Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Ntakitafuta na nitakisoma lakini, kwa uliachinda hapa kambona alikua anapigania maslahi yetu, na ni kwanini ndugu zake waliteswa na kuuwawa kwa kitu wasichohusika nacho?
 
shukran sana umetufumbua Macho japo nawewe haupo deep sana yan kama umehadithiwa au umeskia mahala then ukaja kutuambia.

please anayefahamu vizuri historia ya huyu mtu (Kambona) atiririke, tujue alizaliwa wapi, amesoma wapi, alikua na nyadhifa zipi , kafa mwaka gani. Pia atueleze tz ya sasa kipi kimefanyika ambacho Kambona alikiona na Nyerere alikuwa hakiamini

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Kumbe hata Mwenyeheri alikuwa na mitusi kama ' mitano tena'

Unamwitaje mwenzio Malaya kisa tu ana mawazo tofauti na wewe

1984 Mzee Jumbe alikataa kutukaniwa Mama yake akaona kuliko kumezea bora nijibu na liwalo na liwe

Kina Seif Hatib na Msekwa wanakumbuka mengi

Waliishia kumpaka matope.
View attachment 1665493
 
shukran sana umetufumbua Macho japo nawewe haupo deep sana yan kama umehadithiwa au umeskia mahala then ukaja kutuambia.

peleas anayefahamu vizuri historia ya huyu mtu (Kambona) atiririke, tujue alizaliwa wapi, amesoma wapi, alikua na nyadhifa zipi , kafa mwaka gani. Pia atueleze tz ya sasa kipi kimefanyika ambacho Kambona alikiona na Nyerere alikuwa hakiamini

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
nimekusanya dots za hapa na pale nikasoma stories zake , cha ajabu wale ambao walishuhudia haya yote kwa macho yao huwezi kuskia wakiongelea haya mambo watuambie ukweli
 
shukran sana umetufumbua Macho japo nawewe haupo deep sana yan kama umehadithiwa au umeskia mahala then ukaja kutuambia.

peleas anayefahamu vizuri historia ya huyu mtu (Kambona) atiririke, tujue alizaliwa wapi, amesoma wapi, alikua na nyadhifa zipi , kafa mwaka gani. Pia atueleze tz ya sasa kipi kimefanyika ambacho Kambona alikiona na Nyerere alikuwa hakiamini

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Nimesoma historia ya Huyu jamaa kidogo miaka ya nyuma, nitaelezea kidogo nachojua, Oscar S. Kambona alizaliwa Songea, Kambona na Nyerere walikutana Tabora boys, Baadae Kambona alipata Scholarship ya Gavana na kwenda kusoma uingereza, Baada ya Tanu kuanzishwa, Nyerere alimuomba Kambona arudi Tanganyika ili kuongeza nguvu kwenye chama, baada ya Uhuru, Mwalimu alipendelea zaidi mfumo wa ujamaa aliiona China alipofanya ziara nchini chini ambayo kipindi hiki ilikuwa chini ya utawala wa Mao Ze Dong, Kambona hakupenda Sera ya ujamaa, Tofauti ilianzia hapo, Baadaye wakati vuguvugu la vyama vingi lilipoanza, Kambona alipendekeza vyama vingi na mwalimu

Hakupendelea mfumo huo, Kambona aliamini Tanu ingeshinda maana ilikuwa inapendwa na wananchi na pia alisema endapo watu wataichoka Tanu, basi watakuwa hawana haki ya kuitoa Tanu kwa mfumo uliokuwepo wa Chama kimoja, Baada ya tukio la uasi lilifanywa na jeshi mwaka 1964, Nyerere alikimbilia kigamboni na Kambona alifanikiwa kuzima uasi huo, Baada ya Nyerere kurudishwa Ikulu, Washukiwa walioratibu uasi walianza kukamatwa akiwemo mwanamama Bibi Titi, mwanamke aliyeipambania sana Tanu.

Kambona baada ya kutonywa kwamba atakamatwa aliamua kukimbilia Kenya na familia yake kisha kuelekea Uingereza, Waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo, Agustino Lyatonga Mrema, aliwaambia wananchi kwamba Kambona atakapokanyaga Tanzania, atashtakiwa, Mdogo wake Kambona, Otini Kambona alikamatwa bila na kuswekwa ndani bila kusomewa kesi yoyote, Bibi Titi alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani japo baada ya mwaka mmoja alisamehewa kwa msamaha wa rais, Bibi titi alifariki mwaka 2000 nchini Afrika kusini, Kambona

Alirudi Tanzania mwaka 1990's na hakukamatwa ila serikali ilisema jamaa si Mtanzania, hivyo alitakiwa kuthibitisha uraia wake,katika utawala wa Nyerere Kambona alikuwa Waziri wa mambo ya ndani, Kambona alifariki mwaka 1997 na serikali ilishughulikia msiba wa Kambona na alizikwa kwa heshima zote. Niko tayari kusahihishwa wakuu, ahsanteni

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
nchi nyingi kua na changamoto nyingi kuliko TZ haimanishi tupo nafasi nzuri, Tungeweza kufanya vizuri zaidi ya hapa lakini tulifeli kwasababu ya mtu mmoja

Kupanga ni kuchagua! Wengi wa wale walioanza na ideology ya Ubepari wakati nchi zao bado ni changa wameishia kupata matabaka either ya kikanda au kikabila! Inawezekana ukaona kuwa tumechelewa sana lkn amini kuwa misingi aliyoijenga mwalimu ndio leo tupo wamoja hivi unavyoona hatuulizani makabila wala dini. Sasa kama kujenga nchi tuanzie hapo baada ya kujenga Amani na Umoja wa Kitaifa.
 
Ni kweli kabisa kwa unavyoona kati ya mwalimu na nyerere nani alikua sahihi?
 
Kambona alikuwa Katibu Mkuu wa TANU anayehubiri Ujamaa kwa muda mrefu sana.

Wanaosema alipingana na Nyerere kwa sababu ya Ujamaa inabidi waje na detail zaidi.

Kambona deserves his own book. But I did learn a lot regarding this period from Paul Bjerk's "Building A Peaceful Nation: Julius Nyerere And The Establishment of Tanzania 1960-1964".

Nn ilikuwa chanzo cha ugomvi wa Hawa mabestman wawili
 
Ile nyumba ya Kambona alipewa Obote wa Uganda, wakati alipokuja huku baada ya kupinduliwa na Amin wa Uganda.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
OK. Nilijua Obote alipewa nyumba ya serikali, ila for some reason nilifikiri ilikuwa karibu na St. Peter's.

Ila kuna wakati familia ya Kambona walirudishiwa ile nyumba. Nafikiri ilikuwa wakati Mwinyi anarudisha baadhi ya nyumba zilizotaifishwa na serikali.

Niliwahi kwenda pale na rafiki zangu walikuwa wanakwenda kumsalimia rafiki yao Neema Kambona alikuwa anaishi pale. Ndipo nilipojua kwamba kumbe Kambona na Nyerere walikuwa majirani wa siku nyingi sana.
 
Kosa kubwa la Nyerere ni kuwachukia wakoloni na mazuri yao pia. Ilitakiwa achukue mazuri mabaya aayache.

Mfumo sahihi wa kiuchumi ni ule wa kikoloni ( nguvu Kazi ktk uzalishaji, wote lzm wazalishe)
 
Kupanga ni kuchagua! Wengi wa wale walioanza na ideology ya Ubepari wakati nchi zao bado ni changa wameishia kupata matabaka either ya kikanda au kikabila! Inawezekana ukaona kuwa tumechelewa sana lkn amini kuwa misingi aliyoijenga mwalimu ndio leo tupo wamoja hivi unavyoona hatuulizani makabila wala dini. Sasa kama kujenga nchi tuanzie hapo baada ya kujenga Amani na Umoja wa Kitaifa.
kwa hiyo ni kama tulichagua umasikini na umoja dhini ya maisha bora and it was a wrong choice! kwa nje nyerere alikua anaonekana anahubiri umoja kwa sababu alituona ni "mafala" lakini kwa undani nyerere aliwakamata kuwatesa na kuwafunga watu waliompinga na alikokua anaona ni tishio kwake kisiasa! mfano mzuri ni kaka zake na kambona ambao hata hawakua wanasiasa ila waliteswa na kufungwa
 
OK. Nilijua Obote alipewa nyumba ya serikali, ila for some reason nilifikiri ilikuwa karibu na St. Peter's.

Ila kuna wakati familia ya Kambona walirudishiwa ile nyumba. Nafikiri ilikuwa wakati Mwinyi anarudisha baadhi ya nyumba zilizotaifishwa na serikali.

Niliwahi kwenda pale na rafiki zangu walikuwa wanakwenda kumsalimia rafiki yao Neema Kambona alikuwa anaishi pale. Ndipo nilipojua kwamba kumbe Kambona na Nyerere walikuwa majirani wa siku nyingi sana.

Sio jirani tu ni ndugu wa kupika na kupakua, sema tu walitofautiana ideology tu
 
Kila mlengo unafaida na hasara zake, Mwalimu kwa Sera ya ujamaa angalau Ardhi, elimu na afya tunafaidi japo kadri miaka inavyosonga Elimu inakuwa ghali kuipata ile nzuri, Ubepari nao unamabaya yake waone Kenya na Zambia baada ya Rais Kaunda ndo utajua kwanini kila Sera inamabaya na mazuri yake
 
kwa hiyo ni kama tulichagua umasikini na umoja dhini ya maisha bora and it was a wrong choice! kwa nje nyerere alikua anaonekana anahubiri umoja kwa sababu alituona ni "mafala" lakini kwa undani nyerere aliwakamata kuwatesa na kuwafunga watu waliompinga na alikokua anaona ni tishio kwake kisiasa! mfano mzuri ni kaka zake na kambona ambao hata hawakua wanasiasa ila waliteswa na kufungwa
Nyerere alikuwa ni cold blood dictator sema ni dictator aliyekung'ata anapuliza na sio pure dictator.
 
nimesusanya dots za hapa na pale nkasoma stories zake , cha ajabu wale ambao walishuhudia haya yote kwa macho yao huwezi kuskia wakiongelea haya mambo watuambie ukweli
ok shukran kk. ukiachana na kuamini ubepari na mfumo wa vyema vingi, kipi kingine kinacho fuction now ambacho Kambona ali dream kipindi iko?

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom