Tanzania watu zaidi ya milioni 40 hawana makazi yao ya kuishi

Tanzania watu zaidi ya milioni 40 hawana makazi yao ya kuishi

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Kiwango cha umasikini na sera ya nchi ya kumiliki ardhi na viwanja ni changamoto kubwa sana! Ukiacha watoto inaonyesha kuwa watu MILLION 40 MPAKA 45 hawana makazi, tatizo ni nini?

Sera ya nchi ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na makazi salama inaharibiwa na utaratibu mbovu wa watu kumiliki ardhi, unakuta jitu moja limeshikilia ardhi kijiji kizima.
 
Hizi takwimu utakuwa umetohoa kwenye idadi ya majengo kulinganisha na idadi ya watu, unachosahau..

1. Katika hayo majengo kuna maghorofa makubwa yanabeba watu wengi
2. Kuna watoto wanaokaa kwa wazazi wao
3. Kuna wanandoa wanaokaa wawili kwenye paa moja
4. Kuna wazee wasiojiweza wanaokaa kwa watoto wao
5. NK
 
Nadhani Jibu la swali lako tayari limejibiwa na Mkuu Replica
 
Ungeomba kuelekezwa kwanza sio kila ni nchambuzi wa takwimu.

Kwanza kabisa naamini mada yako imekuja baada ya kuona idadi ya majengo na watu kutokana na matokeo ya mwanzo ya sensa yaliyotangazwa Jana.

Kama ndivyo basi elewa jambo moja idadi ya majengo hata siku moja haiwezezi kuwa sawa na idadi ya watu.

Kwanza unatakiwa unatambue kwamba watu wengine ni tegemezi na pia jengo moja linaweza kukaliwa na MTU zaidi ya mmoja. Kwanza mfano ni apartment za kwenye ghorofa, unaweza kukuta ghorofa moja lina apartment zaidi ya 40
 
Kama hiki ulichokiandika ni kutokana na takwimu za sensa basi kwa Tanzania makazi siyo issue at ceteris peribus kila jengo wanaishi watu wanne hivi
 
Kiwango cha umasikini na sera ya nchi ya kumiliki ardhi na viwanja ni changamoto kubwa sana! Ukiacha watoto inaonyesha kuwa watu MILLION 40 MPAKA 45 hawana makazi, tatizo ni nini...
unajua kuwa katika hiyo sence karibia theluthi mbili ni teenegers and below wanaishi kwa wazazi wao? stop reached biased conclusion and think first. makazi ya watu hayawezi kuwa sawa na idadi ya watu.

Au kwenu - baba, mama na watoto kila mmoja ana nyumba yake ya kuishi ili idadi ya makazi yenu iendane na idadi yenu? don't they live in one roof?
 
Nchi ya watu wasio na makazi ndio kwanza tunafanya royal tour kwa bilioni 7 na sherehe za sensa kwa bilioni 6.
 
Kiwango cha umasikini na sera ya nchi ya kumiliki ardhi na viwanja ni changamoto kubwa sana! Ukiacha watoto inaonyesha kuwa watu MILLION 40 MPAKA 45 hawana makazi, tatizo ni nini...
Issue siyo uhaba wa ardhi. Tatizo ni ufukara walionao watu wetu. Hata wakiwa na ardhi hawawezi kujenga
 
Kiwango cha umasikini na sera ya nchi ya kumiliki ardhi na viwanja ni changamoto kubwa sana! Ukiacha watoto inaonyesha kuwa watu MILLION 40 MPAKA 45 hawana makazi, tatizo ni nini...
Kwa Tanzania ukishindwa kumiliki ardhi ni ujinga wako. Kuna mahali unakuta pori kabisa ni nguvu yako ya kufyeka tu. Tatizo ni uwezo wa kumiliki ardhi hapa mjini ambapo bei ni kichaa.
 
Issue siyo uhaba wa ardhi. Tatizo ni ufukara walionao watu wetu. Hata wakiwa na ardhi hawawezi kujenga

Cha kushangaza hapa Tanzania wenye ardhi wengi ndio masikini zaidi. Nenda huko vijijini kila mtu anamiliki ardhi, lakini hata kulisha familia yake mlo bora hawezi!
 
Kama tuna sera mbovu ya ardhi na wakenya wasemaje???
 
Sijui umewaza nini mpaka ukaleta huu uzi mkuu.

Hapo unapoish mko wangap?

Kwa mimi mahali nilipohesabiwa, usiku wa kuamkia siku ya sensa tulikua 10 kwenye nyumba moja.

Kwa hesabu za mleta mada kwahiyo watu 9 pale hawakua na makazi 😂😂
 
inaonyesha kuwa watu MILLION 40 MPAKA 45 hawana makazi, tatizo ni nini?
Nadhani unakusudia kusema Kuna Idaho hiyo ya watu hawamiliki nyumba, Kwa maana ya kwamba wanaishi kwenye nyumba ambazo sio mali yao bali wamepanga. Mi sioni shida ktk hilo- watoto na vijana ndio wengi ktk jamii na bado hawajawa na uwezo wa kujenga nyumba.

Lakini pia kumiliki nyumba sio lazima. Ni muhimu sana kumiliki pesa na mali (mali sio lazima iwe nyumba). Ukiwa na pesa unaweza kupanga (au kuishi kwenye mahoteli maisha yako yote 🤩😂😂😂)
 
Kiwango cha umasikini na sera ya nchi ya kumiliki ardhi na viwanja ni changamoto kubwa sana! Ukiacha watoto inaonyesha kuwa watu MILLION 40 MPAKA 45 hawana makazi, tatizo ni nini...
Inaonesha? Lakini hauna uhakika? Basi sawa
 
Ungeomba kuelekezwa kwanza sio kila ni nchambuzi wa takwimu.

Kwanza kabisa naamini mada yako imekuja baada ya kuona idadi ya majengo na watu kutokana na matokeo ya mwanzo ya sensa yaliyotangazwa Jana...
Sijui watu walienda shule kusomea nini?

Bora mnamuelewesha.
 
Back
Top Bottom