nifute tongotongo, tanzania oneni nani
Baada ya hapo, zilifuata kampuni ndogo ndogo kama KTN OIL [kampuni mwenza wa KTN INDUSTRY pamoja na kituo cha televisheni cha KTN kinachopatikana nchini KENYA], SIMBA OIL, KILIMANJARO OIL, PETROCOM, BIG BON na MSN OIL, pia ilipatikana kampuni mpya ya mafuta iliyokuwa inaitwa AFROIL.
Hii kampuni ya AFROIL ni kampuni kubwa kwa kiasi chake na inafanya vizuri kwa upande wa kibiashara.
Baada ya kampuni ya mafuta ya AFROIL, ilifuata kampuni ya LAKE OIL na kufanya kuwa na idadi sita [6] za kampuni kubwa ambazo zinajishughulisha na MAFUTA YA PETROLI, DIZELI NA MAFUTA YA TAA.
Kampuni hizo ni MOIL, MERU OIL, OILCOM, CAMEL OIL, AFROIL na LAKE OIL. Kampuni nyingine ni ndogo ndogo, ijapokuwa SIMBA OIL imeshavuka mipaka na sasa hivi inamiliki vituo vya mafuta nchini ZAMBIA.
Pia kuna kampuni za usafirishaji wa MAFUTA YA PETROLI, DIZELI NA MAFUTA YA TAA ambazo pia zipo nyingi.
Hii kampuni ya kusafirisha MAFUTA YA PETROLI, DIZELI NA MAFUTA YA TAA inayoitwa BLUECOAST bado ni ngeni kwenye biashara na hauwezi kufananisha na kampuni kama PRIME FUELS au DALBIT.
Sasa hivi WATANZANIA wengi wamewekeza kwenye SEKTA YA MAFUTA YA PETROLI, DIZELI NA MAFUTA YA TAA na kupunguza ile nguvu ya kampuni za kigeni iliyokuwepo tangu kipindi cha miaka ya sitini [1960's].
Kwahiyo wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VIKUU VYA USHIRIKA VYA MWANZA, SHINYANGA na TABORA yaani MWASHITA wamejitahidi sana kuwekeza kwenye SEKTA YA MAFUTA YA PETROLI, DIZELI NA MAFUTA YA TAA na hawa ndiyo walioshikilia hii sekta.
Ijapokuwa kampuni kama TOTAL, BP, GBP, ESSO, ENI [AGIP] na ORYX ENERGIES wanamiliki VISIMA VYA MAFUTA na wamewekeza sehemu mbalimbali za duniani, lakini bado soko la ndani kwa upande wa TANZANIA limeshikiliwa na wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VIKUU VYA USHIRIKA VYA MWANZA, SHINYANGA NA TABORA yaani MWASHITA.