Tanzania visiwani waomba msaada wa walimu toka Nigeria, wakati Bara kuna walimu hawana ajira

britanicca

Platinum Member
Joined
May 20, 2015
Posts
18,261
Reaction score
48,864
Serikali ya Zanzibar imeagiza zaidi ya waalimu 300 wa masomo ya Sayansi kutoka nchini Nigeria ambao tayari wameanza kuwasili visiwani humo.

Kwa mujibu wa serikali ya Zanzibar, waalimu hao wanaoingia kwa awamu, na wanatarajiwa kuziba pengo la uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 wa masomo hayo.

Katika mahojiano maalum na BBC naibu waziri wa Elimu Zanzibar Mmanga Mjengo amesema ujio huo utasaidia kuamsha pia morali ya waalimu wengine wa masomo ya sayansi visiwani humo

Mimi kama Britannica sioni mantiki.

======

Katika mahojiano maalum na BBC naibu waziri wa Elimu Zanzibar Mmanga Mjengo amesema ujio huo utasaidia kuamsha pia morali ya waalimu wengine wa masomo ya sayansi visiwani humo.

Ameongeza pia wameamua kwenda mchini Nigeria kwa sababu kuna wingi wa waalimu na wenye ubora na haikuwa rahisi kuchukua kutoka nchi za karibu kwa sababu na wao pia wana tatizo la uhaba wa waalimu.

''Mchakato wa upatikanaji wa waalimu hawa hufanywa kwa kutegemea uwezo wao katika ufundishaji na pia ubora wa kazi zao.'' alisema waziri Mjengo.

Serikali ya Zanzibar imesisitiza kuwa sio mara ya kwanza kwa ujio kama huu kwani katika miaka ya nyuma waalimu hawa wamekua wakija kwa kujitolea.

Ujio wa waalimu hawa ambao watakuwepo kwa kipindi cha miaka miwili unatajwa kupunguza uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 visiwani humo.

Zanzibar yaagiza waalimu wa sayansi kutoka Nigeria
 
serikali hizi mbili ni za kipuuzi kupita maelezo,yule kaagiza matani ya sukari toka brazil wakati ya zenji ipo na huyu nae kaagiza walimu wakati huko bara wamejazana wanataka ajira,ndio maana nataka trump aendelee kututukana miaffrika hasa hii ya east africa,
 
Umeandika "Tanzania visiwani" nilikua sijaelewa heading yako mpaka nimesoma uzi.
 
Serikali ya Zanzibar imeagiza zaidi ya waalimu 300 wa masomo ya Sayansi kutoka nchini Nigeria ambao tayari wameanza kuwasili visiwani humo.

Kwa mujibu wa serikali ya Zanzibar, waalimu hao wanaoingia kwa awamu, na wanatarajiwa kuziba pengo la uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 wa masomo hayo.

Katika mahojiano maalum na BBC naibu waziri wa Elimu Zanzibar Mmanga Mjengo amesema ujio huo utasaidia kuamsha pia morali ya waalimu wengine wa masomo ya sayansi visiwani humo

Mimi kama Britannica sioni mantiki.

Zanzibar yaagiza waalimu wa sayansi kutoka Nigeria

Yaani sijuwi watafundishaje maana Ningerians hicho kiingereza chao ni utata mtupu....bora hata waongee kiyoruba au Kiigbo tu maana hawaeleweki wanaongea kitu gani.
 
serikali hizi mbili ni za kipuuzi kupita maelezo,yule kaagiza matani ya sukari toka brazil wakati ya zenji ipo na huyu nae kaagiza walimu wakati huko bara wamejazana wanataka ajira,ndio maana nataka trump aendelee kututukana miaffrika hasa hii ya east africa,
Huu muungano hauna maana yoyote kama hatuwezi kusaidiana,kitu kimoja muhimu katika kuungana ni ufanyaji wa biashara baina nchi mbili zilizoungana ili kuinua uchumi wa nchi husika na kuenua hali ya maisha kwa raia wa nchi husika,katika muungano huu silioni hilo,kila kukicha majungu na kuvimbiana vifua,huu mungano bora uvunjike tu
 
Mahali ambapo maslahi ya watawala hayaguswi hata aje nani. Lakini ingekuwa kuleta wachunguzi toka nje kusaidia uchunguzi ungesikia wasiingilie mambo yetu ya ndani!
 
Back
Top Bottom