Naanza kwa kutoa hongera, maana mkifanikiwa kuna baadhi yetu tunaovuka mipaka ya EAC tutanufaika kiaina. Lakini naomba makada wa Tanzania watumie muda mwingi kuelimisha Watanzania umuhimu wa reli hii kiuchumi badala ya wanachokifanya sasa kufungua nyuzi nyingi wakilinganisha gharama za ujenzi wa reli ya Kenya. Nina uhakika Watanzania wengi wanahitaji kujua watakavyonufaika zaidi ya kujua gharama baina ya Kenya na Tanzania.
Kufikia hapo bado hamjafanya hata design, hamjabaini idadi ya madaraja, na kama kutakua na kupitia kwenye mahandaki, vituo vyenyewe hamjajadili vitakua vipi na vyenye design ipi, treni na mabehewa bado hamjaonyesha, na tafiti nyingine nyingi sana ambazo zinaambatana na ujenzi wa reli. Sasa leo mumejazana kwenye mitandao mnajadili kulinganisha na Kenya shilingi kwa shilingi.
Halafu wengine mnadanganya eti treni yenu itasafiri kwa kasi ya 160km/h au 120km/h ikiwa na mabehewa 100, mnafaa kuelewa trains and ratio of Wagons/Locomotives, ingia kwenye Google kabla hujaanza uongo.