Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Watapona soon tu hao. Mfungo wa siku tatu ukiisha tutakuwa tupo vizuri kabisa
Najaribu kufungulia stesheni za redio 80% zinapigwa ngoma za singeli tena za matusi ndani yake,jamani Raisi katangaza mfungo kwann hizo stesheni zisijarbu kupiga ngoma hata za wenzetu taswida au Gospo ambazo zitamkumbusha mtz kuwa ni kipindi kigumu tumwombe mungu wetu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambao mzima wa Bahari kuanzia Tanga Dar Pwani na Lindi corona imeshatia timu sasa Mwanza itasambaza kwenda mikoa yote ya kanda ya Ziwa.

Mkakati wetu ni uleule wa Mtukufu Magufuli ambao ni "Do nothing" na sasa ameongeza "Sala za siku tatu" juu yake corona itajiju irudi ilikotoka.
 
Unathibitishaje hili?
Mkuu nadhani haukunielewa kutokana na makosa yangu ya uandishi.
Nilikusudia kuandika "Wachina siyo walioleta maambukizi ya COVID-19 moja kwa moja toka China kuja nchini mwetu".

Maambukizi yaliyo ingia nchini yametokea nchi za magharibi yaani Ulaya na Amerika, na baadae Mashariki ya kati yaani Uarabuni.
 
LICHADI,
Lawama zote kwa John

Sidhani kama ni muda sahihi kuwa tunapeleka lawama sehemu fulani. Muda huu ni muhimu kwa sisi wote, kila mmoja kwa nafasi yake kuchukua hatua stahili kuhakikisha tunadhibiti maambukizi ya huu ugonjwa. Ndio namna pekee ya kushinda. Lawama hazitotusaidia.
 
Tunachukua tahahadhari huku tunachapa kazi

Wanaotaka tuwekwe lockdown watatulisha?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu wewe unataka kula au kulishwa na wanaoona twende kwenye lockdown?

Ni vizuri kuwa wazi mkuu maana hayo mawili ni tofauti.

Ila ukweli uliowazi, kupitia kwenye lockdown ugonjwa utadhibitiwa, hatimaye ugonjwa utakwisha na maisha yako, yangu na yule yataokolewa.

Unapaona je hapo mkuu? Hakuna matamu bila machungu wahenga waliokwisha sema.
 
Polepole yu wapi. Eti corona itapigwa kama CHADEMA, haya sasa hili hapa linatutafuna,tuma green guard wakahudumie waathirika
 
Sidhani kama ni muda sahihi kuwa tunapeleka lawama sehemu fulani. Muda huu ni muhimu kwa sisi wote, kila mmoja kwa nafasi yake kuchukua hatua stahili kuhakikisha tunadhibiti maambukizi ya huu ugonjwa. Ndio namna pekee ya kushinda. Lawama hazitotusaidia.

Mkuu hakuna anayetaka kumlaumu mtu bila sababu.

Angalia hata sasa badala ya kuchukua hatua tunaitisha mikusanyiko mingine kwenye ibada ya maombezi.

Kwa nini bunge linaendelea kule?

Kwa nini pamoja na makelele yote hatua stahiki hazichukuliwi kwa wakati? kwa nini hata sasa dar haifungwi ugonjwa ukadhibitiwa huku?

Hadi ugonjwa utawanyike hadi Makongorosi ndiyo tugutuke?
 
LICHADI, Kwa nini unamlaumu sana RAIS kama vile yeye ndiyo aliyeleta ugonjwa?ukitazama jinsi ugonjwa unavyo kwenda unaona wazi tunamuhitaji MUNGU zaidi kuliko kuziba mipaka,hapo hukui hata kama wajanja wa dunia wamerusha hewa hiyo kwetu huna uhakika,wewe ni kulaumu tu!!!

kumbukeni maneno mengi nayo inatia hofu wengine na kusababisha uoga mkubwa ilihali ni kweli kabisa MUNGU anaweza akatunusuru pakubwa,inawezekana watu wakaugua na wasiondoke vile vile maana pia kwetu alituumba tukiwa wagumu kupita kiasi.

Wengine husema watu wafungiwe ndani,maisha ya waTanzania sisi mpaka tutoke ndiyo watoto wale chakula ukifungia watu ndani nini kitatokea? Watu hawana akiba hata tone,sema tu mnaoongea mna kahali fulani ka maisha kanako wasahaulisha kua kuna wenye shida kubwa ya kifedha na chakula

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Mungu tunakuomba uliponye taifa letu. "Wewe ndiwe Mungu wetu! Waadhibu, kwani sisi hatuna uwezo wowote mbele ya jeshi kubwa kama hili linalotujia. Hatujui la kufanya ila tunatazamia msaada kutoka kwako.” 2 Kumbukumbu la Torati 20:12
 
Bado mashindano ya kutanganza waathirika yanaendelea sijui yana tija gani. Wangapi wamepona? Bado nasimamia pale pale dunia nzima ime overeact na huu ugonjwa.
No, you're wrong. Ingekua watu hawafi ungemake sense
 
Ni hatari sana wakuu pamoja na ndoo za maji tiririka kuwekwa kila mahali lakini ndo idadi ya maambukizi inapanda hadi inastua.

Mimi naona serikali ingesitisha safari zote za mikoani kwa kipindi hiki la sivyo yajayo yanasikitisha!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom