Hivi unadhani kila unayetaka kumpa uraia wa Tanzania naye anataka huo uraia? Labda tuanzie hapo, maana tunajifunga kwenye mawazo kwamba eti akina Wawa na wengine wanapenda kuwa Watanzania. Tukumbuke kuwa kuna watu kwao kucheza timu ya taifa sio kipaumbele ukilinganisha na kujitenga na jamaa zao
Unaweza ukamtaka Wawa awe Mtanzania, lakini yeye hataki kwa sababu nyingine za kijamii, maana faida ya kuichezea Taifa Stars huenda ni ndogo kuliko faida ya kuwa karibu na jamaa zake aliowaacha Ivory Coast, ukizingatia kwamba umri wa kucheza mpira sana sana ukizidi ni miaka 35