Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

G'taxi, China imefanikiwa kupunguza maambukizi kwa kuwafungia ndani na kufuata maagizo ya wataalamu . Si kwa maombi. Hata ujerumani wanakuambia ni kwa kukaa ndani .

Serikali ihudumie watu hii ni dharura kama dharura nyingine.

Odhis *
 
LICHADI, Tofauti na virusi vya UKIMWI, ambavyo vina dawa ya kufubaza na maambukizi ya kisiri, huu unasambaa haraka. Pamoja na kuwa hivyo, bado kuna watu, kama wewe, hamtumii kinga kufanya mapenzi na kupima hamtaki.

Utakuwa mjinga kusubiri Serikali ikuagize kujifungia au ikusimamie kuzingatia ushauri wa wataalamu.
Sasa mkuu tulipo shauri mipaka ifungwe na kuzuia ndege ulitaka mwananchi azuie au serikali?

Hali imekua mbaya mnaanza kusema tusingoje serikali daah!
 
Watu wenye dalili ndo waambiwe wasiende Muhimbili maana yake ukisema muhimbili wasiwapokee itaongeza tatizo zaidi maana mtu atafunga safari hadi muhimbili halafu arudishwe, anapokwenda anaweza kuambukiza watu njiani na anapo rudi vile vile.
Ushauri wangu wananchi watangaziwe kwamba akijiona ana dalili asiende muhimbili.
 
Roving Journalist,
Tatizo kufanya mambo bila kujali,na hii inasbabishwa na misifa mingi,watu wanamsifia mtu mpaka anajisahau, mie mambo ya maombi hapana, ila napendekeza awakusanye wale wachungaji hasa wa miujiza na watu wadua awatembeze kwa wagonjwa wafanye maajabu, sio kila siku kitudanganya eti kiwete anatembea, kipofu anaona, sasa walivamie Covid-19.
 
brazaj,
Mkuu ndio maana nikasema kila mtu kwa nafasi yake na kwa utashi wake aamue kufanya lile ambalo ni sahihi kwa wakati sahihi.
 
Una hakika mkuu ?!.

Odhis *
Siwezi kusema kwa hakika 100% , lakini kwa kuangalia muda tulioanza kupata maambukizi na wagonjwa wote waliokutwa na huu ugonjwa baada ya kupimwa na serikali tuliona wametokea nchi nilizosema.
 
LICHADI,
Acha lawama, China leo watu 1290 wamerejea kwa mungu, na wao wamlaumu Xian Ping? Hili sio tatizo la JPM tu la wote mpaka anayetangaza idadi pia! Na wabunge wote!
 

Attachments

  • 2127677_IMG-20190801-WA0025.jpeg
    2127677_IMG-20190801-WA0025.jpeg
    104.4 KB · Views: 1
Hivi ukiondoa issue ya sala na maombi, kuna strategies zozote za maana za kupambana na huu ugonjwa? Decisive measures? Kwa mfano kulazimisha raia wote kuvaa masks wakitoka nje kama Kenya na nchi nyingine za Asia.

Au baadhi ya viwanda viwe subsidised na serikali, vitengeneza extra sanitizers, surgical masks and other PPEs kwa wahudumu wa afya na barakoa za kawaida kwa raia.

Mimi naona mambo yanaenda kama kawaida, mikusanyiko mikubwa iko pale pale si kwenye nyumba za ibada si bar and nightclubs. Nasikia polisi wanapiga watu kwenye baadhi ya baa kupunguza mikusanyiko lakini hamna tangazo rasmi la kufunga hizo sehemu.

Hakuna kabisa restrictions za movement za watu, kuingia na kutoka kwenye mikoa tunayoweza ita endemic. Yaani mapambano tunayoyaona nchi nyingine huku kwetu ni kama hamna, tuko poa yaani.

Bado hatupewi idadi ya waliopimwa. Na kwa kweli sijui kama trace,test and isolate inafuatwa. Pia sioni umuhimu wa ku-centralize testing, ati zote zinafanyika Dar maabara ya taifa. Sasa ule msaada wa Test kits wa Jack Ma unatumiwa wapi?

Partial lockdown and even curfew ni muhimu mno kwa sasa.

Pamoja na kuwa na ile kamati ya kupambana na Corona, kuna leadership kweli kwenye hili tatizo?
 
Wametoka sehemu mbali mbali za Tanzania hi ni hatari sanaa manaake ugonjwa umesha enea nchi nzima........naomba Raisi achukue hatua zingine zaidi ya maombi, ili hu ungojwa usiingie ndani sana vijijini ambao wana matatizo ya afya mengi
anaongeza mwezi mzima wa maombi
 
Tatizo ishu ya Corona kwa Tanzania pia kauli za Rais wetu alizotoa huko nyuma eti chapeni kazi Corona ni kaugonjwa kadogo. Eti tunatisha muno nazo zinachangia ona hadi tunadhihakiwa huko nje.

Nilimuonya kuwa ukiwa kama Rais kuna vitu hutakiwi kuongea. Niliposema hivi MATAGA wakiongozwa na Pascal Mayalla wakanipinga wakisema eti Rais wetu ni mkweli!

Yani miluzi ya kejeli kwa huu ugonjwa ilikuwa mingi kuanzia kwa viongozi wa serikali hadi wa dini. Kwa kweli inauma sana Rais anaongea hivyo wakati kwa wenzetu wakati huo walikuwa wanakufa, wanalia wanaomba!
 
Back
Top Bottom