Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Balozi Omar amesema hayo (12.10.2026) alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Ndiame Diop, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia inayofanyika Jijini Bangkok nchini Thailand.
Aidha, amesema kuwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali na matumizi vimeenda vizuri, huku mfumuko wa bei ukiwa ndani ya viwango vilivyokubalika vya asilimia 3 hadi 5.
Kuhusu ushirikiano na Benki ya Dunia, Mhe. Balozi Omar amesema taasisi hiyo inafadhili miradi 33 yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 8.8 katika sekta za viwanda, elimu, afya, kilimo na mifumo ya hifadhi ya jamii kama TASAF.
“Tunashirikiana kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati. Miradi hiyo ya kipaumbele ni pamoja na uendelezaji wa Bandari ya Dar es Salaam, ujenzi wa reli ya Kati (MGR) na Reli ya Kisasa (SGR), pamoja na miradi ya nishati inayolenga kuunganisha gridi ya Taifa na nchi jirani ya Zambia.
Mhe. Balozi Omar amesisitiza kuwa uhusiano na taasisi hizo ni mzuri, akitolea mfano wa ziara za viongozi wa ngazi ya juu wa Benki ya Dunia na IMF nchini Tanzania, ambao wameonyesha kuridhishwa na hatua za maendeleo zinazopigwa na Tanzania.
Kwa upande wa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Ndiame Diop, aliipongeza Tanzania kwa hatua kubwa iliyofikia kiuchumi na kimaendeleo na kuahidi kuwa Banki yake itaenndelea kuwa mshirika wake muhimu kwa kufadhili miradi mbalimbali ya kimkakati ya Serikali na kikanda.
Alitaja miradi ya nishati, elimu, miundombinu ya reli hususan ushiroba wa kati, kusaidia kaya masikini kupitia TASAF, uendelezauji rasilimali watu pamoja na miradi ya kikanda, kwamba itaendelea kupewa fedha na Banki hiyo kulingana na mahitaji ya nchi.