Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Nafikiri watu hawajamuelewa mleta uzi kwamba anachomaanisha Madame President alikua mgombea mwenza na aliihubiri ilani ya Hapa Kazi Tu hivyo ni ilani hiyo hiyo itakayofanya kazi mpaka 2025 atakapogombea na kuja na ilani yake.

Hii ni ukweli ila nafikiri approach zitatofautiana.

Binafsi nafikiri dalili kuu ya kwamba approach yake itakua tofauti ni kuachia mtandao (twitter).
Mleta uzi yuko obsessed mnoo na Magufuli, Yaani yaliyotokea mpaka sasa haaamini kabisa.

Anatamani hata Magu afufuke ila ndio hivyo haiwezekani.

Wakati Magu haonekani alikuwa anatamani adorably kwamba, ' .......mara paaa Magu anatokea hadharani kwa zile mbwembwe zake anafanya ziara ua kushtukiza huku akiwa LIVE kwenye media"

Kwahiyo mleta mada amepata wenge, yaani sijui Magu aliwaahidi nini aisee.

Hapo alipo anataka tu kulazimisha Samia awe Magu, ili ajipe faraja ya nafsi jambo ambalo haliwezekani.

Hata mapacha hawawezi kabisa kuwa hivyo.

Magu is no more, get used to it.
 
Unaongea habari ya AJENDA YA MAGUFULI. Najiuliza hivi hiyo Ajenda ya Magufuli ni ipi hasa? Kuua Upinzani? Miundombinu... miundombinu... miundombinu? Kuimbiwa mapambio? Maendeleo feki ya 'wanyonge'? Naam, maendeleo feki ya'wanyonge'. Umachinga siyo tabaka halisi, bali ni dalili ya sera zilizofeli. Kukiwa na maendeleo ya kweli, hutakuwa na wamachinga, wala mamantilie wanaokera ambao wanalalama kunyanyaswa pale kituo kipya cha mabasi Mbezi Louis. Utakuwa na wajasiriamali wa kada mbalimbali.

Dawa sahihi ya umachinga na mamantilie ni sera sahihi kuhusu KILIMO, ambazo zitatupekeka kwenye viwanda vya ukweli.

Ajenda pekee ya Magufuli ni MAGUFULI. Chato. Usukumani. Ubabe, ubabaishaji. Anajijengea kutokosea, anajua kila kitu, kumbe mbinafsi na mbaguzi.

Unalazimisha Samia aendeleze UMAGUFULI. Kubana vyombo vya habari? Kubana Upinzani? Nani alikuambia Samia ni mshamba? Samia ni Samia bwashee, siyo fotokopi ya Jiwe.

Wengi tunapumua sasa baada ya kubanwa mbavu. Vyombo vya habari vinapumua, japo hajasema wazi, lakini tayari uelekeo unaonekana
 
Tatizo ni kwamba at least as of now tunaanza kuona mwanga fulani, hakuna tena hotuba za kibabe, hakuna kutishiana maisha, Hakuna hotuba za kejeli na kujimwambafyi. Mama samia toka ameapishwa mpaka leo amesimamia misingi ya utawala bora na kufuata katiba.

Anajaribu kila awezalo kubalance mambo yet unaleta propaganda zako kwamba hakuna lililobadilika na kuwa everything is the same.

Nakuhakikishia this is the beginning of the new era/regime na kama usipobadilisha attitude yako you will soon loose relevance katika jamii ya wasomi wa makala zako na hao wanaokutuma wataacha kukutuma tena maana you will have lost your purpose and eventually be of no any use to them.
Yaani kweli nimeamini watu wananunuliwa. Wapi yule Mwanakijiji aliyekuwa anajenga hoja kali? Huyu sasa ni feki, ana mawazo mgando. Kweli huu ni uandishi wa mkodishwaji, aliyepoteza mwelekeo
 
Mleta uzi yuko obsessed mnoo na Magufuli, Yaani yaliyotokea mpaka sasa haaamini kabisa.

Anatamani hata Magu afufuke ila ndio hivyo haiwezekani.

Wakati Magu haonekani alikuwa anatamani adorably kwamba, ' .......mara paaa Magu anatokea hadharani kwa zile mbwembwe zake anafanya ziara ua kushtukiza huku akiwa LIVE kwenye media"

Kwahiyo mleta mada amepata wenge, yaani sijui Magu aliwaahidi nini aisee.

Hapo alipo anataka tu kulazimisha Samia awe Magu, ili ajipe faraja ya nafsi jambo ambalo haliwezekani.

Hata mapacha hawawezi kabisa kuwa hivyo.

Magu is no more, get used to it.
Saaafi sana!
 
Kama kuna kilio kinachekesha basi ni hiki cha Pro Magufuli people. Hawaelewi wanalia nini na hawajui walieje na wasililie nini. Ni wazi wanataka sana kuonekana wanamuunga mkono Rais Samia, lakini wanashangaa mbona ghalfa kila mtu anamuunga Rais Samia mkono, Wanatamani awepo wa kumkosoa kwa niaba yao sababu inaonekana hawana guts za kutoka hadharani kumkosoa Rais Samia hasa kwa namna alivyoanza, Wanatamani kuwasukumizia zigo la upinzani wao kwa wapinzani wa Chama.

Mnatukumbusha kuwa CCM ni ile ile, kwani hatufahamu? CCM ni ile ile ila utashi wa kiuongozi mkuu ndio unaoangaliwa, Rais Samia amechukua uongozi kwa mujibu wa katiba na hajashindana na mtu yeyote mnataka apingwe mapema yote hii kwa sababu gani? Kwa namna alivyoanza lazima aungwe mkono, akikosea baadae atakosolewa vile vile.

Halafu muache kujitoa ufahamu kuwa waliokuwa wanampinga JPM ni wapinzani pekee, JPM alikuwa anapingwa na watu wote wanaothamini Utu, demokrasia na utawala bora, Wasiopenda mabavu, double standards, masimango, kauli mbovu za kiongozi mkuu, na mengi kama hayo.
 
FM, hii hatari wanaitengeneza wenyewe. Sasa hivi walitakiwa waanze kujipanga kudai wanachotakiwa kudai.. wanatakiwa waujaribu uvumilivu wa Rais Samia.
Mzee, Wakati wanaujaribu uvumilivu wa JPM uliwaunga mkono?
Wakati wanadai walichotakiwa kudai wakati wa JPM uliwaunga mkono au uliwapinga kwa kumpinga JPM? Kama uliwapinga, unadhani kwanini sasa hivi unawataka wadai hiko unachotaka wakidai kwa Rais Samia? Je wakianza kudai utawaunga mkono au utajisogeza kwa Rais Samia uanze kumtetea na kujikomba.

Maswali haya yanalenga kuhoji nia yako ya kuwataka wapinzani waanze kujipanga kudai wanachotakiwa kudai. Halafu kumbe wana CCM siku hizi mnawafundisha wapinzani namna ya kufanya siasa zao!
 
Mleta uzi yuko obsessed mnoo na Magufuli, Yaani yaliyotokea mpaka sasa haaamini kabisa.

Anatamani hata Magu afufuke ila ndio hivyo haiwezekani.

Wakati Magu haonekani alikuwa anatamani adorably kwamba, ' .......mara paaa Magu anatokea hadharani kwa zile mbwembwe zake anafanya ziara ua kushtukiza huku akiwa LIVE kwenye media"

Kwahiyo mleta mada amepata wenge, yaani sijui Magu aliwaahidi nini aisee.

Hapo alipo anataka tu kulazimisha Samia awe Magu, ili ajipe faraja ya nafsi jambo ambalo haliwezekani.

Hata mapacha hawawezi kabisa kuwa hivyo.

Magu is no more, get used to it.
Yes
 
Acha UPUUZI WAKO wewe kikaragosi cha jiwe. Kama kuona huoni hata masikio hayasikii pia? Hakuna tena Tanzania ya Magufuli ingiza huo ukweli akilini mwako acha KUJITOA UFAHAMU eti bado ni Tanzania ya dikteta.
 
Nafikiri watu hawajamuelewa mleta uzi kwamba anachomaanisha Madame President alikua mgombea mwenza na aliihubiri ilani ya Hapa Kazi Tu hivyo ni ilani hiyo hiyo itakayofanya kazi mpaka 2025 atakapogombea na kuja na ilani yake.

Hii ni ukweli ila nafikiri approach zitatofautiana.

Binafsi nafikiri dalili kuu ya kwamba approach yake itakua tofauti ni kuachia mtandao (twitter).
Wewe umemuelewa vizuri sana. Na hivyo ndivyo nilivyomuelewa mimi pia.

Tatizo la wengi naona wanatumia hisia zaidi ya akili.

Ni vigumu ku reason na watu wa hivyo.
 
Kuna kautofauti fulani kapo na ndo kalichokuwa kanahitajika, Magufuli amefanya vizuri katika nyanja mbalimbali ila upande wa demokrasia alifeli pakubwa sana na upande wa uwazi wa serikali alifeli sana, hili kwa mama naona linaonesha uelekeo mzuri sana japo ni mapema mno ila acha tuzidi kuangalia
 
Mimi nipo na [emoji897] naangalia hizi moves! Speculations, determinations, Political analysis atmosphere [emoji41] ...ngoja niongeze na [emoji477]
Mlikimbia kumfuata JPM sasa hivi hamuelewi mkimbilie wapi na mfuate nani.. watu waliokuwa wampinga JPM na sasa wanamuunga Mama mkono .. mmeanza kuwafuata na kuwatabiria kugeuka.. poleni sana.. Mlikotoka mliharibu mlikokimbilia hamuaminiki tena.
 
Back
Top Bottom