Tanzania tupate High Speed Train, Wachina watajenga!

 Tanzania tupate High Speed Train, Wachina watajenga!

Kujenga high speed train lazima kuwe na vitu vya kuwahi kwanza, sio unajenga high speed train wakati watu hawawezi kumudu nauli yake haswa kwa sababu uchumi mdogo.

Jenga uchumi, uchumi ukifikia sehemu ya kuhitaji high speed train tutajenga.

Mmarekani na ujanja wake wote high speed trains zimemshinda/ kaziona hazina tija.Ukiondoa hiyo Acela ya Boston/DC ambayo is the steam engine locomotive of high speed trains.

Sio tunataka kuiga tu.

Tuna uchumi mdogo na hayo ma project ya high speed train yanataka sio tu mabilioni ya fedha kuanzia, bali ni high maintenance, yanagharimu sana ku maintain, ajali zake mbaya sana (angalia ajali ya Shanghai Beijing line ilivyokuwa mbaya).

Hiyo mi treni yetu tu inatushinda, unataka twende kwenye high speed trains?

Hujaweza kutembea unataka kukimbia?

Ukiwauliza Watanzania kero kubwa kwao ni nini, kutokuwa na high speed trains hakumo hata kwenye top 10.
 
Kwa hiyo wewe unafkr mwandishi sio muelewa? Punguani weweee hivi vitu ni vya kawaida na vinawezekana hata hapa Tz. Acha kufkr kama kizamani

Mkuu mbona unamshambulia sana watu8? yy amesemea uhalisia wa NCH yetu 50yrs Bado tunajadili km Inawezekana au la! 2we wakweli ikiwa hii TRAIN MANUAL ina2shinda kurekebisha miundo mbinu kwenda KIGOMA zaidi wk NJIA mbovu na Wizara inapeleka Bajeti Bungeni kila mwaka na hakuna kinachofanyika Huoni km mleta mada kaja na maneno ma2pu?
 
Mawazo ni mazuri. Kwa Hawa magamba serikali zao hawawezi.
Labda Magwanda Wakipewa Nchi wataweza pamoja na kuhalalisha Gongo.
 
Acha ushamba wewe watakufaje? Sasa nkt umeme utawekwa kwa juu ya treni..mpk huko juu unaenda kutafuta nin sasa??

Mkuu mwenye wasiwasi na UMEME anzungumzia khs kukatika Hujawahi kuona au kuckia watu wamekwama kwenye LIFT ni vipi UMEME ukizima wakati chombo ndo kiko kwenye mwendo ukichukulia hili shirika lakuasmbaza GIZA halina utaratibu wakutangaza mapema! Watz 2natamani sana mambo mazuri lkn nackitika kuna Baadhi ya watu zaidi ya 50yrs nw! bado hawajamjua ADUI duh,,,!
 
mbona nchi nyingine haziuwi mzee na wanatumia umeme kama wa kwetu tu. una maana kwamba umeme kukatikakatika, si yatakuwepo majenerator special automatic kuwaka umeme ukikatika, na kituo cha umeme wa train kinakuwa tofauti na vituo vya umeme huu wa majumbani etc. inawezekana.
Wishfull thinking
 
Mkuu mwenye wasiwasi na UMEME anzungumzia khs kukatika Hujawahi kuona au kuckia watu wamekwama kwenye LIFT ni vipi UMEME ukizima wakati chombo ndo kiko kwenye mwendo ukichukulia hili shirika lakuasmbaza GIZA halina utaratibu wakutangaza mapema! Watz 2natamani sana mambo mazuri lkn nackitika kuna Baadhi ya watu zaidi ya 50yrs nw! bado hawajamjua ADUI duh,,,!

Eti shirika la kusambaza giza, umenichekesha lakini unayosema ni kweli.

Hatuwezi kusema tunataka treni z akasi wakati hatujui hata umeme unaotakiwa ukoje, gharama yake ikoje, tunaweza kuumudu, je hata kama tunaweza kuumudu haya ndiyo matumizi mazuri kabisa ya fedha zetu chache za kigeni etc etc.

I mean tuna matatizo kibao, maji, elimu, afya, barabara, huo umeme tu hatuna wa kutosha, leo hii unataka treni za mwendokasi.

Kuwahisha nini hasa kinachohitaji kupelekwa kwa kasi ambacho sasa hivi hakiwezi kusafirishwa kwa ndege, mabasi na treni za kawaida?

Dagaa wa Kigoma?
 
Heading ilinipa matumaini nikajua moja kati ya ile mikataba 27 umevuja na kazi inaanza ASAP,hayo mawazo tunayo watanzania wengi hata baadhi ya viongozi pia, tatizo watendaji/watekelezaji vitu kama hivyo hawana mamlaka ya kuamua/kutolea maamuzi
 
Tuwape maji safi..elimu na huduma bora za afya wa tz kwanza....hio miradi mikubwa isubiri kwanza ni mawzo mazuri
 
Ccm ni janga la kimataifa angalia watu wanavyokufa bahari ya hindi almost kila mwaka sasa.uongozi finyu ndio matokeo yake haya. Hawa wanafikiri ni wao wenye uwezo wa kuongozza na kuwafanya watanzania waendeshe nchi yao chini ya kiwango kuliko intrinsic value yao ilivyo. Hapa tuna engineers wa kumwaga wa viwango vya kimataifa na hili jambo wanauwezo nalo lako ccm ni janga jamnai sio uongo. Wanaccm hawataki kufikiri nje ya kibox chao. Tunasema tuwe na serkali za majimbo kugatua madaraka hamtaki mnaleta local government zinazotegemea central government by 95% nawaambia hatutoki hapa hadi yesu arudi atatuacha vilevile. Kama akili za wabunge na madiwani dar. La saba zitaendelea kuongoza maprofesa, madokta masters holders na level zingine za juu basi tusitegemee mabadiliko hapo. Watu wasio na weledi watatwezaje kufanya maamuzi makubwa ya kisayansi ya kuendesha nchi? Ni kosa kubwa kufikiri siasa haihitaji elimu huu ni mtizamo wa kibongo usio na mashiko kimataifa.
 
Tanzania haina mweyewe ina watu baki kwa kuwaza na kutenda mambo ovyo ovyo kama ya wapita njia,hata ipite miaka 100 hatutasogea mbele kwa kasi,kwani kila mbongo ajifanya anajua tatizo na jinsi ya kutatua tatizo,lakini mwisho wa siku ni sifuri au chini ya sifuri.
 
Tatizo kubwa ni mambo yetu mengi tumeingiza siasa kwa asilimia 99,hivyo tukiamua kuondoa siasa kwenye utendaji wetu vyote vya wezekana.Ili barabara zetu zisiharibike mapema ni vyema kutumia treni badala yake.Na kwa sasa hakuna uhakika wa hata hiyo treni ya kizamani yenye mwendo kama jongoo sababu tu ya siasa.Twaweza kufanya vizuri zaidi na uwezo tunao lakini kinachoharibu hapa ni siasa, rushwa,ufisadi na zile % tu.
 
Umegusa ninapopataka siku nyingi.

Utauaje Bandari ya nchi kavu Isaka af unacreate inconviniencies za mifoleni Dar????
Malori yote yangekuwa yanaishia Isaka na kurudi Kigali na Mwanza.

Sasa kwa kifupi kazi bado ipo.
 
Wachina wameichagua Tanzania siyo kwa sababu za urafiki wa muda mrefu bali tuliingia kwenye kumi na nane zao tukauziana mtoto kwa nchi!
 
Idea nzuri saana hiyo Mkuu, lakini kwa uongozi huu wa Ccm hakuna kitakachofanyika.Tutaishia kuonea gere maendeleo ya nchi jirani.

Reli zetu haziwezi kustahimili speed ya juu. Zinatakiwa zijengwe upya katika ubora unaotakiwa. Vilevile mabehewa yanaotakiwa kwa speed ya juu siyo haya tulionayo, yanaspecial design kwa ajili hiyo.
 
Ndg yangu usiogope. twaweza kukuona kama mwota ndoto lakini ni ndoto inayowezekana. Tatizo ni ahadi hewa za hao walioko madarakani leo.
Angekuwa ameanza mpaka hata Morogoro tu huko kwingine akawaachia wengine bado angekuwa na cha kujivunia kwenye sera zake.
Wanatuonesha barabara ya lami kutoka Dar mpaka Mwanza. Sawa, lakini ni mizigo kilo ngapi itapitia hapo kwa siku hiyo barabara idumu?
Reli walioua ndiyo ingekuwa mkombozi wetu leo. Viongozi mliopo madarakani, timizeni ndoto kama hizi. Miongoni mwa mikataba 19 ya haraka haraka na siri, je huu wa treni ya mwendo kasi ipo? Onyesheni mfano hata kwenye hizo reli za Mwakiembe kutoka central mpaka Ubungo maziwa jamani.
Naililia Tanganyika yangu tu. Mungu halali wala hahongwi. Kuna siku ataingia kichaa Ikulu awezeshe haya mambo.
 
Nimekuwa nikushuhudia misururu ya mamia ya malori maeneo ya mizani toka Kibaha hadi Makambako, Chalinze hadi Mwanza n.k. achia mbali mamia nayopishana nayo njiani ambayo hayajafika mizani. yote yana usajiri wa T xxxx YYY. maana yake yamesajiliwa Tanzania na ni ya Watanzania, maana yake watanzania kwa maelfu wamejiingiza ktk biashara ya usafirishaji, hawa ndio tunapigania waondolewe ktk biashara zao badala yake Treni zifanye kazi hii! yaani tuwarudishe ktk umaskini baada ya ukombozi huu waliousotea!
 
Kitu unachosema ni kinawezekana hapa Tanzania lakini tatizo ni kuwa tumekuwa na vipaumbele vingi kiasi kwamba tunakosa 'focus'. Tunahitaji kuwa na vipaumbele vichache vya msingi na kuvisimamia barabara.Mfano tunaweza kuwa na Miundombinu (Reli, barabara, viwanja vya ndege na bandari), Elimu (awali,msingi, sekondari,vyuo) , Huduma za afya na Maji.Treni ya umeme inahitaji miundombinu ya kipekee hivyo inahitaji fedha. Jinsi Wachina wanavyokuja kwa ajili ya rasilmali zetu na sisi pia inatakiwa kujiuliza tunahitaji kitu gani Wachina watufanyie ili nasi kama nchi tunufaike (win-win). Mfano tunaweza kuwauzia mgodi wa chuma kwa makubaliano ya wao kutujengea miundombinu ya treni ya umeme na treni yenyewe kati ya Dar na Morogoro, au Dar na Arusha n.k.
 
Back
Top Bottom