Tanzania ya viwanda yageuka kuwa Tanzania ya vituo vya mafuta

Aisee ni kweli nimeona Chalinze dar kuna vitua vipya vinajengwa vingi sana ni kama walisubiriana kuja kuvijenga
Hivi vituo vitajifunga vyenyewe baada ya ujenzi wa highway (Dar-Moro).
Magari mengi yatatumia hiyo bara bara ambayo itakuwa na vituo vyake maalum vya mafuta).
 
Bila shaka sasa Tanzania mpya iliyokuwa inameremeta kwa ujenzi wa viwanda kila kona ya nchi, sasa imegeuka kuwa Tanzania ya ujenzi wa vituo vya mafuta kiholela na kila sehemu!

Sheria inataka ujenzi wa kituo cha mafuta uwe mita 500 kutoka kimoja hadi kingine lakini sheria hii haifuatwi tena. Kuanzia mwaka 2021 vituo vya mafuta vinaota kama uyoga kwenye nchi yetu. Swali la kujiuliza kimetokea nini?

Mkoa wa Pwani ulikuwa unaongoza kwa ujenzi wa viwanda vingi sana lakini sasa hivi wakifanya utafiti upya watakuta unaongoza kwa ujenzi holela wa vituo vya mafuta.
VITUO vya MAFUTA ni ENEO MUHIMU la kuficha FEDHA ZA WIZI MKUU watumishi wa UMMA wameficha fedha za wizi huko kupitia Wafanyabiashara

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Mkipata kazi kwenye hivyo vituo hamuongei wakipata wenzenu mnakuja kubwabwaja mitandaoni.Tunahitaji wawekezaji zaidi kwenye sekta ya mafuta ili kurahisisha upatikanaji wa mafuta.
 
Viwanda vinaajiri watu wengi na kuifanya nchi kujitegemea kwa bidhaa na zingine kuuza nje ya nchi

Kituo cha mafuta kinaajiri watu wasiozidi 10 na kinaifanya nchi kuwa tegemezi milele
 
Bila shaka sasa Tanzania mpya iliyokuwa inameremeta kwa ujenzi wa viwanda kila kona ya nchi, sasa imegeuka kuwa Tanzania ya ujenzi wa vituo vya mafuta kiholela na kila sehemu!

Sheria inataka ujenzi wa kituo cha mafuta uwe mita 500 kutoka kimoja hadi kingine lakini sheria hii haifuatwi tena. Kuanzia mwaka 2021 vituo vya mafuta vinaota kama uyoga kwenye nchi yetu. Swali la kujiuliza kimetokea nini?

Mkoa wa Pwani ulikuwa unaongoza kwa ujenzi wa viwanda vingi sana lakini sasa hivi wakifanya utafiti upya watakuta unaongoza kwa ujenzi holela wa vituo vya mafuta.
Barabara ya Tandale Uzuri vituo vipo baada ya mita 100.
 
Back
Top Bottom