Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Wanamichezo watatu wa Tanzania walioko Paris kwenye michezo ya 33 ya Olimpiki ya majira ya joto ya Paris 2024 wameendelea na mazoezi makali chini ya makocha wao, wakijiandaa kwa michuano yao inayoanza rasmi kesho Jumatatu Julai 29, 2028.
Tanzania itatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano hii ya 33 ya Olimpiki ya Majira ya joto leo Jumatatu Julai 29, 2024 wakati mchezaji wake wa Judo, Andrew Thomas Mlugu, atakapopanda ulingoni kupambana na William Tai Tin, judoka kutoka nchi ya Samoa. Mpambano wao utakuwa saa 5 asubuhi kwa saa za Tanzania. Huyu Tai Tin anatoka Siumu na Kisiwa cha Manono lakini anaishi Melbourne, Australia, na alikuwa sehemu ya timu ya Samoa katika Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2022 huko Birmingham, umri wake ni miaka 39.
Andrew Thomas Mlugu ni Judoka maarufu nchini huku pia akiwa ni muajiriwa wa Jeshi la Magereza, kiufupi ni askari wa Jeshi la Magereza, na hii inaendelea kutengeneza dhana ya kuwa serikali inatoa motisha tu kwenye majeshi, mfano, JWTZ, Magereza pamoja na Jeshi la Polisi (Sio kwa ubaya). Tukumbuke kuwa Mlugu aliongozana na msafara wa Tanzania katika kushiriki katika Olimpiki ya Majira ya Joto ya 2016, ambapo aliwakilisha Tanzania katika mchezo wa Judo. Mlugu akishinda bado ana kibarua kizito kwani atasubiria mshindi kati ya Lasha Shavdatuashvili kutoka Georgia dhidi ya Mfaransa Joan-Benjamin Gaba.
Siku ya pili, yaani Jumanne Julai 30, 2024 Tanzania itatupa karata yake ya pili wakati muogeleaji Collins Phillip Saliboko, atakapoingia bwawani kushindana katika mita 100 (Freestyle) kwa wanaume mnamo saa 6:15 mchana kwa saa za Tanzania. Kesho tutapata wasaha wa kumtazama kijana wetu, Collins Saliboko akichuana kutafuta nafasi ya kuingia nusu fainali, huyu naye ana kipengele haswa kwani anakwenda kukutana na mashine ya kupiga mbizi, watu kama, Maxime Grousset dogo janja tu ambaye ameanza kucheza na maji toka akiwa na miaka mitano. Saliboko ana kibarua kweli kwani, ukiachana na Grousset pia kuna chuma kingine Matthew Richards, Gen Z mwenye moto wake wa kutisha sana, bila kumsahau Jack Alexy.
Karata ya tatu ya Tanzania itatupwa Jumamosi Agosti 3, 2024 na mwogeleaji Sophia Anisa Latiff ambaye atashindana katika mita 50 (Freestyle) kwa wanawake mnamo saa 6:00 mchana kwa saa za Tanzania. Tukimzunguzia Sophia huyu ni Mzaliwa wa Uingereza, na baadhi ya watu hudai kuwa ni kama tulikwenda kupiga upatu wa jina la Uzalendo baada ya huyu binti kuonesha makali kwenye kucheza na maji, kupiga mbizi kwa dakika moja na sekunde 44 kwenye michuano ya 14th CANA African Junior Swimming and open water Championship ya mwaka 2021.
Mashindano haya ndio yaliyompa umaarufu mkubwa kwani alishika nafasi ya 14. Ila anakwenda Olimpiki kukutana na wajuvi haswa, wadada wenzake wanatembea kwa dakika moja na sekunde 10, hivyo ajiandae vyema maana anakwenda kukutana na wadada walio bora haswa, Mélanie Henique, bingwa wa kuogelea kutoka Ufaransa, pamoja na mercenary mmoja, Simone Manuel kutoka Marekani, wadada waliotumwa medali ya dhahabu.
Karata nne za mwisho za Tanzania zitatupwa na wakimbiaji Marathon, ambao watawasili Agosti 7, wakitokea kambini Arusha moja kwa moja, tayari kwa mbio hizo zitazokuwa Agosti 10 na Agosti 11, 2024. Safari hii mfumo wa michuano ya Marathon umebadilishwa, ambapo tofauti na ilivyozoeleka, wanaume ndio wataanza kukimbia na wanawake ndiyo watamalizia.
Tanzania tuna wakimbiaji wa Marathon kwa wanaume, yaani nahodha Alphonce Felix Simbu - nahodha na Gabrield Gerald Geay watashindana mnamo Agosti 10, 2024. Simbu pamoja na Geay wanakwenda kukutana na vipanga haswa, watu kama Bashir Abdi, Kenenisa Bekele, pamoja na Emile Cairess. Wapambane wapate hata medali ya shaba au fedha wajameni.
Wakimbiaji wa Tanzania wa Marathon kwa wanawake, Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri wamepangwa kukimbia Agosti 11, 2024, ambayo ndiyo siku ya mwisho ya Paris 2024 Olympics, na wao wajiandae maana kuna wadada wanafukuza upepo balaa, Alemu Megertu, Amane Beriso Shankule pamoja na Calli Thackery ambaye mwaka 2024 huu amefanya mabalaa yake kwenye mbio za 2024 European Half-Marathon Cup pamoja na women's half Marathon at the 2024 European Athletics Championships.

Kila lililo na heri kwenye michezo yenu! Uzalendo kwanza! Tanzania Kwanza.