kaka tutakuletea uji asubuhi na mkate na soda jioni wala usihofuAlieajiriwa kama anapata mshahara mkubwa na madili ya hela ndefu mtu aliojiajiri sio rahisi kumkuta. We imagine mtu kama Makamba kalamba uwaziri wa Nishati, Salary tu ni zaidi ya 200M kwa mwaka. Bado ajagusa deals za Billions za kutosha.
kwa hiyo ukiajiriwa ndiyo hard work inatosha? kwahiyo Mwenyezi Mungu anatoa bahati kwa waajiriwa tu na si kwa wanao jiajiri??? Hamna eneo lenye kujuana na connection kama kuajiriwa, siyo serikalini au private!! utafanya kazi mpaka uchakaee, unashangaa wezi, wavivu, wazembe ndiyo maboss zako.Sio kwamba watu hawapendi kua matajiri
Ingekua hivo hapa jf kila mtu angekua safi,kua tajiri ni ngumu, pia inachangiwa na bahati na connections,hard work pekee haitoshi 🙆
Aliyejiajiri leo ndo huyo huyo atakuja kuajiri kesho kwa hiyo huwez kumtoaa Aziz kwenye discusion sabb ametokea kwenye kujiajiri mpka kuajiriNi kweli. Ila Aziz hajajiajiri, Ameajiri. Kuna tofauti hapo.
Mada inazungumzia Waliojiajiri, haizungumzii Walioajiri watu.
Ni moyo hauendi mbio au ni akili inakua imelala na kurubiri kulishwa kama kuku wa broiler mwisho wa sku ukaliwe nyama.Ukiajiriwa moyo hauendi mbiyo sana kama kujiajiri[emoji38][emoji38][emoji38]
Basi kua tajiri kama ni rahisi na hardwork yakokwa hiyo ukiajiriwa ndiyo hard work inatosha? kwahiyo Mwenyezi Mungu anatoa bahati kwa waajiriwa tu na si kwa wanao jiajiri??? Hamna eneo lenye kujuana na connection kama kuajiriwa, siyo serikalini au private!! utafanya kazi mpaka uchakaee, unashangaa wezi, wavivu, wazembe ndiyo maboss zako.
Waliojiajir wakafanikiwa ni 10 katika mia au 1000. Yaani wengi waliojiajiri wamepigika na ni watu wanaoishi kwa magumashi. Ukiwataiti kidogo tu hawapumui rejeeni kopindi cha JPM alipo bana ukwepaji wa kodi na ujanja ujanja.Duuh yaani uajiriwe serikali ya ccm afu uvimbe ujiringanishe na aliejiajiri....hilo ni moja ya matatizo ya waajiriwa serikalini..
...waajiriwa wa serikalini matokeo hasi ya kuajiriwa serikali wanayapata wakisha staafu...angalia wastaafu wengi wa serikali majibu utayapata
....kwenye kodi waajiriwa serikali wananyonywa sana na serikali na hawana option...
Ukweli .mtu acha nijitafakari juu ya hi biashraa yangu wacha nirudi job Tena kwa speed kubwaIkiwa alieajiriwa Serikalini na aliejiajiri wote wanaingiza kipato sawa kila mwezi
1. Aliejiajiri anaondoka kwake asubuhi kurudi hadi usiku, alieajiriwa Serikalini anaondoka asubuhi anamaliza kazi zake jioni na bado huko ofisini kuna muda anapata kufanya mambo yake.
2. Aliejiajiri anaweza asizijue weekend lakini alieajiriwa Serikalini anapumzika Jumamosi na Jumapili.
3. Aliajiajiri hana sikukuu za kiserikali, alieajiriwa Serikalini haendi kazini idi (hata kama ni mkristo), mwaka mpya, Mei mosi, sabasaba, siku ya Nyeyere, siku ya uhuru, mapinduzi, nanenane, idi, pasaka, n.k
4. Aliejiajiri akiumwa inabidi ajikaze aende tu lasivyo kipato kinaweza kutikisika, alieajiriwa Serikalini akiumwa anatoa notisi.
5. Aliejiajiri hana likizo, muajiriwa ana likizo siku 30 kila mwaka.
6. Aliejiajiri anaweza kufilisika endapo duka likiungua, akiumwa kwa muda mrefu, akiibiwa, n.k. alieajiriwa Serikalini nafasi yake na mshahara wake ni uhakika
7. Aliyeajiriwa Serikalini ni rahisi kukusanya mtaji, mkopo anapata kwa masharti nafuu sana na kwa haraka sambaamba na kudunduliza mshahara
8. Alieajiajiriwa na Serikali ana muda mwingi wa kuwa na familia yake kuzidi aliejiajiri. ikifika jioni, weekend, sikukuu za serikali, likizo, n.k. ana muda wa kutosha wa kuwa na familia yake
9. Alieajiriwa Serikalini anaweza kuwa ma biashara zake za kumuongezea kipato, hizi biashara zinaweza kumtunza baada ya kustaafu na watoto wake kuzirithi, Mifano ni kina Robert Kiyosaki mwenye kitabu cha Rich Dad Poor dad, Vunja Bei, Marehemu cpa Mengi, n.k. walianza kwa kukusanya mitaji wakiwa wameajiriwa.
Mwisho niseme Kujiajiri watu wanameki bingo lakini ni wachache, wengi wanaanguka na wengine wapo pale pale miaka nenda rudi. wachache wenye wenye roho ngumu, ubunifu, juhudi, kujibana, uvumilivu na connections ndio wanatoboa.
Umemaliza [emoji1787][emoji1787]Ukifa mtoto wako ataendelea kupokea mshahara wako?
Hao kina Sandaland, Sanga Store na Vunja bei wafananishe na kina January Makamba, Mwigulu etc.Huyo dingi yako mkubwa mfananishe na sanga store,vunja bei na sandaland usiwafananishe na wauza chips.
Wauza chips wafananishe na walimu wa Certificate diploma wanaopokea chini ya laki 5
Bei ya unga ikipanda au bidhaa yyte anaelalamika silimia kubwa waajiriwa serikalini na ndo wanaoumia.....coz bidhaa ikipanda na mfanyabiashara nae anaongeze bei kazi kwa mlaji wa mwishoWaliojiajir wakafanikiwa ni 10 katika mia au 1000. Yaani wengi waliojiajiri wamepigika na ni watu wanaoishi kwa magumashi. Ukiwataiti kidogo tu hawapumui rejeeni kopindi cha JPM alipo bana ukwepaji wa kodi na ujanja ujanja.
Walio ajiriwa wanaweza fanya yale ya mtu alie jiajiri mfano ufugaji, kilimo, biashara, utaalamu nk.
Matajiri ni wale walio jiajiri ila sio wengi kivile.
Watu we gi ni wabangaizaji na ndio walalamishi kwa serikali. Bei ya unga ikipanda kidogo tu wanahamaki.
Acha basi.. mtu analipwa 1m halafu pensheni 45m inawezekanaje hii?Halafu jamaa amejizima data na kusahau kwamba hako ka mshahara kake ka milioni 1 hakatampatia pensioni nzuri. Amejitahidi sana 45m. Akistaafu atanza kutapatapa kutafuta kujiajiri na kwa vile hajui ABC za kujiajiri pension yote itateketea na ataanza kuugua BP mara stroke mwisho wake amedanja mapema!
Mshahara wa DC au RC inajulikana na haiwezi kumfanya mtu awe tajiri, labda kama ameiba au kutumia madaraka yake vibaya..Makonda alikuwa mwajiriwa wewe unamzidi utajiri?
Mimi nimekulia Kijijini Kule Watoto wa Mwl ndio walikuwa wanava viatu na kula nyama siku zisizo za sikukuu na vyakula vyao vinaungwa mafuta na kukaangwa.
Watoto wa Mwl ndio wanavaa nguo safi na shati zenye kung'aa
Yaani watoto wa Mwl na Mwl ndio familia kila mtu anakimbilia kukopa akipata shida.
Yaani unaopodharau mtu aliyeajiriwa ni sababu tu ya Ubinafsi kwa kuwa wewe unazo nyingi basi unataka kudharau wengine.
Pamoja na yote uliyosema huna nudhamu ya kazi, hata kama ni kazi yako mwenyewe. Ungekuwa unaondoka saa 12 asubuhi na kurudi jioni daily pengine ungekuwa mbali zaidi ya hapo ulipo.Hapo kwenye N.B. hapo pazingatiwe sana
Mimi toka nimejiajiri naenjoy sana
Kipindi nimeajiriwa nilikuwa natoka home saa kumi na mbili na nusu asubuhi narudi saa tisa au kumi alasiri
Ila sasa hivi naweza kwenda muda wowote ule najua nikikaa masaa kadhaa nikiingiza elf 50, 70 au laki moja narudi zangu home hata kama muda wa kufunga ofisi haujafika mi mradi nimeingiza hesabu yangu ya siku tu basi