Tanzania watu binafsi wasirusiwe kujenga nyumba bali makampuni ya real estate

Mfano mzuri ni hapo Dodoma.
Real estate wanatakiwa waweke mifumo ya kisasa ya makazi na mipango miji.
Mifumo ya maji safi, maji taka , njia za mawasilioano , barabara za zege. Mabomba ya gesi ndani ya nyumba.

Pia hatutaki frem kwenye hayo maeneo.
Alaf nyumba akuuzie million 20?
 
Hili jambo nilisha wahi waambia watu wa wizara ya ardhi,yani unakuwa na Jiji lakini kiuhalisia ni kama uchafu.
Watu wanajijengea vijumba vya hovyo,wengine hawafuati standard kila nyumba ina frame mbele yani ujinga mtupu.

Angalia mfano Dodoma,kuna maeneo walishakubaliana unapoweka bati lazima liwe jekundu au blue au kijani.Unakuta mtu anajenga eneo linalotaka bati nyekundu lakini jitu linakupigia blue.

Lakini zikijenga Kampuni binafsi wataweka mipango miji mizuri zaidi.
 
Kampuni hizi hizi ambazo wanakupigia hesabu kuwa tofali moja inauzwa kuanzia Tshs. 2,500/= hadi Tshs. 4,000/=!!!??
 
Udikiteita tu! CCM utawajua tu! Nenda Sweden ujifunze serikalinau communes zinavyoganyanhicho unachokisema. Hatujafika huko!
 
Alaf nyumba akuuzie million 20?
Ni inakuwa ni mradi wa nyumba nyingi kwenye mahitaji yote ya mipango miji, na pesa unalipa kwa instalment, na pia kutakuwa na nyumba nafuu zaidi ya hapo, hata million 10 unapata nyumba
 
Pia kuwepo na utaratibu na usimamizi wa ujenzi, sio kila MTU akitaka kujenga basi anamtafuta fundi au company na kuuanza ujenzi au kuongeza rooms ,

Bali ujenzi uwe ni kibali kinacho toka munispal, ili kufuata taratibu na mipango miji na standards za ujenzi
 
Kunakua na makampuni yaliyopewa kobali na aina za nyumba wanazotakiwa kujenga
 
Naunga mkono hoja. Wabunge wapitishe hii iwe sheria. Na huduma muhimu zote ziwekwe na kampuni. Mfano mifereji ya maji, mifumo ya mawasiliano kama fibre optic cables etc.
Wanajenga kila kitu mpaka paving watapiga huko mitaani hakutakua na kero na vumbi
 
Inawezekana kama Rais akiamua
 
Bongo tuna NHC , tatizo ni lushuwa hata ka kujenga na kuuza hiyo lushuwa kwenye bei ya kuuzia
 
Ili miji kupendeza inahitaji vitu viwili tu kufanyika wala haitaji kampuni binafsi kutujengea nyumba.

(1) Ardhi ipimwe (2) Kusimamia vibali vya ujenzi .

Ardhi ikipimwa kila mmoja atajenga kwenye ardhi iliyopimwa , Idara ya Ardhi waweke standard ya nyumba kila plot na iwe ni sheria kwa kila halmashauri ya miji.Mtu kabla ya kununua kiwanja ajiridhishe standard ya nyumba kwenye hiyo plot.

Serikali ijenge sewage system na sio wananchi kuchimba makaro na pia iweke miundo mbinu ya maji safi na umeme.

Hii ni rahisi zaidi.
 
πŸ–•πŸ–•πŸ–•πŸ–•πŸ–•πŸ–•

Wazo la kichoko
 
Nhc housing Morocco na kawe pale si mmejenga
Bei yake umeiona lakini

Ova
Bei za nyumba zinazojengwa na Real Estate Developers Tanzania hazina uhalisia na ni kubwa sana kwa wakulima, wafanyakazi na hata wafanyabiashara wengi katika taifa hili kuweza kuzimidu

Unashangaa hata National Real Estate Developer(NHC) nae ameingia katika biashara ya kuuza nyumba za makazi kwa bei kubwa sana

Jambo la muhimu serikali isaidie kupimia watu maeneo yao na isimamie kwa ukamilifu sheria za mipango miji bila kuwapa ukiritimna watu wachache na nchi itapendeza tu. Si unaona Dodom? Wanaelekea kuweza
 
Ni kweli lakini kwa kipato cha mtanzania na asilimiaa kubwa hatukopesheki, hizo nyumba zilizojengwa na real estate zinazokuwa overpriced tutaziweza kweli?
 
Ni kweli lakini kwa kipato cha mtanzania na asilimiaa kubwa hatukopesheki, hizo nyumba zilizojengwa na real estate zinazokuwa overpriced tutaziweza kweli?
Kila jambo linamwanzo wake
uholela ukiendelea hivi miji inazidi kuaharibika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…