Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Mimi dingi mkubwa alikuwa mtumishi akafikia level ya ukuu wa idara, baadae akawa professor kabisa anapigisha mapindi chuo na kuandika miradi akastaafia huko. Ila maisha yalikuwa mazuri sana tu mbona gari 5 uwani watoto kasomesha shule za maana kisha chuo kasomesha Canada wote hakuna aliesoma chuo cha umatumbini 🤣🤣🤣 so inategemea ni level gani mtu kaajiriwa. Ajira sio mbaya ukiwa upo kwenye level zenye maslahi.Mimi kwa experience yangu ya maisha naona wafanyabiashara wengi maisha nyumbani mazuri, wakati tupo wadogo ukiingia tu sebuleni kwa mfanyabiashara una notice utofauti na kwenu au nyumba za waajiriwa, nyumba za wafanyabiashara huwa zina vitu excess yani sebuleni kuna accessories ambazo muajiriwa ngumu kuwa nazo, nje usafiri wa kutosha alafu mara nyingi nyumba huwa wamejenga wao sio kupanga. Watoto wapo private schools
Tuseme tu ukweli wafanya biashara wengi japo wanaweza kuishi na stress sana ila maisha yao ndio hasa maisha ya mtanzania wa kipato cha kati, watumishi wengi (sio wote) sebuleni utakuta Tv nchi 32-43 , fridge na radio, sofa set moja na nje gari sana sana moja,wachache wana mbili basi, lakini nyumba za wafanya biashara madude mengi, huko nje gari nne na kuendelea
Ni mbaya tu kama uko kwenye level za laki 3 kwa mwezi.