Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Serikali wahimize matumizi ya barakoa hasa watu wanapotoka nje kwenda makazini na kwenye shughuli nyingine, siyo lazima watumie zile 'medical masks kama N95' tutumie tu za vitambaa, mfano. ujerumani wanatumia tu za vitambaa.

Serikali wa- identify kampuni ambazo zinaweza kutengeneza barakoa za vitambaa kwa wingi ili zianze kusambazwa mitaani kwa wingi kwa bei nafuu....ili baadaye iwe mandatory watu kuvaa barakoa in public..
 
Sibonike, Idadi ya 54 ndo idadi nzima ya wa athirika wote nchini Uganda sisi tumewapata siku moja wenzetu wako lock-down hi wiki ya tatu na wameongezewa wiki tatu zingine wakati sisi bado tunadunda tuko bize kusali duh......' now who is fooling who'?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unauhakika huko ndani ya nyumba zao watu hawafi kwa magonjwa mengine au corona enyewe pamoja na njaa? Hivi umejiuliliza ni janga gani litaloweza kufuatia baada ya lockdown? Halafu kwa nini uone kuwa hatua tulizochukua sisi kama taifa hazifai mpaka utake tufanane na Uganda? Wewe badala ya kushauri watu wafuate maelekezo ya wataalamu wa afya unataka watu watibu janga kwa kuzalisha majanga mengine.

Sijui kama umewahi jiuliza ni masikini wangapi watakao kufa kwa njaa na msongo wa mawazo endapo nchi yetu itawekwa lockdown, sijui kama umewahi jiuliza ni watoto wangapi wa masikini watakao kufa kwa utapiamlo endapo nchi yetu itawekwa lockdown.

Binafsi sipendi kuona watu wakizagaa ovyo barabarani au kukusanyika ovyo masokoni na minadani bila kuchukua tahadhari, ila ni vyema kwa wale waliojitoshekeza kwa mahitaji yao wakajifungia ndani ili kupunguza msongamano barabrani na masokoni na kuwaacha wale masikini wanaotafuta ridhiki za kila siku wajitafutie mkate wao ili wasife kwa njaa.
 
njia muhimu ya awali ya kujilinda na korona ni kuvaa harakoa nashangaa serikali mpaka leo
hawajafanya kuwa ni sheria kwa kila mwananchi kuvaa kimsingi asilimia 99 ya maambukizi ya korona kutoka mmoja kwenda kwa mwingine.

vinapitia kwa njia ya mdomo na pua sasa kwa nini mpaka leo hizi njia za kutokea virus zipo wazi. tafazari serikali isifanye mzaha kwa hili hatua kubwa na muhimu za kujilinda na korona ni mbili tu aidha watu wote kuvaa barakoa au watu kuwekwa karantini ila kwa hali tulinayo sasa ni vizuri tungeanza na hii ya barakoa hizi njia zote zinazotumika sasa ni visaidizi vya ziada wala si njia ambazo zinaweza kudhibiti maambukizi ya janga hili.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado mashindano ya kutanganza waathirika yanaendelea sijui yana tija gani. Wangapi wamepona? Bado nasimamia pale pale dunia nzima ime overeact na huu ugonjwa.
Nakubaliana nawe dunia ime over react, kwa sababu hawa mabeberu wanajua wamekitengeneza kirusi, na wanajua kilikuwa kinaua vipi panya huko maabara.

Ndiyo maana tunaona kuna kutupiana lawama mataifa makubwa, hatujui nani mkweli nani muongo..Tutakaoumia zaidi ni sisi maskini..hiyo ndiyo hofu yetu..

Watu tumesahau vifo vingine, tunaogopa kifo kitokachanacho na CORONA, sababu inakuondoa fasta kwa dalili tu za kipuuzi za mafua..

Everyday is Saturday...................... 😎
 
Waziri wa afya mh Ummy Mwalimu ameitangaza hospitali ya Rufaa ya Amana katika manispaa ya Ilala Dsm kuwa kituo cha kuhudumia wagonjwa wa Covid 19.

Mh Ummy amesema uamuzi huo umefikiwa ili kuinusuru Muhimbili na kuiacha iendelee kutoa Huduma nyingine muhimu pia kwa wagonjwa wa moyo, figo, mishipa ya fahamu, mifupa nk.
Hivyo kuanzia sasa wagonjwa wa Covid 19 wasipelekwe muhimbili.

Source ITV habari
 
Naona na hapa Mwanza takwimu za maambukizi zinazidi kupanda,hadi sasa wamefika 4 kwa mujibu wa wizara ya Afya

Na nionavyo wananchi kwenye hili jiji wachache sana wanazingatia kanuni elekezi,wengi ni mzaha,kwenda wilaya za Magu,Sengerema,Misungwi na Kwimba watu hawana habari na maambukizi

Mongela sijui unafanya nini ofisini,toeni elimu

Bila lockdown, Geita,Musoma na Tarime watashuhudia visa vya maambukizi wiki za karibuni

WHO wameonya Afrika Maambukizi kufika vijijini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najaribu kufungulia stesheni za redio 80% zinapigwa ngoma za singeli tena za matusi ndani yake,jamani Raisi katangaza mfungo kwann hizo stesheni zisijarbu kupiga ngoma hata za wenzetu taswida au Gospo ambazo zitamkumbusha mtz kuwa ni kipindi kigumu tumwombe mungu wetu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Tuwaombee tu mungu awasaidie wabadilike
 
Ungekuwa mkazi wa Dar ungetamani sana kuwa mwanza
Mwanza sound good right now
 
Sisi wa machimboni na wachina mkaa hatuna shaka
 
cutelove,
Kumbe una ishi Mwanza apo vizuri, nimefurai kusikia unaishi Mwanza, kuhusu Korona Tuzidi kumwomba Mungu na tuchukue tahadhari.
 
Back
Top Bottom