Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

Leo waajiriwa mnajipamba au sio ?
Basi wacha nikae hapa unitajie muajiriwa
Makonda alikuwa mwajiriwa wewe unamzidi utajiri?

Mimi nimekulia Kijijini Kule Watoto wa Mwl ndio walikuwa wanava viatu na kula nyama siku zisizo za sikukuu na vyakula vyao vinaungwa mafuta na kukaangwa.

Watoto wa Mwl ndio wanavaa nguo safi na shati zenye kung'aa

Yaani watoto wa Mwl na Mwl ndio familia kila mtu anakimbilia kukopa akipata shida.
Yaani unaopodharau mtu aliyeajiriwa ni sababu tu ya Ubinafsi kwa kuwa wewe unazo nyingi basi unataka kudharau wengine.
 
Well said
 
na alieajiriwa anaweza kujiongeza akajiajiri pia.. aliyejiajiiri akijiongeza ataajiri watu wa kuwatoa ngeu. genuine aliyejiajiri anaweza kukua na kuwa mkubwa zaidi...
Wengi hujipa moto majority ni majanga.

Wanaoacha ajira wakafanikiwa ni wale wenye nidhamu ya kazi kama akina Bill Gate.

Madoja hata wakienda kujiajiri wanaangukia pua au kwenye biashara haramu.
 
Kuna watu nawajua tangia nipo shule ya msingi wanaondoka majumbani saa 12 asubuhi kwenda kuuza dukani mpaka saa 2 usiku,
Halafu kuna mimi sasa nnae toka home saa tano/ sita/ saba/ nane/ tisa mchana/ alasiri na kufunga ofisi saa moja na nusu jioni na nna uhakika wa kuingiza kuanzia 50k na kuendelea halafu siwazi sasa
 
Nitoe mfano halisi tu binafsi kujiajiri ni bora zaidi ya kuajiriwa,wazazi wetu walikuwa wanamiliki hospital, sisi watoto baada ya kumaliza medical school tukawa wasimamizi wa hospital baada ya wazazi kufariki kifupi hatujawahi kupata tabu ktk ajira.

Kuna kipindi uwa nawaza je endapo wazazi wetu wangekuwa wameajiriwa serikalini halafu wamefariki tungeweza kurithi kazi zao?

Jibu hapana tusingeweza kurithi kazi zao Wala mishahara yao zaidi tungeendelea kutanga tanga tu na bahasha mkononi.
 
Aliye jiajiri anaweza endeleza mradi wake vizuri ndani ya miaka5 akawa anaingiza zaidi ya m10 kwa mwezi, wakati huo wewe uko
Hapo kwenye N.B. hapo pazingatiwe sana
Mimi toka nimejiajiri naenjoy sana

Kipindi nimeajiriwa nilikuwa natoka home saa kumi na mbili na nusu asubuhi narudi saa tisa au kumi alasiri

Ila sasa hivi naweza kwenda muda wowote ule najua nikikaa masaa kadhaa nikiingiza elf 50, 70 au laki moja narudi zangu home hata kama muda wa kufunga ofisi haujafika mi mradi nimeingiza hesabu yangu ya siku tu basi
 
mjadala huu

utapendeza kama utajali layers.... kuna watu kariakoo wanakunja mpaka m1 kama faida kwa siku. hawa huwez kuwawekea mada ya kuajiriwa mkaelewana
M1 ni nyingi sana mkuu

Mimi nikikunja zangu 50k tu pale kariakoo kisha ukiniletea story za kuajiriwa nakuzingua

Maana kuna mwamba alitaka kuniajiri kisha anilipe 900k kwa mwezi nimemtolea nje
 
yupi ana nafasi nzuri ya kukua zaidi?
Aliejiajiri ana nafasi ya kukua.

Nitakupa mfano mdogo tu.

Juzi kati nilikutana na mdogo wangu mmoja nieyewahi ishI nae huko udogoni. Anapush SUBIE. Wakati naanza kazi huyu dogo alikuwa Chuo.

Amejiajiri na kaajiri watu kadhaa.

Wakati bro wake hata Toyo Sina.

Huu ni mfano mdogo tu
 
yupi ana nafasi nzuri ya kukua zaidi?
Aliejiajiri ana nafasi ya kukua.

Nitakupa mfano mdogo tu.

Juzi kati nilikutana na mdogo wangu mmoja nieyewahi ishI nae huko udogoni. Anapush SUBIE. Wakati naanza kazi huyu dogo alikuwa Chuo.

Amejiajiri na kaajiri watu kadhaa.

Wakati bro wake hata Toyo Sina.

Huu ni mfano mdogo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…