Ukisoma historia ya Tanzania, Mwalimu J.K Nyerere alipata tabu sana kuwafundisha Watanzania dhana ya uraia.
Nyerere alisimamia uraia wa Tanzania kama kitu ambacho mtu ambaye hata si mzawa anaweza kuwa nacho, kwa kiapo.
Jambo hili lilimletea upinzani mkubwa kutoka kina Christopher Kassanga Tumbo, na hata jeshini.
Mpaka akaletewa jaribio la mapinduzi na wanajeshi mwaka 1964. Akavunja jeshi na kuliunda upya kwa aibu kubwa.
Mpaka Nyerere akafanyiwa uasi na wanajeshi ambao hawakutaka kuongozwa na watu wasio wazawa.
Professor Paul Bjerk kaandika vizuri sana katika "Building a Peaceful Nation: Julius Nyerere and tge Establishment of Sovereignty in Tanzania, 1960 -1964".
Ukisoma utaona kabisa Nyerere alivyopigania uraia wa Tanzania uwe na maana kubwa zaidi ya uzawa, na jinsi Watanzania wengi walivyokuwa hawajaeleea hilo somo.
Na mpaka leo, bado hawajaelewa hilo somo.
Wanaona mtu akizaliwa nchi nyingine, au akiwa na wazazi waliozaliwa nchi nyingine, hawezi kamwe kuwa raia wa Tanzania.
Xenophobia tu.