Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Asante sana..
Kuna kikundi cha wahuni marehemu kakiacha ndio kinaumia na hakina uhakika wa kuendelea kuwepo katika mazingira haya ya utawala wa sheria
 

 
Acha kumfananisha kiongozi wetu na mambo ya laana. Namshukuru Mungu ametuinua!
 
Walizoea kuishi kwa ujanjaujanja huku wakiwatengenezea wengine matatizo feki bila kuchukuliwa sheria
 

Kwa bandiko lako umejichanganya sana mkuu. Haiyumkiniki wewe ni mmoja katika wale pichani chini au japo binamu zako.

La msingi tambua hizi sasa ni zama mpya. Zama zilizoleta faraja kwa watanzania walio wengi. Zama hizi ni zama za maridhiano. Agenda za kuuwana na kufarakanisha watu hazina nafasi tena.

Umeyasikiliza mambo hapa?


Ya Chatto Inc? Zama hizo hazipo tena!

Ni furaha iliyoje kuwa ukurasa huu unatuleta wengi zaidi pamoja?

Wachache hawa na namlie tu. Machungu ya njaa za matumbo yenu tunayajua:





Nyuso hizo leo ndiyo zinatambua umuhimu wa katiba na institution madhubuti. Laiti wangejua au siyo?

Hiyo ndiyo habari yenyewe.
 
Unaota ndoto za mchana JIWE kashaenda na mambo yake yashakwenda,cheche tumeziona jana kwenye ripoti ya CAG kuhus madege,angekuwepo KICHERE asingethubutu kutaja hiyo hasara.
 

Hata hawa hawakuungi mkono wewe wala bandiko lako:


Pia hawa:







Sembuse wewe wakulungwa?

Si mseme tu msiotaka umoja na ustawi wa watanzania mmevurugwa!

Hizi ni zama mpya. Tanzania mpya inayohitajika na wengi ndiyo hii inayokubalika sasa.

Mama Samia anaungwa mkono na walio wengi zaidi na huo ndiyo ulio ukweli wenyewe.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Tatizo lako unadhani Magufuli alichukiwa na wapinzani pekee. Na usijitoe ufahamu kuwa Magufuli alilazimishwa tu kuwa na Mama Samia kama mgombea mwenza na hatimaye Makamu wake...
Lakini na wewe kiongozi wakati wa kampeni za 2015 si ulikuwa kwa Magufuli na ukawa unatuaminisha kwamba Magu ni bora kuliko Lowassa? Utanisamehe kama nimekuchanganya na Mzee Mwanakijiji, nakumbuka kama mlikuwa timu moja!
 
Sawasawa; na nadhani (niseme najua) kuna watu ambao walipenda ajenda ya Magufuli ili hawakupenda jinsi alivyokuwa anaiendesha maana ni kama alikuwa anajigongelea misumari miguuni huku akijaribu kukimbia...

Wacha kupotosha hajawahi kuw ana ajenda yenye maono na faida kw ataifa zaidi ya ajnda kuu ya UFISADI, n ainajulikana Duniani kote ukitaka kuiba wewe fanya Miradi ya ujenzi upige percent zako na ndicho anachokijua tokea akiwa waziri.
 
hupendi kufikiria
 
Lakini na wewe kiongozi wakati wa kampeni za 2015 si ulikuwa kwa Magufuli na ukawa unatuaminisha kwamba Magu ni bora kuliko Lowassa? Utanisamehe kama nimekuchanganya na Mzee Mwanakijiji, nakumbuka kama mlikuwa timu moja!
Ni Kweli Magu wa 2015 kurudi nyuma alikuwa bora kuliko Lowassa.

Hata mimi nilikuwa namkubali sana.
 
FM, hii hatari wanaitengeneza wenyewe. Sasa hivi walitakiwa waanze kujipanga kudai wanachotakiwa kudai.. wanatakiwa waujaribu uvumilivu wa Rais Samia.
MM, ni mapema mno kuwashutumu kuwa hawajipangi. Hasa ukizingatia platforms za wao kufanya hivyo ni chache mno. Sijakuelewa unaposema wanatakiwa waujaribu uvumilivu wake. Unataka watangaze maandamano? Ili iwaje? Katika mazingira ambayo watu wamewekwa ndani kwa kunywa ulanzi na Mheshimiwa Rais hajasema neno nadhani tayari ujumbe umefika.

Amandla...
 
Nitadharau hilo la kuniambia kuwa siwajui watanzania wakati mimi mwenyewe ni mtanzania.

Unamfokea kama ulikuwa unampelekea pesa za kutengeneza hilo daraja na hafanyi hivyo.

Kuna taratibu za kuwashughulikia watumishi wazembe, kufokeana hadharani si mojawapo.

Wengi tu walionewa kwa sababu viongozi wengi waliiga tabia hii. Na wengi hawakuishia kuwafokea tu bali wali wasweka ndani. Makandarasi wameswekwa ndani kwa kutokamilisha miradi wakati wanaidai serikali mabilioni!

Amandla....
 
Wazee wa Waraka mmeanza
Acheni mama atawale
 
Ni mapema mno kumpa hizo sifa. Alikuwa sehemu ya serikali ya marehemu Rais na hakuwahi kuonyesha kuwa hapendezwi na yanayoendelea. Watu wanakumbuka matamshi yake katika kampeni kuhusu shabaha za askari wao na ushindi wa chama chake. Muda ndio utaonyesha kama kweli ni tofauti au kama alivyosema mwenyewe, ni muendelezo wa utendaji wa aliyemtangulia.

Amandla...
 
Mlikurupuka! Sisi tuliokuwa tunajua tulibaki ngangari!
Lowassa hajawahi kuwa safi. Lakini Magufuli amewahi kuwa na afadhali.

Rangi halisi ya Magu ilianza kuonekana baada ya kupewa madaraka.

Ishtoshe genge lililotaka kumweka Lowassa Ikulu baadaye likawa linakula na kunywa Ikulu.

Rushwa, ufisadi ni vibaya ila kukoswa utu na UBINADAMU ni roho ya ajabu sana iliyodhihirika wakati wa Magu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…