Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

walikua close kana kwamba hakuna mtu aliyeweza kusimama mbele ya mwalimu na kumuambia unachofanya sio, inasemekana the rest walikua ni wazee wa ndio mzeee

Mkuu shukrani kwa huu uzi.

Hata kama ukweli wa Oscar Kambona hautajulikana vizuri leo au kesho, bado historia ni mwalimu mzuri na kuna mengi ya kujifunza katika huu uzi na michango ya wadau.

Moja ya hayo ni kutenganisha majukumu ya uongozi wa umma na mahusiano binafsi kama urafiki, undugu wa damu, mapenzi n.k
 
Mfumo wa uchumi wa kijamaa afrika hauwezekani sababu mwafrika ni mvivu. Wakoloni ndio walienda na mfumo sahihi wa kuwalazimisha watu kufanya kazi direct au indirect. Mfano ukitengeneza ajira kwa kuanzisha estates, viwanda, fursa, uhakika wa soko, hapa watu watafanya kazi.
kwenye vijiji vya ujamaa watu walifanyishwa kazi kwa nguvu...mbona mafanikio hayapo?
 
Asante mkuu.

Sio tuhuma. Ni habari tu kwenye magazeti ya nyakati hizo ambayo hata hayakuwa na uhusiano na serikali ya Tanzania.

Madai ya wanahabari hao ni kuwa Kambona alichukua pesa za wareno takribani shilingi elfu thelathini ambazo kwa wakati huo zilikuwa si haba. Akaenda nazo UK katika matayarisho ya hiyo coup d’etat.

Lakini baada ya muda wareno wakagundua kuwa jamaa anaishi London kama playboy na hakuna mipango yoyote ya mapinduzi.

Ndipo wareno walipodondosha fliers mpakani mwa Tz na Msumbiji zikionesha makubaliano yao na Kambona na baada ya hapo Nyerere akamcharukia best wake.

Mkuu Malcolm nimeileta kama nilivyoisoma na nimeikumbuka tu kwa sababu ya huu uzi. Huenda ilikuwa propaganda chafu dhidi ya Kambona au conspiracy theory tu ya watu fulani. Kwa kweli sijui.

Ila kwa maoni yangu hawa icons wetu yaani Mwl Nyerere na Oscar Kambona walichanganya sana urafiki binafsi na majukumu yao kama viongozi kiasi ambacho ukweli wa haya masuala unakuwa mgumu kupatikana.

Tukumbuke pia kuwa tofauti kali kati ya hawa wawili zilijitokeza zaidi baada ya Azimio la Arusha ingawa ni wazi kuwa Nyerere alikuwa tayari ana mashaka na Kambona baada ya lile jaribio la mapinduzi la 1964.

R I P Mwl J K Nyerere(a great African revolutionary scholar among other things)

R I P Oscar Kambona( A truly charismatic leader whose story has never been told in full).

Nyerere alikuwa scholar wa kitu gani?
 
Hizi comments zindhihirisha namna gani Watanzania wengi tulivyojaa upumbavu.

Wengi humu wala hawajawahi kufuatilia historia yoyote, na wanarukia tu hoja zinazotolewa humu na kuzitolea hisia zao.

Inashangaza kuna mengi yaliyokuwa yanavumishwa tu na Watu wenye malengo yao na bado kuna Watu leo hii wanayarudisha na yakisomwa na kizazi kipya chenye upeo finyu wanaishia kuhemuka....kuna moja ya hotuba Mwalimu aliongea kwa hisia sana kuhusu uvumi uliokuwa unazuka kila kukicha nchini wakati huo na haswa kiini kikiwa hapo Dar es salaam.....alitoa mfano wa uvumi wa kuwa yeye anajiuzulu na kuhamia Uingereza na Wavumi walitoa hata safu mpya ya Uongozi.

Kiufupi kuna ombwe kubwa sana kwenye historia yetu na hii inawapa fursa wapotoshaji kuingiza fikra zao wakitumia vibaya ufahamu haba wa kizazi kilichopo.
 
Watu kushangilia kufeli kwa siasa za Mwalimu ni ushahidi tosha kuwa Waafrika/Waswahili hawakuwa/hatuko tayari kujitegemea.

Mwalimu aliamini kuwa chochote anachoweza kufanya Mzungu basi na Mswahili anaweza....kumbe hakuwa sahihi maana asili ya Mtu mweusi ni Mvivu, tegemezi na hana ubunifu.

Hivi kweli kuna Kizazi kinacholalama kwamba kwa nini Mwalimu alifunga milango tusipate sabuni na colgate zilizotengenezwa na Wazungu?, kabla ya Wazungu tuliishije?, yaani kuonjeshwa tu vya Wazungu basi tukawehuka?.... hivi hatuoni aibu kuishi Dunia ambayo tuna Mjomba wa kumtegemea kwa mahitaji yetu? Hivi huyo Mzungu wakati anaanza yeye alimtegemea nani?

Hivi kweli tunampiga vita Mtu aliyejitoa kwa hali na mali kutaka kumjengea Mswahili imani ya kuwa anaweza kuishi bila Mzungu?.

Kuna hotuba moja Mwalimu anatoa mfano wa Raisi wa Korea aliyeitwa na Vijana wake wakamuoneshe Trekta walilotengeneza na kwa bahati mbaya wakati wanamuonesha Trekta lilirudi nyuma badala ya kwenda mbele...Raisi yule aliwapa moyo na kuwaambia endeleeni maana mkirekebisha kidogo tu Trekta litaenda mbele...Mwalimu alimalizia kama utani kwa kuomba na yeye Vijana watengeneze Trekta linalorudi nyuma....sasa nani angetengeneza Trekta ikiwa vichwa vyote vinamuangalia Mzungu?.

Hivi inahitaji elimu gani kujua maono ya Mwalimu yalikuwaje kwa Mtu Mweusi?

Baadhi ya comment humu zinatia simanzi sana kwa Mtu yeyote anayejithamini na kuamini kuwa naye ameumbwa na Mungu kama wengine na hakuja duniani kuwa Mtumwa wa mwingine.

Wakati anaomba uhuru Mwalimu alijigamba kwa Wakoloni kwamba baada ya miaka kumi warudi waone Mswahili alivyofanya makubwa, huku nao wakimkebehi kwamba hakuna chochote kitafanywa na Mtu asiyeweza kutengeneza hata sindano. Hivi leo tunashangilia kufeli kwa hilo?, sasa hiyo ni aibu ya Mwalimu au sisi wote?, hivi kweli tunaona fahari kumpa Mzungu ushindi wa kucheka na kuuliza "kikowapi Watumwa tu nyie?"

Hivi ni nini haswa dhambi ya ujamaa?, kwamba Watu mna imani za dini lakini hamtaki kuamini kwenye kuishi pamoja kupendana na kufanya kazi pamoja, kuvuna pamoja na kula pamoja?, kufeli kwa Ujamaa sio kufeli kwa Mwalimu bali ni kufeli kwa utu miongoni mwa binaadamu...hivi kuamini kwamba ni vibaya wewe ule ushibe na jirani yako alale njaa nalo ni kosa?.

Baada ya uhuru na wakati anataka kujenga umoja Mwalimu aliweka wazi kuwa hawezi kujenga taifa ambalo limegawanyika, ambapo sehemu ndogo ya Watu wake wanamiliki mali huku wengi waliobaki ni hohe hahe...tena wachache hao wenye uwezo walikuwa ni wa ngozi nyeupe....kwamba Wahindi waendelee na maisha yao kama kikundi fulani maalumu na bado Mwalimu ajigambe kuwa anaongoza nchi moja na huru? .

Hivi wangapi wanafahamu kuwa baada ya uhuru kulishaanza kuzuka fukuto kuhusu wasio na asili ya Tanzania?. Kuna Waswahili walianza kuhoji kuwa kama hawa nao ni Wenzetu mbona hatuwaoni kwenye shughuli mbali mbali kama maandamano n.k... na nani kama sio Mwalimu aliyesimama kidete kuhakikisha hilo jambo halipati nafasi?.

Na kama Wanalalamika kunyang'anywa majumba yaliyovunwa hapa hapa kwenye ardhi yetu, hivi si huyo huyo Mwalimu pia aliyewanyang'anya taasisi za dini shule zao ili tu hata wasio waumini wa dini hizo wakasome huko?.

Mfano hapa Arusha ile shule ya msingi Meru ilikuwa ni ya Wahindi tu, wakati sisi tunaanza shule ndio tulikuta kidogo kidogo kunaanza kuwa na uwiano wa Waswahili na Wahindi huku idadi ya Wahindi ikienda ikipungua kadri siku zilivyokuwa zinaenda...sasa je hivyo ndio tulitaka Mwalimu atawale taifa likiwa na hayo matabaka?.

Hivi ni kizazi gani cha kulaumiwa haswa, ni kile cha enzi ya Mwalimu au hiki cha sasa?. Marehemu Mzee wangu pamoja na kuwa Daktari alikuwa pia anajua useremala, nyumbani alikuwa ana cherehani na alikuwa ananunua kitambaa na anatushonea nguo Watoto wake...nyie kizazi cha sasa mnaoimbiana nyimbo za "binuka nipachike" na mnashangiliana kama Mazuzu ndio mnakaa chini na kuanza kulaumu nyakati za Mwalimu?.

Ni kama uingie kwenye nyumba iliyojengwa na mwingine na kuwekwa samani zote, wewe Mswahili unachotaka ni kuketi tu kwenye sofa laini miguu uweke juu na remote control ya TV ya inchi 60 mkononi, huku Mwenye nyumba Mzungu anakuhudumia chochote unachotaka, maziwa, mayai, Kuku n.k....na kweli bado unadhani hapo upo salama?

Na akijitokeza Mswahili Mwenzako kukwambia hivi sio sawa turudi kwenye ile nyumba yetu ya Msonge tushirikiane tuitengeneze iwe kama hii unaanza kumtukana kwa kukukatisha starehe na kukupeleka kwenye taabu?.
 
Hizi comments zindhihirisha namna gani Watanzania wengi tulivyojaa upumbavu.

Wengi humu wala hawajawahi kufuatilia historia yoyote, na wanarukia tu hoja zinazotolewa humu na kuzitolea hisia zao.

Inashangaza kuna mengi yaliyokuwa yanavumishwa tu na Watu wenye malengo yao na bado kuna Watu leo hii wanayarudisha na yakisomwa na kizazi kipya chenye upeo finyu wanaishia kuhemuka....kuna moja ya hotuba Mwalimu aliongea kwa hisia sana kuhusu uvumi uliokuwa unazuka kila kukicha nchini wakati huo na haswa kiini kikiwa hapo Dar es salaam.....alitoa mfano wa uvumi wa kuwa yeye anajiuzulu na kuhamia Uingereza na Wavumi walitoa hata safu mpya ya Uongozi.

Kiufupi kuna ombwe kubwa sana kwenye historia yetu na hii inawapa fursa wapotoshaji kuingiza fikra zao wakitumia vibaya ufahamu haba wa kizazi kilichopo.
ni kweli ,tufungue macho mkuu kama una chochote unachokifahamu kwasababu sisi tulishakuta mambo yamefanyika na sasa tunauliza kwanini hiki kilikua hivi? we need the answers
 
Tanzania ukiangali vita vyaMaji Maji vilipiganwa na makabila zaidi ya moja ya huko kusini ili kumtoa mkoloni hii inaonesha wazi watanganyika baadae watanzania walikuwa na umoja hata kabla ya uhuru.

Hii morali ya kuungana ili kupambana ingeweza kuendelezwa na System hata ndani ya Ubepari.
Eti Tanzania ilikuwa moja, unamjua Thomas Marealle wewe?
Sio kweli, tatizo lilianza pale tulipolazimisha mabepari kufuata siasa za kijamaa. Wengine wakakosa vyanzo vya mapato na utajiri wakaamua kuiba serikalini na kuwa mafisadi.

Kwa mfumo wetu wa ulinzi wala taifa hili lisingekufa. Tuna mfumo imara sana kiulinzi na watu wanafanya kazi kubwa mimi na wewe tuweze ku comment hapa.

Hili halina uhusiano na huo Ujamaa wala Ubepari
Mifumo hiyo ya ulinzi ina misingi ya ujamaa (nyumba kumi kumi).
 
Tangu nipo shule ya msingi tulikua tunaaminishwa kwamba Mlm Nyerere ndio "icon" pekee apa nchini, tulikua tunaimba nyimbo nyingi ni za kumsifu, lakini hatukuwahi kuambiwa kua kuna watu wengine ambao bila wao mwalimu "asingetoboa" na pengine tusingemjua kabisa mwalimu nyerere, au story yake ingekua "short lived". Mmoja wa hao watu ni OSCAR KAMBONA.

Nimezaliwa hapa Tanzania miaka ya 90 mpaka nimekua mtu mzima kila kitu ni Nyerere tu. Kambona nilimsikia badae sana baada ya kuskia kisa cha huyu mtu nikawa interested sana kufuatilia stories zake.

kwa mujibu wa maandiko Kambona alikua bega kwa bega na mwalimu ktk kudai uhuru yaani ilikua akitoka mwalimu anaefuata ni Kambona lakini huwezi sikia hichi kitu kinasemwa waziwazi na pengine bila mawazo na support ya kambona mwalimu "angefeli vibaya mno". Kambona ndio mtu aliezima mapinduzi yalioilenga serikali ya nyerere kutoka kwa askari waliotaka kuasi, yaani kwa ufupi ni kwamba Nyerere asinge endelea kua mtawala wa nchi hii kama sio Kambona.

Kambona aliona mbali kuliko mwalimu Tanzania ya sasa ndio aliyoiona kambona lakini mwalimu alipinga, Kambona aliona ubepari ndio utafanya kazi lakini mwalimu aliona ujamaa ndio unafaa, mwalimu "failed miserably" akatupeleka chaka mpaka leo we still pay for his "grave mistake". Mwalimu alikua mbishi na aliamini kwamba yeye ndio ana maono bora kuliko wengine ,chochote kile ambacho kilikua hakiendani na sera zake alikipinga hata kama kilikua "viable". Fikiria mtu mmoja tu kaenda urusi akafurahishwa na mfumo wa ujamaa akaja kuufanyia "experiment" hapa nchini na ukafeli kwasababu alikataa kusikiliza maoni ya watu wengine, kwa wakati huo mwalimu ndio alikua "kila kitu"

Kambona akatofautiana na mwalimu , yeye alitaka ubepari mwalimu alitaka ujamaa. Kutokana na ushawishi mwalimu alishinda japo kambona ndie aliekua sahihi lakini hawakumskiliza. Baadae mwalimu alijua amekosea akaturudisha kwenye Ubepari na bado akaonekana ni "hero" . Kitu ambacho oscar alikiona miaka kadhaa kabla wakati huo mwalimu alikua "blind" almost everyone was blind except the very few including Kambona

Haya leo 2021 TZ hii ya leo ndio kambona aliyoiona na tumechelewa sana, kwa mtazamo wangu bado tupo nyuma kwa miaka 15 kutokana na sera mbovu za mwalimu nyerere

Wote ni marehemu wapumzike kwa amani lakini, mwisho wa siku Oscar Kambona ndio AMESHINDA!!!!! Kwangu mimi shujaa wa kweli nchi hii ni OSCAR KAMBONA na sio mwalimu! Na ndio mtu muhimu sana sawa na mwalimu lakini ndio aliesahaulikia kuliko wote nchi hii, natamani watanzania wengi tuliozaliwa miaka ya 90 wajue habari za huyu shujaaa ambaye ni co-founder wa hii nchi kwangu mimi alichangia 50% ktk kutengeneza taifa hili sawa sawa na mwalimu, yaani ni kama vile "stive wozniak na stive jobs", steve jobs alitumia akili za stive wozniak na credit akajiapa yy mwenyewe

Aliyeweka Nyerere day kama public holiday alitumia vigezo gani ilihali si kweli kwamba Nyerere ndie mtu pekee aliepigania uhuru wa nchi hii

Ukiniambia nichague kati ya Nyerere na Kambona itakua ni Kambona always

UPDATE:
Watu wengi kwenye comments wanasema kwamba ujamaa ulituleta karibu, lakini ujamaa huo huo ndio uliotuletea umaskini, kwa hiyo logic yake ni kwamba mwalimu alichagua umaskini na umoja dhidi ya maendeleo ambayo hatuna uhakika kama yangetugawa, lakini kabla ya yote Kambona alimshauri kwamba kabla ya ku adopt ujamaa tuufanyie kwanza majaribio , tutengeneze vijiji vichache ambavyo vitaishi kijamaa ili tuone hii system itafanya kazi lakini mwalimu alikataa akaiingiza moja kwa moja bila kujua risks zake ni nini kitu ambacho kambona alishakiona


"Oscar Kambona was one of the best presidents Tanzania never had"
refence:

====

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!!

Christopher Makwaia

WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.10.jpeg

1. Usuli
Jioni ya Ijumaa ya tarehe 13.8.1925, huku mvua kubwà na radi kali zikirindima kijijini Kwambe, wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma, alizaliwa mtoto wa kiume akiwa buheri wa afya. Wazazi wa mtoto huyo, Rev. DAVID KAMBONA na Bi. MARIAM KAMBONA, wakampa mtoto huyo jina la OSCAR SATHIEL DAVID KAMBONA. Mvua na radi hiyo, kwa mujibu wa mila za kijijini hapo, "nyumbi hii, bombi hii", ilikuwa ni baraka na ishara kuwa mtoto huyo atakujakuwa wa kipekee.

2. Elimu Chini ya Mwembe
KAMBONA, tofauti na watoto wengine, hakusomea shuleni elimu ya awali bali alifundishwa na wazazi wake pamoja na mjomba wake ambao wote walikuwa walimu. Mafunzo hayo ya awali yalikuwa yakifanyika chini ya mwembe huku chai na mihogo vikiwa pembeni.

3. Elimu ya "Middle School"
Baadae KAMBONA alipelekwa shule ya Kati ya Mt. Barnabas, Liuli. Akiwa shuleni hapo, KAMBONA alikuwa kipanga na "aliwatimulia vumbi" wanafunzi wote kwa miaka yote alipokuwa shuleni hapo.

4. Alliance Sec. School
KAMBONA alifaulu vizuri mitihani yake na akachaguliwa kujiunga na "Alliance Sec. School", Idodomia ambayo baadae ikajaitwa Mazengo Sec. School. Almanusra KAMBONA asiendelee na masomo kwani baba yake hakuwa na uwezo wa kulipa £ 30 kwa mwaka. Uwezo wa KAMBONA "kutema yai" ndio uliomponya kwani alifanikiwa kumshawishi Askofu kumlipia ada hiyo baada ya kusali Sala ya Baba Yetu kwa Kiingereza!.

5. Tabora Boyz Sec. School
KAMBONA alisoma shule hii pamoja na J. Lusinde, E. Mzena, B. Ngwilulupi, A. Nsekela, A. Nyirenda na K. Chiume. Ni akiwa shuleni hapo ndipo kwa mara ya kwanza, KAMBONA alionana na NYERERE aliyekuwa akifundisha St. Marys, Tabora.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25281%2529.jpeg

6. Ualimu Alliance Sec. School
Baadae, KAMBONA alienda kufundisha shule hii na akakutana na J. Lusinde na K. Chiume na baadae akawa "Schoolmaster".

7. KAMBONA akutana na NYERERE tena
KAMBONA alikutana na NYERERE kwa mara ya 2 kwenye Mkutano wa taifa wa waalimu mwaka 1954.

8. KAMBONA Ajiunga TANU
Mwaka 1955, KAMBONA alijiunga na TANU iliyozaliwa tarehe 7.7.1954 na akaonesha bidii kubwa huku akifanya kazi kwa kujitolea kwani TANU haikuwa na fedha. Bidii yake ilipelekea kuwa Katibu Mkuu wa TANU.

9. KAMBONA Awaingiza TANU Watanganyika 100,000
KAMBONA alitembea nchi nzima kwa miezi 6 akionana na Machifu na wanavijiji na kufanikiwa kuingiza wanachama 10,000. Baadae akiendelea na harakati hizo na baada ya miezi 12 akawa ameingiza wanachama 100,000. Viongozi wenzake wa TANU walimpongeza sana kwani TANU ikawa inaenea kwa kasi sana.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25282%2529.jpeg

10. KAMBONA Afungua Akaunti ya Kwanza ya TANU
KAMBONA alikuwa na mawazo ya kimaendeleo kwani kutokana na michango ya wanachama aliweza kufungua akaunti ya kwanza ya TANU. Kwa hakika, hili lilikuwa ni jambo la kihistoria.

11. KAMBONA afuma "Governor's Scholarship" kusomea Sheria, UK
Mwaka 1957, KAMBONA alipata fursa ya kwenda UK kusomea LLB kwa miaka 3 na hivyo akaenda huko.

12. KAMBONA Awa Mtangazaji wa 1 wa Kiswahili BBC 1957
Tarehe 27.6.1957, KAMBONA aliweka historia kwa kutangaza Kiswahili BBC kwa mara ya 1 akisema-: "Hapa ni London, kwa mara ya kwanza BBC inawaletea habari kwa Kiswahili wananchi wa Afrika Mashariki. Asalaam Aleikhum".

13. KAMBONA awa Mwenyekiti wa TANU London
Kutokana na talanta yake kubwa ya uongozi, KAMBONA alichaguliwa kuwa Kiongozi wa wanafunzi chuoni na Mwenyekiti wa Tawi la TANU, London.

14. KAMBONA na NYERERE Washeachumba Chuoni London
Kati ya tarehe 26.6.1959 na 7.8.1959, NYERERE alikwenda UK kwa matayarisho ya uhuru wa Tanganyika na akalala chumba kimoja na KAMBONA ambaye walikuwa "wameshibana" sana. Katika "Press Conference" ya 1991 KAMBONA alisema- "TANU haikuwa na hela hivyo ili kubana matumizi, nikakaa na NYERERE room yangu chuoni na hii ilisaidia tuwe na muda mwingi wa majadiliano".

15. KAMBONA Amuoa MISS Tanganyika
Tarehe 19.11.1960, KAMBONA alimuoa Miss Tanganyika mrembo, Bi. FLORA MORIYO toka Kilimanjaro. Harusi hiyo ya kukata na shoka ilifanyika St. Paul Cathedral, London na kuhudhuriwa na wageni waalikwa 400. NYERERE alikuwa ndiye msimamizi aliyemsindikiza Bi. FLORA altareni. Ilikuwa ni harusi ya kwanza ya watu weusi kanisani hapo na ilitoka kwenye magazeti mbalimbali ya Ulaya.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.12.jpeg

16. KAMBONA Arejea Bongo
KAMBONA alirejea Bongo kuendelea na harakati za uhuru akihudumu kama Waziri wa Elimu na Katibu Mkuu wa TANU.

17. KAMBONA Awa Waziri wa 1 wa Mambo ya Nje
Katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Tanganyika, KAMBONA aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi.

18. KAMBONA Kipenzi cha 2 cha Wananchi baada ya NYERERE
KAMBONA alipendwa sana nchini kwani alikuwa msomi, mwanasiasa hodari, mtanashati na vijana wengi walimuiga staili yake ya nywele "KAMBONA Style". Kwa hakika, KAMBONA alipendwa sana.

19. KAMBONA- Kiongozi PEKEE Aliyewakabili Waasi, 1964
Usiku wa tarehe 19.1.1964, askari wa kambi ya Colito(Lugalo) waliasi wakidai marupurupu na nafasi za juu za vyeo kwa Waafrika. Rais NYERERE na Mh. RASHID MFAUME KAWAWA walitoroshwa na mlinzi wao, PETER BWIMBWO usiku wa manani hadi Kigamboni na kufichwa kwenye nyumbaya Mzee KIZWEZWE.

Mawaziri wote walibanisha makwao baada ya kupigiwa simu na Mh. J. LUSINDE, Waziri wa Mambo ya Ndani, kuhofia usalama wao. KAMBONA ndiye pekee aliyeingia "fronti" kwani si tu raia waliokuwa wakimpenda bali pia askari. Waasi walionekana kutulia baada ya mambo yao kuwekwa sawa lakini baada ya Rais NYERERE kuibukia Ikulu toka mafichoni baada ya siku 3, waasi "wakalianzisha" tena hivyo ikabidi maasi hayo yalizimwe kwa msaada wa Waingereza na baadae Wanaijeria.

20. KAMBONA Ashuhudia mchakato wa Muungano 1964
KAMBONA alikuwa ni mmoja wa mawaziri wachache sana waliokuwa wakijua mchakato wote wa muungano kwa undani na pia alishuhudia utiaji saini hati za muungano huko Zenji, tarehe 22.4.1964 kati ya Rais NYERERE na Rais wa Zanzibar, Mh. ABEID AMAN KARUME.

21. KAMBONA Atofautiana na NYERERE Mfumo wa Chama Kimoja
Baada ya ziara ya China 1965, NYERERE alivutiwa na "alikuwaameoza" kwa siasa za China na mfumo wao wa siasa hivyo akaunda Tume tarehe 28.1.1964 ili ipendekeze mfumo gani unaifaa nchi yetu. Tume hiyo ilikuwa chini ya Mh. KAWAWA ikapendekeza mfumo wa chama kimoja. KAMBONA, ambaye daima alikuwa hapepesi macho wala hayumbishwi, aliweka kunji na kutosaini ripoti hiyo na badala yake akatayarisha ripoti yake ya kutaka mfumo wa vyama vingi na NYERERE akahuzunishwa sana na msimamo huo wa KAMBONA.

Kipindi hiki NYERERE aliishamuondoa KAMBONA kwenye wizara zile nyeti.

22. NYERERE "Amchana" kiaina KAMBONA 77 ya 1966
Tarehe 7.7.1966, NYERERE, akihutubia Taifa katika sherehe za 77, NYERERE alitumia mafumbo "kumpa za uso" KAMBONA ambapo alisema viongozi wanaonekana kujipatia mali nyingi kiajabu hawafai hata kidogo.

23. KAMBONA Ajiuzulu u-Waziri na U-Katibu Mkuu TANU 1967
Tarehe 9.6.1967, KAMBONA alibwaga manyanga kwa kujiuzulu U-Katibu Mkuu wa TANU na Uwaziri wa Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini ambapo alitaja sababu za kiafya kuwa ndizo zilipelekea achukue uamuzi huo.

24. KAMBONA Atorokea Kenya, 1967 ki-James Bond !!
Kwakuwa KAMBONA alikuwa ni mtoto wa mjini, alitonywa kwamba kuna mpango wa kumkamata na kumsweka kizuizini.
Hivyo, usiku wa kuamkia tarehe 26.7.1967, KAMBONA, mkewe, watoto wake 2 na msaidizi wa kazi walifunga virago na ku-drive hadi Kenya kwa staili ya "James Bond"! Watu wengi walipigwa butwaa ni kwq vipi aliweza kutoroka bila kubambwa!.

Usiku wa siku hiyo jijini Nairobi, KAMBONA na familia yake walikwea "pipa" East African Airways Flight 720 kwenda "Kwa Mama, huku, huku nyuma ikadaiwa alitoroka na mamilioni ya fedha!.

25. NYERERE Aelezea "Kusepa" kwa KAMBONA
Siku chache baada ya KAMBONA "kula kona", NYERERE, akiongea na viongozi wa TANU Morogoro, alisema : "Itachukua muda mrefu kufahamu sababu za Bw. KAMBONA kujiuzulu, lakini jambo moja ni dhahiri; KAMBONA amenidanganya mimi, TANU, TZ na Afrika".

26. KAMBONA Ajitetea UK
Baada ya kusikia vijineno kwamba amesepa na mamilioni, tarehe 6.9.1967, KAMBONA alikanusha vikali na kuitaka serikali ya Tanzania iwasiliane na ya Kenya kupata uthibitisho kitu ambacho serikali ya TZ hakikufanyika.

27. OTTIN na MATTIYA KAMBONA "Wasukumiziwa Ndani",1967
Hawa wadogo zake KAMBONA walionja "joto ya jiwe" kwani walinyakwa usiku tarehe 30.12.1967 na kuwekwa kizuizini, Ukonga.
Familia zao zikasambaratika vibaya sana kufuatia kukamatwa kwao. OTTIN alikuwa ni "Journalist" na MATTIYA alikuwa mfanyakazi Wizara ya Kilimo. OTTIN alikuwa amemuoa raia wa Martinique na walikuwa na watoto 2 wadogo na MATTIYA alikuwa amemuoa Mgambia wakiwa na mtoto wa miezi 3 tu. Wanawake hao walifukuziliwa mbali na kurudishwa makwao pamoja na watoto wao!.

28. KAWAWA "Amchana" KAMBONA Bungeni, 1968
Jumanne ya tarehe 23.1.1968, KAWAWA, 2nd VP, alilitaarifu Bunge:
"Wote mnajua kwamba Bw. KAMBONA aliikimbia nchi mwaka jana, 1967. Kabla hajaondoka, tarehe 6.12.1966, TZS 500.000/= ziliingizwa kwenye akaunti yake toka benki moja ya Uingereza. Uchunguzi wa BOT toka KAMBONA atoroke umeonesha kuwa tangu Juni 1965 na Desemba 1966, KAMBONA aliingiza katika akaunti yake jijini Dsm TZS 896,800/=. Kambona pia alikuwa anamiliki majumba mengi (Nyumba Magomeni-Plot No. 21,39 31), (Kunduchi bichi-Plot No.28), (Msasani bichi -Plot No. 92), (Morogoro-Plot No. 89) ns (Songea-Plot No.21)".

29. KAMBONA Amchana NYERERE nchini Nigeria, 1968
Baada ya TZ kuitambua Biafra, serikali ya Rais YAKUB GOWON ilikasirishwa sana hivyo ilimwalika KAMBONA aichafue TZ . Kwahakika, "jipu likawa limepata mkunaji" Hivyo, KAMBONA akaenda na kutoa muadhara Lagos tarehe 14.6.1968 ambapo "alimchana" vilivyo Rais NYERERE na kumwita dikteta. KAMBONA akaonesha kukosa uzalendo kwa taifa lake pale alipozomoka, bila ushahidi, kwamba TZ imepeleka vifaa vya kijeshi Biafra badala ya Zimbabwe!.

30. TANU "Yamfyekelea mbali" KAMBONA
NEC ya TANU iliyokuwa ikiketi Tanga, tarehe 19.10.1968, ilimvua uanachama KAMBONA pamoja na wabunge wengine 8 "Vichwa-maji" waliohoji uhalali wa TANU kuwa juu ya Bunge. Wabunge hao ni W. Mwakitwange, M. Choga, S. Kibuga, J. Bakampenja, E. Anangisye, G. Kaneno na Dr. F. Masha.

31. NYERERE "Amchana" tena KAMBONA, 1969
Tarehe 12.1.1969 kwenye sherehe za Mapinduzi Znz, NYERERE "alimuwakia" KAMBONA na kusema- "KAMBONA ni mwizi na mhuni kisiasa.

32. KAMBONA Akejeliwa Mashuleni na Majeshini
Nyimbo nyingi za kumkejeli KAMBONA zilitungwa majeshini na mashuleni lakini zilizokuwa maarufu ni hizi 2:
1. KAOMBONA Kaolewa wapi....? Kwa Wazungu...Kisa nini?...Tamaa ya Mali!

2. Alimselema ...alija, akija KAMBONA chinja... chinjilia mbali..!!.

33. KAMBONA Adaiwa ni _"Mastermind"_wa Uhaini, 1969
Mwaka 1969, KAMBONA alidaiwa kuwa "Mastermind" wa uhaini. Mashitaka yalikuwa kwamba washtakiwa 7 wakishirikiana na KAMBONA kati ya Machi 1968 na Octoba 1969, walitaka kumuua Rais NYERERE na kuipindua serikali. Washtakiwa hao 7 ni (Bibi Titi Mohamed , Michael Kamaliza, Gray Mattaka, John na Eliya Chipaka, Capt A. Milinga na W. Chacha).

Kesi ilianza kurindima Jumatatu tarehe 6.6.1970 na ilisikilizwa na Jaji Mkuu Georges na iliendeshwa na AG Mark Bomani. Wanafunzi wa Sekondari Tambaza(F.V Arts akiwepo Othman Chande, Jaji Mkuu wa 7) walikuwa wakijongo vipindi kwenda kortin kushuhudia kesi hii iliyokuwa na mvuto wa aina yake.

Washtakiwa wote walitiwa hatiani kasoro A. Milinga na KAMBONA ambaye hakuwepo. M. Kamaliza na mwenzake walipigwa "mvua" 10 na wengine walifungwa maisha na Bibi Titi akapata msamaha 1972.

34. OTTIN MATTIYA Waachiwa 1978
Tarehe 5.2.1978, katika kusheherekea mwaka 1 wa kuzaliwa CCM, NYERERE, akitumia ibaracya 45 ya Katiba, aliwaachia huru OTTIN na MATTIYA pamoja na JOSEPH KASELABANTU( Mwasisi wa TANU).
OTTIN na MATTIYA, baada ya kugundua familia zao hazipo, wakaona Bongo hamna ishu nao wakaamua pia kusepa. Walivuka mpaka wa TZ na Kenya usiku Kininja kwani mpaka huo ulikuwa umefungwa kutokana na uhasama bainavya TZ na Kenya na wakaelekea UK.

35. NYERERE NA KAMBONA walikuwa majirani Msasani
Baada ya KAMBONA kuondoka nchini 1967, nyumba yake ikawa inakaliwa na Rais MILTON OBOTE kwa takribani miaka 10 baada ya kupinduliwa na Nduli IDD AMIN, 1971.

36. Vyama Vingi vyaanzishwa Bongo, KAMBONA ataka kurejea
Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, KAMBONA akiwa London alisema, ije mvua, lije jua, anarejea kwenye Taifa lake. Serikali ikamuonya kuwa asithubutu na akijifanya fyatu au kichwa-maji akatia pua yake tu Bongo, "hakuna rangi ataacha kuiona".

37. KAMBONA Aitunishia msuli serikali, Atinga Bongo
KAMBONA aliamua kuwa kama "Mbwai, mbwai tu" hivyo akaonesha "Shoo za kibabe" na kurejea nchini akisafiria nyaraka za Umoja wa Mataifa zilizotolewa na serikali ya UK. Aliporejea hakukamatwa na badala yake, tarehe 4.9.1992, serikali ilimpa miezi 3 aweke sawa uraia wake kwakuwa ni Mmalawi! Miezi hiyo iliisha tarehe 4.12.1992 na serikali "ikaufyata" kwani haikumfanya kitu chochote!.

38. KAMBONA aeleza sababu za kutoroka, 1967:
Baada ya kurejea nchini, KAMBONA alikata kiu ya wote waliotaka kujua kilichopelekea asepe "Kwa Mama" ni nini ambapo alitiririka:
"Mimi na NYERERE tumetoka mbali. Sisi ndio tuliokuwa Viongozi wakuu wa TANU; Yeye Mwenyekiti, mimi Katibu Mkuu. NYERERE aliporudi toka China 1965 alitaka kuleta sera za China na mfumo wa chama kimoja. Nikapingana nae.."

39. KAMBONA Aeleza alichokuwa akifanya UK
Wiki 2 baada ya kurejea nchini, KAMBONA alitiririka kitu alichokuwa akifanya nchini Uingereza kwa miaka 25 aliyoishi huko ambapo alisema- "I did business. I used to go to the Arab countries but this did not last. I then depended on income support from Britain. Every Tuesday You take your book to the Post office...

40. KAMBONA atishia "Kumwaga ugali na mboga" kuhusu NYERERE
Badala ya kushugulikia uraia, KAMBONA akaendeleza bifu lake na NYERERE ambapo alisema anataka kufanya mkutano mkubwa viwanja vya Jangwani ili aeleze ufisadi wa NYERERE. Mapadri na masheikh walimsihi sana lakini akashikilia msimamo wake.

41. KAMBONA Ambwelambwela Jangwani,1992
Tarehe 21.11.1992, viwanja vya Jangwani viliweka rekodi kutokana na umati mkubwa wa "wapenda ubuyu" uliojitokeza toka mida ya mchana kulisikia Jabali hilo litaeleza nini kuhusu Baba wa Taifa, Mwalimu NYERERERE.

KAMBONA aliwaboa sana 90% ya waliohudhuria kwani alidai, bila ushahidi, kuwa NYERERE, AMIR JAMAL na KAWAWA wameficha mamilioni ya fedha mabenki ya Ulaya. KAMBONA akaenda mbali na kudai NYERERE ni Mtutsi, KAWAWA na MKAPA ni watu wa Msumbiji na MALECELA ni Mcongoman!. Ikaonekana ni hekaya za Abunuwasi na hadithi za Esopo tu!.

42. NYERERE Amjibu KAMBONA
NYERERE, siku chache baadaye akiwa Msasani, aling'aka- "Mimi ni lofa. I dont have a single penny abroad, I can assure you. Kama RASHID na AMIR hawawekwi kundi la watu waaminifu duniani, labda neno uaminifu ni neno tu, halina maana. Hawa ni waaminifu sana. Pia, mimi sipendi kuhusishwa na mambo ya kijingajinga. Ni makosa kushindana na kundi la wapumbavu. Kambona alete ushahidi maana "any blessed fool could stand up there" na kusema chochote".

43. MAWAKILI wamchimba Mkwara-Mbuzi KAMBONA
Baada ya KAMBONA kutoa kashfa dhidi ya viongozi hao mashuhuri nchini, mawakili wa Viongozi hao walimpa siku 14 toka tarehe 8.12.1992 kuomba radhi au kutoa ushahidi.

KAMBONA aliwajibu kuwa _"Mtu mzima hatishiwi nyau"_na akachekesha watu pale alipodai _"Nondo" zake kuhusu "bank accounts" za viongozi hao amezisahau UK!.

44. KAMBONA Aunda TADEA
KAMBONA aliunda chama cha TADEA ambacho hakikuleta upinzani wowote wa maana.

45. KAMBONA afariki London, 1997
KAMBONA alifariki jijini London mwaka 1997 na mwili wake kuletwa nchini na kupokelewa na ndugu zake na kiongozi wa serikali, Mh. J.M. KIKWETE, Waziri wa Mambo ya Nje. Rafiki yake NYERERE hawakuwahi kuonana toka atoroke mwaka 1967 na wala hakwenda kwenye mazishi yake.

46. RAIS KIKWETE Akutana na Mke wa KAMBONA, 2007
Tarehe 28.6.2007 katika hotel ya Kilimanjaro Kempisk, Rais wa awamu ya nne, Mh. JK alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 50 ya BBC KISWAHILI. Mh. JK, akiwa na mcheshi na mwenye bashasha kama kawaida yake, alikutana na kusalimiana na Bi. FLORA KAMBONA ambaye alikuwa mgeni mahsusi kwani mmewe, KAMBONA ndiye aliyekuwa Mtangazaji wa 1 wa BBC Kiswahili, 1957.

46. MWISHO:
Huyu ndiye OSCAR SATIEL DAVID KAMBONA aliyekuwa chanda na pete na Mwalimu NYERERE lakini mwisho wakawa maadui wasio na mfanowe!.

Tafakuri Tunduizi:
ATIKALI HII YA KUKATA NA SHOKA ina Tafakuri Tunduizi 100!!!

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!! - MICHUZI BLOG (issamichuzi.blogspot.com)

Oscar Kambona - Wikipedia

Msingi wa yanayoendelea leo Tanzania kiuchumi na kisiasa mwanzo wake ni jinsi Nyerere alivyomfanyia Kambona. Kambona alikuwa kiongozi mwenye upeo mkubwa sana na aliona mbali sana kuwa Sera za Nyerere sizingeweza kuzalisha Tanzania waliyokuwa wanaipigania dhidi ya Mkoloni.

Kiburi cha Nyerere na watu wake ndo mwanzo wa Tanzania yetu kuanguka vibaya kiuchumi na kuwa na mfumo mbovu zaidi wa utawala unaotengeneza watu wanafiki wanaomzunguka mtawala mkuu ambao kazi yao sio kumwambia mtawala mkuu ukweli bali kumlisha maneno ya uongo ili matumbo yao yaendelee kushiba.

Kambona aliona mbali sana. Alipinga kabisa uanzishwaji wa Azimio la Arusha na akajiuzuru nafasi zake zote. Waliokuwa wanampinga na kumuungua mkono Nyerere ndo walioshuhudia nchi ilivyoanguka vibaya kiuchumi kutokana na sera mbovu za ujamaa, na Nyerere alipoondoka tu walizitupilia mbali sera za ujamaa na kuanzisha soko huria.

Kama Tanzania Leo tusingekuwa na ujamaa Leo Tanzania ingeweza kuwa nchi yenye uchumi mkubwa zaidi Africa maana kwa miaka ya 60 Tanzania ilikuwa na wakulima vijijini waliokuwa wakilima kwa tractors. Sasa hali ingeendelea kuwa vile hadi leo tungekuwa wapi???

Ukweli lazima usemwe, ipo siku lazima tutamkumbuka Kambona kama shujaa wa Taifa hili na ukweli utasemwa kweli kuwa Nyerere ndo chanzo cha hii Tanzania mbovu tuliyokuwa nayo leo.
 
Eti Tanzania ilikuwa moja, unamjua Thomas Marealle wewe?

Mifumo hiyo ya ulinzi ina misingi ya ujamaa (nyumba kumi kumi).

Nimeongelea kusini tena kipindi cha maji maji mbona umemleta Mangi wa kaskazi tena kipindi cha harakati za uhuru 1950s??

Tukirudi kwenye mada, hata habari za Thomas nyingi ni propaganda za kijima ili ionekane tupo sehemu salama huyu hana mbadala, hawezi kuzibika nafasi yake, yule na yule hawafai. Upuuzi fulani wakirusi enzi ya Stalin
 
Msingi wa yanayoendelea leo Tanzania kiuchumi na kisiasa mwanzo wake ni jinsi Nyerere alivyomfanyia Kambona. Kambona alikuwa kiongozi mwenye upeo mkubwa sana na aliona mbali sana kuwa Sera za Nyerere sizingeweza kuzalisha Tanzania waliyokuwa wanaipigania dhidi ya Mkoloni.

Kiburi cha Nyerere na watu wake ndo mwanzo wa Tanzania yetu kuanguka vibaya kiuchumi na kuwa na mfumo mbovu zaidi wa utawala unaotengeneza watu wanafiki wanaomzunguka mtawala mkuu ambao kazi yao sio kumwambia mtawala mkuu ukweli bali kumlisha maneno ya uongo ili matumbo yao yaendelee kushiba.

Kambona aliona mbali sana. Alipinga kabisa uanzishwaji wa Azimio la Arusha na akajiuzuru nafasi zake zote. Waliokuwa wanampinga na kumuungua mkono Nyerere ndo walioshuhudia nchi ilivyoanguka vibaya kiuchumi kutokana na sera mbovu za ujamaa, na Nyerere alipoondoka tu walizitupilia mbali sera za ujamaa na kuanzisha soko huria.

Kama Tanzania Leo tusingekuwa na ujamaa Leo Tanzania ingeweza kuwa nchi yenye uchumi mkubwa zaidi Africa maana kwa miaka ya 60 Tanzania ilikuwa na wakulima vijijini waliokuwa wakilima kwa tractors. Sasa hali ingeendelea kuwa vile hadi leo tungekuwa wapi???

Ukweli lazima usemwe, ipo siku lazima tutamkumbuka Kambona kama shujaa wa Taifa hili na ukweli utasemwa kweli kuwa Nyerere ndo chanzo cha hii Tanzania mbovu tuliyokuwa nayo leo.
nyerere aliingiza mambo binafsi kwenye maslahi ya taifa
 
Ni kweli mwl hakufanya kazi peke yake lazima wasaidizi kama hawa wawepo.. hii ni kawaida hata katika makampuni makubwa na taasisi zote zenye mafanikio rekodi huwekwa kwa maCEO licha ya kwamba hawa hufanya kazi kwa ushauri wa watu wachache nyuma yao. Leo hii microsoft imemfanya BillGate atambulike duniani kote ila tafuta historia yake utajua waliokuwa nyuma yake... Hata mpirani historia itamkumbuka sana Leonel Messi ila wapishi wake wakuu akina Iniesta, Xavi hawatakumbukwa kwa muda mrefu... Ndivyo ilivyo
 
nchi nyingi kua na changamoto nyingi kuliko TZ haimanishi tupo nafasi nzuri, Tungeweza kufanya vizuri zaidi ya hapa lakini tulifeli kwasababu ya mtu mmoja
Miaka 35 sasa tangu aachie ngazi, wote waliofuata nn wamekifanya cha maana... kitu kikubwa ambacho nyerere alitujengea na ni cha kujivunia ni amani tuliyonayo..... ukitembelea nchi nyingi za kiafrika utagundua mipasuko mikubwa iliyomo miongoni mwa raia wake.. nenda cameroon,nigeria, ethiopia, sudan, rwanda, SA hata tu hapo kenya utagundua hili....
 
Nimeongelea kusini tena kipindi cha maji maji mbona umemleta Mangi wa kaskazi tena kipindi cha harakati za uhuru 1950s??
Umoja huo wa kusini haukuwa wa kitanzania bali wa vikundi vidogo vidogo. Na hii ndiyo sababu Mjerumani aliweza kututawala, alipiga hapa leo, kesho akapiga pale, kidogo kidogo akaichukua nchi. Na hii ndiyo sababu ya Nyerere kuondoa uchifu ili kubadilisha mfumo ulioshindwa na kuweka mfumo madhubuti ambao hauingiliki kirahisi.

Uchifu ulikuwa unaangalia himaya ndogo sana ambayo kwa sasa ni sawa na eneo la kata au wilaya mmoja tuu. Nadharia ya nchi ya mamilioni ya watu hatukuwanayo waafrika. Nyerere alifahamu hilo na kuhakikisha anajenga utaifa ili nchi isije ingilika kirahisi kama walivyofanya wajerumani.
 
Umoja huo wa kusini haukuwa wa kitanzania bali wa vikundi vidogo vidogo. Na hii ndiyo sababu Mjerumani aliweza kututawala, alipiga hapa leo, kesho akapiga pale, kidogo kidogo akaichukua nchi. Na hii ndiyo sababu ya Nyerere kuondoa uchifu ili kubadilisha mfumo ulioshindwa na kuweka mfumo madhubuti ambao hauingiliki kirahisi.

Uchifu ulikuwa unaangalia himaya ndogo sana ambayo kwa sasa ni sawa na eneo la kata au wilaya mmoja tuu. Nadharia ya nchi ya mamilioni ya watu hatukuwanayo waafrika. Nyerere alifahamu hilo na kuhakikisha anajenga utaifa ili nchi isije ingilika kirahisi kama walivyofanya wajerumani.

Mkuu hivi unaifahamu vyema historia ya vita vya Maji Maji?

Kwa Tanzania hivi ndio vita vya kwanza vyenye mwelekeo wa kitaifa, na havikupiganwa ndani ya himaya ndogo kama unavyodhani vilipiganwa mikoa zaidi ya minne kuanzia mikoa ya kusini hadi baadhi ya sehemu za mkoa wa Pwani.

Kitendo cha watawala wa enzi zile kuungana ili kumtoa mkoloni ilikuwa ni kielelezo cha utaifa kama haujui hilo mkuu.

Soma historia vizuri achana na historia ya sekondari ya kuunga unga.

Mwl. Nyerere alifuta uchifu ili aweze kutawala atakavyo yeye.

Uganda wanashindwa na Uchifu kwa sababu ya rushwa na viongozi corrupt walafi wa madaraka, hii haimaanishi na sisi tungeshindwa na mfumo wetu ule
 
shukran sana umetufumbua Macho japo nawewe haupo deep sana yan kama umehadithiwa au umeskia mahala then ukaja kutuambia.

please anayefahamu vizuri historia ya huyu mtu (Kambona) atiririke, tujue alizaliwa wapi, amesoma wapi, alikua na nyadhifa zipi , kafa mwaka gani. Pia atueleze tz ya sasa kipi kimefanyika ambacho Kambona alikiona na Nyerere alikuwa hakiamini

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Naona vitu vingi ulivyouliza vipo katika uzi hapo juu
 
Nitafarijika sana kama siku moja mzee Mohamed Said ataandika makala maalumu ya kumuelezea Kambona kama vile anavyofanya katika kuwaandikia makala wazee wake wa Kariakoo walioshiriki katika harakati za kisiasa kabla na baada ya uhuru.


Najua uwezo huo unao ila hajajisikia tu kufanya hivyo. Labda kwa kuwa Kambona hakuwa mwenzetu kiimani.
Hujazuiwa kumuandika Kambona na historia yake badala ya MS na wale wazee wa mjini waliowatoa tongotongo washamba.
 
Back
Top Bottom