Wachina juzi kule kwao wamesherehekea ufunguzi wa train yenye very high speed. high speed trains ni za muda mrefu china na zinasaidia sana nchini china, nilikuwa najiuliza, watz tunashindwa nini kuzielectrify train zetu zitumie umeme badala ya mafuta na ziende kwa kasi, ziongezwe njia pia?
angalia kwa mfano: TAZARA tayari ipo imejengwa ni kiasi cha kutandaza mfumo wa umeme toka dsm hadi kaprimposhi zambia. Reli ya Kati ipo, kilichobaki ni kutandaza umeme toka dsm hadi kigoma na mwanza tu. reli ya toka dsm hadi Tanga na Tanga hadi moshi arusha ipo, ni kiasi tu cha kutandaza umeme na vitu vinaanza kufanya kazi. badala ya watu kutembea kwa train kwa siku tatu njiani, wanatembea kwa siku moja au pengine masaa tu wamefika kigoma.
tunashindwa nini? kwasasa japani wameshajiunga na ndugu zetu wa kusini/mozambique hadi wamewapatia dola milioni miasaba na wameomba kuwa rafiki yao kwasababu ya gas na mafuta. china imechagua tz kwasababu ya urafiki wa kihistoria na kwasababu ya mafuta na gas. pengine bomba likifika dsm tukafua umeme pale kinyerezi umeme wanaosema tutakuwa nao mwingi kiasi cha kuuza nchi za nje(nje za nchi) tutatumia umeme huo wa ziada kuifanya train system yetu itumie umeme na kuwe na speed ya usafirishaji wa mizigo, kama mzigo ukishushwa dsm leo asubuhi ufike kigoma au mwanza baada hata ya masaa kumi na mbili. inawezekana, badala ya masiku mengi na kwa malori yanayoharibu barabara zetu.
NI MUHIMU SANA KUBORESHA MIUNDO MBINU YETU HASA RELI NA BANDARI, barabara tumeshajitahidi tuhamishie nguvu kwenye bandari na reli tuone.
pia nashauri TUJENGE BANDARI KAVU KUBWA SANA PALE KAGONGWA AU ISAKA KAHAMA ambapo itufanya mji wa kahama uungene hadi Tinde pale toka kahama mjini. kwa mzunguko wa pesa wa kahama kwenye migodi ambao inakadiriwa kuisha miaka zaidi ya hamsini ijayo, na mzunguko wa bandari kavu, eneo lile litakuwa eneo la kibiashara sana. na nilisikia wanajenga kituo cha uwekezaji pale kahama/isaka (kwa wale wenyeji wa kule wanapaelewa). Mungu ibariki tz ifikie mafanikio haya. KIKWETE, TUNAHITAJI TRAIN ZA KUTUMIA UMEME ILI ZIENDE HARAKA, HII INAWEZEKANA KWASABABU UMEME TUTAKUWA NAO. hakuna linaloshindikana hapa duniani. south africa zipo, morroco zipo, tz tunashindwa nini?
halafu, kwanini ile reli/train toka KIA kule moshi hadi arusha isiboreshwe na itumie umeme pale ili watu tuishi maisha ya kisasa, tutaishi maisha ya kuona kama hatutaweza hadi lini jamani? tupeni sisi wengine uongozi muone kama nchi hii itabaki kama ilivyo. MUNGU IBARIKI TZ, MUNGU IBARIKI MIUNDOMBINU YA TZ.