back
Top Bottom