Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Nilipokuwa chuo kuna kitabu nilisoma kinachoelezea historia ya waliopigania uhuru was Tz,kitabu kilielezea jinsi Nyerere alivyoende Uganda kusoma,akawa mwalimu,anaenda dar kwa mara ya kwanza na watu waliompokea,harakati za kudai Uhuru na kwanini Nyerere alichaguliwa kuwa kiongozi wa mapambano ya kudai Uhuru, kuna akina Bibi Titi wameelezwa kiundani humo,toka hapo niliona Nyerere ana mchango wa kawaida sana ktk harakati za kudai Uhuru wetu,kuna historia za watu wengi hazielezwi mtaani ila kila kitu Nyerere
 
What did you smoke? Ujamaa isn't natural and isn't that old. If it was, we could have seamlessly fitted in without the use of force.

Kwanini una ndugu, unawasaidia, unasaidia kijiji chako, kuhrsibiwa. Kila nwaka?
 
Ubepari ndio mfumo sahihi aliotupa Mwenyezi Mungu kwa maana matajiri na masikini wanayo chance sawa ya kuwa masikini au kuwa matajiri ni uamuzi tu
 

Mfumo wa uchumi wa kijamaa afrika hauwezekani sababu mwafrika ni mvivu. Wakoloni ndio walienda na mfumo sahihi wa kuwalazimisha watu kufanya kazi direct au indirect. Mfano ukitengeneza ajira kwa kuanzisha estates, viwanda, fursa, uhakika wa soko, hapa watu watafanya kazi.
 

Asante mkuu Malcolm Lumumba.

Naamini unaweza kutujulisha juu ya suala la Kambona na Wareno(wakoloni wa Msumbiji)

Kwamba Kambona alifanya makubaliano na hao Wareno wamsaidie kumpindua Nyerere na yeye angeacha kuwaunga mkono wapigania uhuru wa Msumbiji.

Niliisoma hii kwenye magazeti ya zamani ya familia yangu na sina hakika na ukweli wake.
 

Mkuu ruaharuaha.


What is the greater good for the society?

And please, who determine that this the greater good for any particular society?
 
Hizi tuhuma unazozileta hapa ni nzito sana, ila siyo mpya: Zinaweza zikawa zina ukweli au wongo vilevile.
Wengine hudai Kambona aliungana na Wareno, kuna kipindi wakapitisha ndege ikatupa flyers zinamkashifu Nyerere.
Zote hizi ni tuhuma, hivyo ili kambona ahukumiwe (Post-Humously) ni lazima utolewe ushahidi kuhusu usaliti wake.

Jambo ambalo halituingii wengi akilini ni hili:
Kama Kambona alikuwa anaonea kijicho nafasi ya Nyerere, nini kilimzuia kumuondoa Nyerere mwaka 1964 ???
Ikumbukwe kama Waziri wa Ulinzi Kambona alikuwa ndiyo The Most Influential Figure in the new Republic !!!
Lakini yeye na Lusinde ndiyo walienda kuwaomba Waingereza watume msaada wa kuyazima mapinduzi.
 
Hii nchi kuna mambo mengi yamefichwa kwa faida ya watu wachache ...

Na sio huyo tu kuna wengi hawazungumzwi mbaya zaidi kizazi kinachojua historia kinapotea bila kuanika wazi haya mambo
 
Hii nchi kuna mambo mengi yamefichwa kwa faida ya watu wachache ...

Na sio huyo tu kuna wengi hawazungumzwi mbaya zaidi kizazi kinachojua historia kinapotea bila kuanika wazi haya mambo
 
na walisema pia alipokimbia aikimbia na pesa nyingi sana ila wanasema jamaa aliishi maisha magumu sana uko uingereza akawa anafanya kazi za kipato cha chini ili aweze kutunza familia huku nyerere & co wanasema opposite
 
na walisema pia alipokimbia aikimbia na pesa nyingi sana ila wanasema jamaa aliishi maisha magumu sana uko uingereza akawa anafanya kazi za kipato cha chini ili aweze kutunza familia huku nyerere & co wanasema opposite
Wanasema alikimbia na shilingi laki saba za miaka hiyo,
Sasa unajiuliza kama Raisi Nyerere alikuwa analipwa mshahara elfu sita (6000),
Hizo laki saba Kambona aliziibaje na anavyoondoka aliziweka sehemu gani maana ni pesa nyingi sana.

Lakini tuseme kweli Kambona aliziiba hizo pesa,
Mbona serikali ya Tanzania haikuamua kuomba EXTRADITION ya Kambona kutoka Kenya ambako alikimbilia awali ???
Ikumbukwe mwaka 1967 Kenya alikuwa nchi mwanachama wa EAC ya kwanza hivyo walikuwa na Extradition Treaty.

Kama kulikuwa na Extradition Treaty baina ya nchi wanachama wa Africa Mashariki,
Kwanini serikali ya Nyerere haikuamua kuomba Kambona mkwapuaji akamatwe na kurudishwa nchini ???
Ikumbukwe serikali ya Nyerere ilikuwa inaomba msaada wa kukamata wahalifu wengi sana kutoka nje ya nchi.

Hapa unapata jibu moja la haraka:
THE ABSENCE OF OSCAR KAMBONA was duly welcomed by top bureaucrats the likes of Nyerere & Kawawa.
OTHERWISE wasingemuacha hata kama angekuwa uhamishoni, laki saba ya kipindi hicho ilikuwa pesa kubwa mno.
 
Mkuu ruaharuaha.


What is the greater good for the society?

And please, who determine that this the greater good for any particular society?
Greater benefits to society
Something beyond and above personal interest. (Kujali maslahi ya umma zaidi maslahi yako binafsi.)
 
and yet aliwaambia wadhibitishe kama ni kweli aliondoka na hilo pesa ila walishindwa, kusema ukweli sasa hivi namuona nyerere alikua ni advocate wa shetani na ni kiongozi mbovu zaidi kuwahi kuwepo ktk historia ya tanzania
 
nafkiri aliona hatokua salama ndani ya nchi yoyote ya afrika and the funny thing ni kwamba aliishi maisha ya ukata sana lakini huku nyumbanni nyerere & co. walisema Mkwanga unaonekana. It was a shame this giant was struggling.
Mkwanga unaonekana.
 
and yet aliwaambia wadhibitishe kama ni kweli aliondoka na hilo pesa ila walishindwa, kusema ukweli sasa hivi namuona nyerere alikua ni advocate wa shetani na ni kiongozi mbovu zaidi kuwahi kuwepo ktk historia ya tanzaniaHui
Hujinui, usitumie neno shetani, unajua madaraka yana tuyevya. Hata wewe ungekuwa hivyo hivyo ukipata madaraka


Muhimu kuwe na sheria ku limit power (unfetted power.)
 

Asante mkuu.

Sio tuhuma. Ni habari tu kwenye magazeti ya nyakati hizo ambayo hata hayakuwa na uhusiano na serikali ya Tanzania.

Madai ya wanahabari hao ni kuwa Kambona alichukua pesa za wareno takribani shilingi elfu thelathini ambazo kwa wakati huo zilikuwa si haba. Akaenda nazo UK katika matayarisho ya hiyo coup d’etat.

Lakini baada ya muda wareno wakagundua kuwa jamaa anaishi London kama playboy na hakuna mipango yoyote ya mapinduzi.

Ndipo wareno walipodondosha fliers mpakani mwa Tz na Msumbiji zikionesha makubaliano yao na Kambona na baada ya hapo Nyerere akamcharukia best wake.

Mkuu Malcolm nimeileta kama nilivyoisoma na nimeikumbuka tu kwa sababu ya huu uzi. Huenda ilikuwa propaganda chafu dhidi ya Kambona au conspiracy theory tu ya watu fulani. Kwa kweli sijui.

Ila kwa maoni yangu hawa icons wetu yaani Mwl Nyerere na Oscar Kambona walichanganya sana urafiki binafsi na majukumu yao kama viongozi kiasi ambacho ukweli wa haya masuala unakuwa mgumu kupatikana.

Tukumbuke pia kuwa tofauti kali kati ya hawa wawili zilijitokeza zaidi baada ya Azimio la Arusha ingawa ni wazi kuwa Nyerere alikuwa tayari ana mashaka na Kambona baada ya lile jaribio la mapinduzi la 1964.

R I P Mwl J K Nyerere(a great African revolutionary scholar among other things)

R I P Oscar Kambona( A truly charismatic leader whose story has never been told in full).
 
Suala la pesa lilikuwa ni stori tu baada ya tukio lenyewe la Kambona kukimbilia uhamishoni.

Maana hata huyo Kambona alikuwa anasema Nyerere alificha pesa nyingi sana nje ya nchi, jambo ambalo mpaka leo inaonekana siyo kweli.
 
walikua close kana kwamba hakuna mtu aliyeweza kusimama mbele ya mwalimu na kumuambia unachofanya sio, inasemekana the rest walikua ni wazee wa ndio mzeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…