Tanzania yagundua Gas yenye futi za ujazo bilioni 223 katika Kisima cha Kasa Mkoa Mtwara

Tanzania yagundua Gas yenye futi za ujazo bilioni 223 katika Kisima cha Kasa Mkoa Mtwara

Smartkahn

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2020
Posts
1,028
Reaction score
1,790
Waziri wa Nishati Dkt. Juma Homera ametangaza rasmi ugunduzi mpya wa Gesi Asilia yenye futi za ujazo bilioni 223 katika Kisima cha Kasa kilichopo Katika Kitalu cha Mnazi Bay Mkoa Mtwara.

Dkt. Homera amefanya uzinduzi huo leo Oktoba,27, 2026 na kusema kuwa hilo ni tukio kubwa katika maendeleo ya Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi nchini na kutoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono, miongozo na jitihada zake za kuhakikisha Nchi inaendelea kupiga hatua katika Sekta ya Nishati.

Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwemo gesi asilia iliyogunduliwa mwaka 1974, baadaye kuendelezwa na kuanza uzalishaji wake mwaka 2004, chango wa gesi asilia umekuwa mkubwa katika kuzalisha umeme na kutumika kama nishati viwandani, majumbani na kwenye magari.

Soma Pia: Rais Samia: Nchi zetu mbili zimegundua akiba kubwa ya gesi baharini, Namibia ina futi za ujazo trilioni 8.7 Tanzania futi za ujazo trilioni 57.5

Serikali imefanikisha haya kupitia Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na wawekezaji binafsi wa Makampuni ya Kimataifa ya Mafuta na Gesi (IOCs).

Screenshot 2026-10-27 233144.png
 
Hii ni mara ya ngapi wanagundua gas ?

Na ni kwa nini inagundulika membezoni mwa bahari TU ? May be kuongeza gharama za uendeshaji
 
Back
Top Bottom