Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Hii ni imani tu...
Ni imani kwamba Mh Samia kafanya tofauti na mzee wa chato?

Mimi naona kwa macho yangu na ninasikia kwa masikio yangu kwamba rais wa sasa yupo vyema sana katika kuongoza wananchi wake zaidi ya milioni 60 tofauti na jamaa mkatili na mpenda sifa aliyepita wewe unanijibu eti ni imani!

Hivi unasoma na kuelewa kweli?
 
Chama kilekile.

Ilani ileile.

Katiba ileile.

Watu ni walewale kasoro mmoja tu.

I am sober. I am managing my expectations.

Sitegemei tofauti kubwa.
Tofauti itakuwepo Mama Samia atakapoendelea kuzingatia katiba na sheria. Na ameanza na TAKUKURU, amewaambia kesi zote zisizokuwa na msingi na zile za kubambika wazifute. Najua anajua kesi za namna hiyo zipo, na TAKUKURU wanajua hivyo pia. Ni mwanzo mzuri na ni tofauti ya dhahiri na mtangulizi wake.
 
Pole sana mleta mada.
Umeamua kuja kujifariji hapa JF.
Zama za Magufuli zilishakwisha, na Magufuli hayupo tena, ni mfu.

Usilazimishe mambo, soma alama za nyakati, wewe jua tu mtawala wa sasa ni mama Samia Suluhu. Ndio rais wa sasa, tutake au tusitake tutaucheza muziki wake.
 
Tofauti itakuwepo Mama Samia atakapoendelea kuzingatia katiba na sheria. Na ameanza na TAKUKURU, amewaambia kesi zote zisizokuwa na msingi na zile za kubambika wazifute. Najua anajua kesi za namna hiyo zipo, na TAKUKURU wanajua hivyo pia. Ni mwanzo mzuri na ni tofauti ya dhahiri na mtangulizi wake.
Sawa.

Time will tell...
 
Siku 21 bado sana
tapatalk_1607940808235.jpeg
 
Chama kilekile.

Ilani ileile.

Katiba ileile.

Watu ni walewale kasoro mmoja tu.

I am sober. I am managing my expectations.

Sitegemei tofauti kubwa.
Kama Magufuli aliweza kubadiri upepo kwa kiasi kikubwa na kila mtu akawa mwimba mapambio isipo kuwa baadhi mitandaoni tu.

Kwa nini usiamini huyu mama naye anaweza tenda yaliyo mema kwa watu wake kwa kasi ile ile.
 
yaani, unafikiri kuna mtu anaweza kunituma kuandika kitu? yaani wiki hii tu tayari mmejua hakuna tena ubabe au kutishana maisha... ngoja awageuka mtamsemaaaa...
Hawa vijana wa bavicha ni wajinga Sana, na mbaya zaidi huu ujinga umefika Hadi kwa viongozi wao wakubwa. Wamesahau kabisa kuwa mama Samia ni CCM, na wanaonyesha kuwa ccm bado Kuna viongozi wengi wazuri na unabaki unajiuliza hivi 2025 watasimamisha mgombea?
 
Ni wazi hujui tofauti ya kinachotokea kufuatia uchaguzi na hili lililotokea.. ntaacha wengine watusaidie.

Tofauti ipo Ndio maana kuna mtu kaondolewa kwa haki kupisha uchunguzi huko Bandari.

Enzi za Mzee wa kujimwambafai alikuwa akiwatimua watumishi kwa kutazama vigezo vya ukabila,ukanda........ Mama hamwonei mtu anatoa nafasi ya uchunguzi halafu unahukumiwa kwa haki.

Enzi za Mwendazake kulizuka vikundi vya wasiojulikana ambavyo kazi yake kubwa ni kuwashughulikia wale wote waliomkosoa.Kulizuka aina ya viongozi wa ajabu ajabu wauwaji hadi wakazuiliwa kukanyaga USA.

Mama kamwe hawezi kujenga Chake Chake International Airport
 
Wamuache achague Makamu wa Rais ambaye ataweza kufanya naye kazi, atakayeweza kumuamini, na ambaye likitokea lolote basi anaweza kuishikilia nchi.


Na muhimu zaidi ni lazima awe mtu ambaye aliamini katika ajenda ya Magufuli na si nje ya hapo, maana wakati wa kampeni walinadi ajenda moja.
 
Mkuu hii ndio makala yenyewe au ni sehemu ya makala? Angalau kwa hotuba ya leo SSH sio JPM hata kwenye matamshi mfano tutaongeza wigo,tu(ni)
Ni kweli SSH ni ccm kama alivokuwa JPM ila kumsifia leo haimaanishi hatokosolewa kesho!
 
Back
Top Bottom