Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

Namba mbili na tatu inategemea umejiajiri vipi?
Mfano una daladala zako kadhaa mjini unasubiri jioni uletewe hesabu wala hautakua involved na kua kazini 7days a week.
Mtoa mada nadhani ni muajiriwa aliyekata tamaa na ametoa thread kama njia ya kujifariji.
 
Namba mbili na tatu inategemea umejiajiri vipi?
Mfano una daladala zako kadhaa mjini unasubiri jioni uletewe hesabu wala hautakua involved na kua kazini 7days a week.
Mtoa mada nadhani ni muajiriwa aliyekata tamaa na ametoa thread kama njia ya kujifariji.
Mmiliki wa daladala kaajiri madereva na kondakta.
Hao ndio wanaozungumziwa.
 
Wengine humu mnasema biashara sio ngumu wakati mmekuta alishakufungulia baba yako kafanya kukuachia urithi. Umekuta foundation imekaa vizuri we kazi kusugua kisigino tu Mtupishe
Sasa hapo ndio uone faida ya kujiajiri maana unawaachia urithi watoto mpaka wajukuu,wewe uliyeajiriwa ukifa unadhani kazi yako na mshahara wako wataurithi watoto wako?? Zaidi familia itapata msongo wa mawazo tu maana tegemezi umeshakufa.
NB:Baba/mama aliyeajiriwa ikitokea akifa anaiacha familia katika wakati mgumu sana maana yeye ndiye aliyekuwa tegemezi
 
Sasa hapo ndio uone faida ya kujiajiri maana unawaachia urithi watoto mpaka wajukuu,wewe uliyeajiriwa ukifa unadhani kazi yako na mshahara wako wataurithi watoto wako?? Zaidi familia itapata msongo wa mawazo tu maana tegemezi umeshakufa.
NB:Baba/mama aliyeajiriwa ikitokea akifa anaiacha familia katika wakati mgumu sana maana yeye ndiye aliyekuwa tegemezi
1. Kila mtu akifanya biashara nani atakua mteja?

2. Nlishaandika huko juu. Una uhakika gani ukifa watoto wako watakua na uelewa wa biashara yako au watagain interest ya biashara yako. Umesomesha mtoto aje kuwa pilot ukimwambia akasimamie machine za kukobolea mahindi atakuelewa?

Endeleeni na nadharia zenu za madaftari ila asikwambie mtu serikalini kuna security kubwa sana.
Hata usiende mbali ile bima ya afya tu, imagine una watoto sita, wewe na mkeo wote mjikatie bima ya najali afya uone milioni zitakazokudondoka. Ila serikalini sio gharama kubwa.

Biashara hata ikiyumba vipi serikalini utapokea mshahara ila wajasiriamali wanayumba kweli.

Endeleeni kukaza fuvu ila wanaokula asali ni walioko serikalini na wana vitega uchumi. I rest my case
 
Mada sio kuajiriwa tu mada ni kuajiriwa serikalini au kujiajiri, kupi kuna nafuu ya maisha? Wewe unaleta stori za jamaa njaa mwenzako sijui alitaka kukuajiri na blah blah kibao, serikalini hakuna mbambamba na watu wanaishi kwa marupurupu hawategemei mishahara, kila siku ana uhakika wa kula na akistaafu kuna kiinua mgongo na bado ataendelea kupokea mshahara mpka kufa kwake, japo ni nusu mshahara.
Sawa ana njaa lakini kumbuka sisi tunafanya kazi zetu, hatupangiwi na mtu nini cha kufanya ratiba zote tunazipanga wenyewe

Popote ambapo tunaona kuna mzunguko mzuri wa kupiga pesa tunawekeza

Tunafunga mahesabu ya mwaka mzima mwezi huu
 
Somebody had to say this!! Mimi nimefanya sana biashara, nimetoka sana jasho la hustle za hapa na pale ila asikudanganye mtu Serikalini ni Serikalini tu!!!! Kipindi cha corona biashara ziliyumba, kwenye private sectors baadhi waliondolewa. Ila Serikalini mserereko uliendelea.

Na nyie mnaosema kama watoto wao watarithi kazi, kwani ukizaa mtoto una uhakika gani atapenda kitu unachokifanya? Una uhakika gani atakuja kupenda hiyo biashara yako ya mahindi.

Rai, tafuta kazi Serikalini, establish vitega uchumi au biashara ambazo sio lazima uwepo 24/7.. unazichanga unawanunulia ardhi wakija kukua hao wanao wana cha kurithi. Na wenyewe unawajengea misingi ya kujitegemea kimaisha hata kama umewaandalia chochote kitu incase ukidondoka. Full stop.

Hii mada haihusu wale wanaume wenye watoto sita ndani ya ndoa wanne nje. Nyie mkifa familia zenu zinatamanigi ziwachape makofi ngedere
Na hakuna mtumwa tajiri sasa raia mil 61 wote watafute kazi serikalini? Mtu anaewaza kuajiriwa fkira zake ni za kimasikini

Sent from my PRA-LA1 using JamiiForums mobile app
 
Ikiwa alieajiriwa Serikalini na aliejiajiri wote wanaingiza kipato sawa kila mwezi

1. Aliejiajiri anaondoka kwake asubuhi kurudi hadi usiku, alieajiriwa Serikalini anaondoka asubuhi anamaliza kazi zake jioni na bado huko ofisini kuna muda anapata kufanya mambo yake.

2. Aliejiajiri anaweza asizijue weekend lakini alieajiriwa Serikalini anapumzika Jumamosi na Jumapili.

3. Aliajiajiri hana sikukuu za kiserikali, alieajiriwa Serikalini haendi kazini idi (hata kama ni mkristo), mwaka mpya, Mei mosi, sabasaba, siku ya Nyeyere, siku ya uhuru, mapinduzi, nanenane, idi, pasaka, n.k

4. Aliejiajiri akiumwa inabidi ajikaze aende tu lasivyo kipato kinaweza kutikisika, alieajiriwa Serikalini akiumwa anatoa notisi.

5. Aliejiajiri hana likizo, muajiriwa ana likizo siku 30 kila mwaka.

6. Aliejiajiri anaweza kufilisika endapo duka likiungua, akiumwa kwa muda mrefu, akiibiwa, n.k. alieajiriwa Serikalini nafasi yake na mshahara wake ni uhakika

7. Aliyeajiriwa Serikalini ni rahisi kukusanya mtaji, mkopo anapata kwa masharti nafuu sana na kwa haraka sambaamba na kudunduliza mshahara

8. Alieajiajiriwa na Serikali ana muda mwingi wa kuwa na familia yake kuzidi aliejiajiri. ikifika jioni, weekend, sikukuu za serikali, likizo, n.k. ana muda wa kutosha wa kuwa na familia yake

9. Alieajiriwa Serikalini anaweza kuwa ma biashara zake za kumuongezea kipato, hizi biashara zinaweza kumtunza baada ya kustaafu na watoto wake kuzirithi, Mifano ni kina Robert Kiyosaki mwenye kitabu cha Rich Dad Poor dad, Vunja Bei, Marehemu cpa Mengi, n.k. walianza kwa kukusanya mitaji wakiwa wameajiriwa.

Mwisho niseme Kujiajiri watu wanameki bingo lakini ni wachache, wengi wanaanguka na wengine wapo pale pale miaka nenda rudi. wachache wenye wenye roho ngumu, ubunifu, juhudi, kujibana, uvumilivu na connections ndio wanatoboa.
Kujiajiri si rahisi kama mnavosimuliana kwenye vijiwe au uko chuoni kwenye course ya entrepreneurship. Sifa ya kwanza ya kutoboa Kwa kujiajiri ni uwe na roho ngumu na ukubali muda mwingine utapita njia za panya utoboe. Wengi ambao hawapiti njia za panya wako hivi mpaka leo, wengine wanaanguka.
 
Wengi hujipa moto majority ni majanga.

Wanaoacha ajira wakafanikiwa ni wale wenye nidhamu ya kazi kama akina Bill Gate.

Madoja hata wakienda kujiajiri wanaangukia pua au kwenye biashara haramu.
Hakuna atakaejitoa ajiran kama mvivu. Mana kujiajiri hakuhitaji relax hata second. Watu wanaopambana kwenye kujiajiri wanafanikiwa sana. Hii nimeona kwa mzee moja hiv amejiajiri Ana kampuni 3 lakin kulala kwake kwa machale pampja na kuwa na wafanyakaza zaid ya 50
 
Back
Top Bottom