Tanzania yafundisha wanajeshi wa DRC TMA - Monduli

Tanzania yafundisha wanajeshi wa DRC TMA - Monduli

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Vijana wa kikongo DRC wapewa mafunzo ya kijeshi TMA - Monduli kwaajili ya kuilinda nchi yao wenyewe.Wiki mbili zilizopita mji wa Arusha umeshuhudia vijana toka taifa kubwa barani Afrika wakifurika katika vitongoji mbali mbali jijini Arusha siku za jumamosi na jumapili.Kwa kawaida siku za weekend wanafunzi wanaochukua mafunzo ya uofisa wa jeshi wanapewa ruhusa ya kutakasa macho jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni wanarejea chuoni Monduli.Ni rahisi sana kuwatambua wanafunzi wa TMA hasa uvaaji unaoambata na suti na tai pia upenda kutembea kwa vikundi vikundi.

Tanzania ambayo iliongoza kikosi cha UN dhidi ya kikundi cha M23 kinachoungwa mkono na Rwanda na Uganda imebaini pasipo shaka yoyote mkakati wa kuilinda Congo wa muda mrefu dhidi ya serekali ya Kagame na Museveni ni lazima uongozwe na waCongo wenyewe.

Nakala jMali Ruzibiza Happy Feet Bongolander MGOSI132 JokaKuu murutongore Koba kabavamwo Remote TZ kwanza mpiga domo Ndahani
 
Last edited by a moderator:
apigwe nduli kagame..........apigwe,wasije wakatoroka wakafungua bendi au saluni,JWTZ WATENGENEZENI WAWE IMARA WAINGIE MPAKA KIGALI
 
Katika hili naunga mkono hoja,na waletwe wengi tu ili kumsambaratisha kagame na museveni.
 
Sio wakongo tu hadi wamarekani wapo TMA

Ni utaratibu wa kawaida wa majeshi kushirikiana kimataifa
 
dawa za maadui wa kongo ni kuungana na tz na kuwa na serikali tatu, ya muungano na 2 za nchi husika, hivyo part of our army ina base huko nao wana leta kwetu, hapo sisimizi hawezi pita, wizara za muungano zitakuwa 1 ulinzi na usalama, zingine kama nchii husika zitakavyo ona.
 
dawa za maadui wa kongo ni kuungana na tz na kuwa na serikali tatu, ya muungano na 2 za nchi husika, hivyo part of our army ina base huko nao wana leta kwetu, hapo sisimizi hawezi pita, wizara za muungano zitakuwa 1 ulinzi na usalama, zingine kama nchii husika zitakavyo ona.
brilliant idea
 
Ngongo ni kweli usemavyo na hata leo jumamosi utaowaona wengi sana wakitalii ndani ya jiji na ni katika makundi.

Na utawaona katika usafiri wa Ashok Leyland Bus kama tatu hv wakiwa ktk mavazi ya suti safi na tai kama ulivyokwisha kusema Mkubwa Ngongo
 
Last edited by a moderator:
wanafundisha hadi wale wapasua tofali kwa vichwa?wakitugeuka ndahani itapidi wapigane vichwa kama kondoo ili vipasuane.
 
Acha wakapigwe circumcision tu wakalinde kwao! !!!!!!
Hapo sasa wamefika!!!!!!
 
Wapo toka mwaja jana kuanzia Mwezi wa kumi kama sikosei
 
Hongera sana Tanzania. Tumekuwa ni kitovu cha ukombozi Barani Afrika
 
Ila tujifunze.kwani wale wa kabila senior pia tulifundisha na waasi.sijui this time km wamehakikisha gharma halali haitrain na waasi,ambao wengi watajituma kuliko halali ili wakirudi kule wao wakawashinde wazalendo.
 
wawe wanatulipa basi. Tusirudie makosa yale ya miaka ya nyuma ya kutoa misaada ya kijeshi burebure halafu uchumi wetu unadorora wa wenzetu unapaa. Tufanye hayo profitably kama vile USA anafanya!
 
apigwe nduli kagame..........apigwe,wasije wakatoroka wakafungua bendi au saluni,JWTZ WATENGENEZENI WAWE IMARA WAINGIE MPAKA KIGALI

kagame aliwahi kupigana na nchi 8 iweje congo ikiwa moja wapo na akawashinda just a year after capturing kigali...iweje leo hii kuweni na akili....RWANDA bana ni nchi ndogo ila achana nayo kabisa zungumzeni mambo mengine
 
Mamluki wote baada ya kushughulikiwa na zimbabwe na namibia na angola hawapo tena kongo, tanzania imewakomboa wote hao, hata kongo kipindi hicho mliomba msaada uganda KIJANA USICHEZEE MOTO
 
Itakuwa ni busara sana kuwa na Taifa la Congo lenye amani. Kibiashara Tanzania itaneemeka mno na Congo kuliko Uganda na Rwanda. Kwa mtazamo huo, na kwa malengo ya muda mrefu, ni vema tukaingiza mkono wetu wa kuhakikisha Congo inakuwa na amani mapema.
 
Back
Top Bottom