Tanzania yagoma kupiga kura ya kuunga mkono Mipaka ya nchi ya Ukraine(Territorial Integrity) huko UN

Tanzania yagoma kupiga kura ya kuunga mkono Mipaka ya nchi ya Ukraine(Territorial Integrity) huko UN

Kwani Zanzibar itakapoamua kujitenga na bara nakutaka kujiunga na Kenya wataonekana wamewakosea bara? Kwa vipi kwani Zanzibar si nchi huru?.Urusi waharibu miundombinu ya ukrein na kuua raia halafu Manashabikia ?
Na kwa kua huyo nyoka anaelelea kushindwa macho yake yanatazama silaha za nuklia,Ulimwengu unaelekea wapi?
uhuru una mipaka mkuu, kama wadhani uhuru hauna mipaka bado una safari ndefu

kawashawishi wajiunge kenya ndo utajua uhuru unao zungumza ni wa kwenye makaratasi tu
 
Kwa wanaojua ukweli kwanini russia anaendesha opereshen zake ukrane hawawezi kujihusisha na mambo hata ya kupiga kura.
Tanzania ina wazee wenye hekima, busara na ubobezi katika kuitambua haki na usawa. Hata kama wananchi wake wengi wamo kwenye mkumbo kwa sabab ni ill_informed na unknowledgeable!
......tushirikiane kupinga unilateralism.
 
Bora hata Resolution ingehusu Urusi kuvamia Ukraine hapo tungeweza kujibaraguza na kuabstain LAKINI kura inahusu kutambua na kuheshimu mipaka ya Ukraine ambaye ni mwanachama mwenzetu wa UN , ambaye kasaini articles za kila nchi kuheshimu mipaka ya nchi nyingine kama sisi tulivyosaini, tunashindwaje kulinda hii principle kwa Wivu mkubwa?

Tanzania chini ya serikali ya CCM haiwezi kwenda kinyume na utashi wa Russia. Ifahamike Russia na China ndio nchi zisizohoji chaguzi za kihuni, na CCM wanajua hilo ndio kimbilio lao iwapo itachezea uchaguzi na nchi za magharibi kutaka kuchukua hatua.
 
Mrusi wa Manzese anajua kila kitu kuhusu uhalali wa Urusi kushambulia raia wa Ukraine na kujimegea ardhi ya Ukraine. Utasikia anakupigia kelele NAM (ya Cold war Era), NATO (fear from the cold war era), na Minski Agreement (iliyopangwa na Urusi) lakini hatambui Budapest Memorandum (iliyohusisha Urusi, Ukraine, USA na UK kuhusu usalama wa Ukraine) na Article 2(4) ya UN kuhusu kuhesimu mipaka ya nchi nyingine.

Yaani Mrusi wa manzese anajua sana uhalali wa vita hiyo kuliko hata warusi wa ndani ya Urusi wakiwemo hata wale waliokuwa mawaziri na mabalozi kwenye serikali hiyo hiyo ya urusi. Manzese kuna warusi wanaoijua urusi vizuri sana
ndio sisi ni warusi wa manzese nyie endeeleeni na kibabu chenu. hii vita mtapigwa kama ngoma. ngumi ya putin inajikunja inaitwa ndoige! uraaa uraaa
 
Back
Top Bottom