Mfano alieajiriwa na aliejiajiri wote wanaingiza milioni 1 kwq mwezi?
Mtumishi wa serikalini na mtu aliejiajiri kama wana vipato sawa ni heri uwe muajiriwa tu.
1. Aliejiajiri anaondoka kwake asubuhi kurudi usiku, alieajiriwa serikalini anaondoka asubuhi anamaliza kazi zake jioni, na hata huko ofisini kuna muda anapata kufanya mambo yake.
2. Aliejiajiri anaweza asizijue weekend lakini alieajiriwa serikalini anapumzika jumamosi na Jumapili.
3. Aliajiajiri hana sikukuu za kiserikali ama dini, asipoenda imekula kwake, alieajiriwa serikalini haendi kazini mwaka mpya, meimosi, sabasaba, siku ya Nyeyere, siku ya uhuru, mapinduzi, nanenane, idi, pasaka, n.k
4. Aliejiajiri akiumwa inabidi ajikaze aende tu lasivyo kipato kinaweza kutikisika, alieajiriwa serikalini akiumwa anatoa notisi.
5. Aliejiajiri hana likizo, muajiriwa ana likizo siku 30 kila mwaka.
6. Aliejiajiri anaweza kufilisika endapo duka likiungua, akiumwa kwa muda mrefu, akiibiwa, n.k. alieajiriwa serikalini nafasi yake na mshahara wake ni uhakika.
7. Aliyeajiriwa serikalini mkopo anapata kwa masharti nafuu na KWA haraka aliyejiajiri hawezi pata mkopo kibwerere.