tony92
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 2,398
- 3,691
Ukitaguta mabeki wazawa walocheza mechi nyingi za kimataifa sidhani kama wapo kwa sasa? Na kama wapo basi hawapo katika viwango vyao.Huyo Kibu angeweza kupewa uraia hata kama sio mchezaji, yaani hata kama angekuwa mkulima tu, sheria inampa uwezo waziri kufanya hivyo na wala hakuna mtu wa kuhoji. Kwa hiyo povu la kusajiliwa Kibu kama Mtanzania lisihamishe mjadala.
Badala ya kuangalia wanaopewa uraia, hebu tuangalie mabeki wetu ambao wana uraia halali usio wa kupewa, akina Dickson na Mwamnyeto. Ni wa viwango vya kutupeleka WC? Wamewahi kucheza mechi ngapi za kimataifa? Kama sio kucheza, basi walau wana uwezo gani uwanjani?