PETER THE ROCK
JF-Expert Member
- Feb 17, 2014
- 528
- 807
Mawazo ya kujenga haya. Hii mitandao ingekuwa inatumika kushauriana hivi tungekuwa mbali sana. Nakushukuru sana mleta uzi.Umeelezea vema,tunaishi nchi ya sifia sifia tu,wataalaam wetu wote wameokotwa jalalani,kituko cha RPC Dodoma eti ataanza to escort buses zinapoingia mkoani kwake!ni kichekesho kitupu,we need to be serious hapa hii T1 ni uchafu mtupu hasa Mbeya to Tunduma,Dar to Mikumi ,hii barabara inabidi tuijenge upya sio kuitia viraka!life span ya barabara hii imeshapitwa na wakati,hii barabara imejengwa Nyerere era,inabidi tuipanue hasa pale Mikumi National park ikiwa ni pamoja na kusafisha vichaka vyote 20m both sides (faida yake tutapunguza wanyama wadogo kuwa maeneo karibu na barabara),Kitonga Pass tuweke njia mbili pale,Chimala to Mbeya papanuliwe na njia hii ichepushwe isipite katikati ya Mbeya.Natamani waziri wangu wa mawasiliano afanye utalii wa kikazi kwa barabara,aanzie N1 from Beitbridge to cape town,then N7 from Cape town to Namibia border,pale achukue B1 to windhoek,then aruke kwa ndege to Gaborone pale akamate A1,A2 na A3 towards kazungula,definitely akirudi Dar ataona tofauti kubwa kati yao na sisi.
Binafsi mapendekezo yangu ni mawili:
1.Makusudio ya awali ya kuanzishwa TANROADS yazingatiwe na uendeshaji wake pia uwe katika kiwango cha kimataifa, tusirudi tena kwenye kuiendesha kisiasa. Huu ndio ugonjwa mkubwa wa nchi yetu kwa institution kadhaa ambazo ni nyeti kwa maendeleo yetu: proper governance.
2. Tuwakodi na kuwapa tenda mabingwa wa ku design miondombinu, Wachina, watusaidie kupendekeza namna ya kufupisha na kukiweka sawa kipande kile cha maili 8 cha Mlima Kitonga. Likitokea tatizo pale njia mbadala kutoka Kusini Nyanda za Juu, Malawi, Zambia na sehemu ya DRC kuja bandarini Dar ni kuzunguka kupitia Dodoma ambako tena unakutana na mtihani mwingine wa mlima Nyang'oro! Wajapan hawakutengeneza Kitonga kwa ajili ya miaka mingi ijayo. Tusahihishe hizo maili 8 tu!