Tanzania yajiondoa kwenye Mkakati wa Uwazi, Ushiriki na Uwajibikaji(OGP)

Tanzania yajiondoa kwenye Mkakati wa Uwazi, Ushiriki na Uwajibikaji(OGP)

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Serikali ya Tanzania inadaiwa kujitoa kwa muda kwenye Mkakati wa Uwazi, Ushiriki na Uwajibikaji yaani Open Goverment Partnership(OGP). Inadaiwa Serikali imeamua kujikita kwenye "kutumbua majipu" kwanza kabla ya kujikita kwenye uwazi.

OGP ilianzishwa mwaka 2011 na ilianza na Serikali 8 hadi 70 na Tanzania ilijiunga 2011 na kutekeleza mipango kazi ya kitaifa 3 hadi sasa (3 National Action Plans).

Ahadi 7 zilizokuwa kwenye Mpango Kazi wa 3 wa Kitaifa wa OGP ni

i) Kutungwa kwa Sheria ya Upatikanaji wa Habari(Access to Information Act)

ii) Bajeti kuwa wazi(Open Budgets)

iii) Taarifa mbalimbali za Serikali kuwa wazi(Open Data)

iv) Uwazi wa masuala ya ardhi ikiwemo taarifa za umiliki wa Ardhi nchi nzima kuweza kupatikana mtandaoni(Land Transparency)

v) Uwazi katika Sekta ya Madini

Ahadi za Nyongeza
(vi) Uwazi katika Sekta ya Afya kwa ujumla(Medical and Health Service Transparency)

(vii) Kuwepo kwa mifumo ya utendaji kazi wa Serikali iliyo wazi kabisa (Performance Management Systems)


Anaandika Mbunge wa Kigoma Ujiji, Zitto Kabwe:

Nimeshangazwa na uamuzi wa Serikali kujiondoa OGP. Hivyo nimeamua kuwasilisha swali Bungeni kutaka maelezo ya Serikali, inayojipambanua kwa kupambana dhidi 11 ufisadi, kujiondoa kwenye jukwaa la Kimataifa linalopigania Serikali kuendeshwa kwa uwazi na uwajibikaji.

Uwazi ( Transparency/Openness ) ni silaha muhimu sana katika vita dhidi ya rushwa na katika kuwezesha ufanisi Serikalini.

Licha ya kwamba Tanzania ilikuwa haitimizi ahadi zote kwenye Action Plans, lakini kulikuwa na msingi kwamba Nchi yetu inaamini katika Uwazi na Uwajibikaji. Uamuzi wa Serikali kujiondoa OGP unarudisha nchi yetu nyuma. Ni uamuzi ambao haukufikiriwa Sawa sawa.

Kujua Zaidi kuhusu OGP:

Msafara wa Kikwete Brazil Kwenye Mkutano wa OGP

OGP announces 15 subnational govt that will be part of a pilot program, Kigoma Tanzania one of them

Mpango Kazi wa Kitaifa wa kuendesha shughuli za Serikali kwa Uwazi Awamu ya Tatu (OGP NAP III)

======

Serikali imejitoa katika Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership-OGP) hatua ambayo inazua wasiwasi kuhusu utekelezaji wa sera ya uwazi iliyoasisiwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Hatua hiyo ya kujitoa kwa Tanzania ilitarajiwa kutangazwa wakati wowote na Kamati ya Uongozi ya mpango huo inayokutana katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea New York, Marekani.

Tanzania ilijiunga na mpango huo mwaka 2011 na hivyo kuwa nchi ya pili barani Afrika ikitanguliwa na Afrika Kusini ambayo ilikuwa ya kwanza kusaini makubaliano hayo yanayotaka nchi kuondokana na kasumba ya kuendesha mambo kwa usiri kati yake na wananchi.

Zaidi ya nchi 70 duniani zimesaini mpango huo unaohimiza dhana ya uwazi na ukweli. Rais mstaafu Kikwete alikuwa mstari wa mbele kuunga mkono mpango huo na alifanikisha mkutano wake uliofanyika kwa mara ya kwanza nchini 2015 ikiwa miezi michache kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu.

Wakuu wa mpango huo wanakutana New York wakijadiliana mambo mbalimbali ikiwamo ajenda inayoangazia kuongezeka kwa hali ya kutoaminiana kati ya Serikali na wafanyabiashara. Pia, wanaangalia njia zinazopaswa kuchukuliwa ili pande hizo ziweze kurejea katika hali yake ya kawaida.

Hata hivyo, Serikali ya Tanzania bado haijaweka hadharani juu ya hatua yake iliyochukua ya kujitoa kwenye mpango huo. Pia, haikuweza kufahamika mara moja kama maofisa wake walioko mjini New York watapeleka ujumbe uliochukuliwa nyumbani na Serikali.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Augustine Mahiga yuko New York akimwakilisha Rais John Magufuli mkutano wa Umoja wa Mataifa.

Alipoulizwa kuhusiana na hatua hiyo iliyochukuliwa na Serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki alikataa kueleza lolote lakini akasema kuwa Serikali itatoa ufafanuzi wake muda utakapowadia.

“Nisikilize, sisi (Serikali) tutalieleza hilo tutakapoona inafaa,” alisema Waziri Kairuki ambaye hakukanusha wala kukiri lolote.

Lakini, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Aziz Mlima alikiri kuhusu Tanzania kujiondoa katika mpango huo.

“ Ndiyo ni kweli lakini ni kwa muda tu kwa sababu Serikali inataka kuutathmini mpango huo kama unaendana na masilahi ya Taifa,” alisema.

“ Kuna mambo tunahitaji kwanza kuyatekeleza kabla ya kutekeleza mpango huu,” alisema. Hata hivyo, vyanzo vya kuaminika vimelidokeza gazeti hili kuwa utawala wa Rais Magufuli unapenda kujikita zaidi katika utekelezaji wa Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora barani Afrika (APRM).

Kabla ya kujitoa katika mpango huo wa OGP, Tanzania ilikuwa tayari imepitia hatua mbili za utekelezaji na sasa ilikuwa ikijiandaa kutekeleza mpango mkakati wa tatu uliokuwa uanze 2016/17-2017/18.

Katika mipango hiyo, Tanzania ilikuwa imeainisha maeneo saba ya kuweka mkazo ikiwamo Sheria ya Kupata Habari, Bajeti ya Uwazi, Uwazi katika ardhi na madini.

Akizungumzia mpango huo mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Faraja Kristomus alisema wengi waliitazama OGP kama mpango wa nje zaidi na kukosa uungwaji mkono katika taasisi za kiserikali.

Katika makala zake zilizochapishwa na gazeti la Citizen, Kristomus ameandika kuwa wizara iliutazama mpango huo kama chombo chenye urasimu na haukusaidia kukaribisha mageuzi.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema hatua ya Tanzania kujiondoa katika mpango huo ni ishara nyingine ya kuanguka kwa demokrasia na uwazi serikalini. “Kitendo cha kujiondoa ni kuiambia dunia kuwa hatuko tayari kwa uwazi,” alisema.

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alisema uwazi kwa serikali ilikuwa silaha tosha ya kukabiliana na rushwa.

“Tanzania ilikuwa haitekelezi kikamilifu mahitaji yote ya OGP. Lakini naamini kuwa angalau ilikuwa njia sahihi ya mwelekeo wetu. Hatua ya kujiondoa ilikuwa siyo wazo nzuri. Tunarudi nyuma katika eneo la utawala bora,” alisema.

Chanzo : Mwananchi
 
Nimeshangazwa na uamuzi wa Serikali kujiondoa OGP. Hivyo nimeamua kuwasilisha swali Bungeni kutaka maelezo ya Serikali, inayojipambanua kwa kupambana dhidi ya ufisadi, kujiondoa kwenye jukwaa la Kimataifa linalopigania Serikali kuendeshwa kwa uwazi na uwajibikaji.

Uwazi ( Transparency/Openness ) ni silaha muhimu sana katika vita dhidi ya rushwa na katika kuwezesha ufanisi Serikalini.

Licha ya kwamba Tanzania ilikuwa haitimizi ahadi zote kwenye Action Plans, lakini kulikuwa na msingi kwamba Nchi yetu inaamini katika Uwazi na Uwajibikaji. Uamuzi wa Serikali kujiondoa OGP unarudisha nchi yetu nyuma. Ni uamuzi ambao haukufikiriwa Sawa sawa.
Unashangaa nini wakati nchi inaongozwa na Magufuli?

Kinachokushangaza ni kipi hasa hapo?
 
Kudhibiti Maandamano

Si umeona Leo Tundu Lissu na Hellen Kijo kisimba wameandamana wakiwa wameshika Mabango ndani ya Fence ya LHRC ingekuwa zamani ingekuwa Vurugu Mji Mzima

Maandamano yalianzia ndani ya Fence na yakaishia ndani ya Fence hiyo hiyo
Yote yatapita tu kama hayo mengine.kupitaje ndio sijui!
 
Nimeshangazwa na uamuzi wa Serikali kujiondoa OGP. Hivyo nimeamua kuwasilisha swali Bungeni kutaka maelezo ya Serikali, inayojipambanua kwa kupambana dhidi ya ufisadi, kujiondoa kwenye jukwaa la Kimataifa linalopigania Serikali kuendeshwa kwa uwazi na uwajibikaji.

Uwazi ( Transparency/Openness ) ni silaha muhimu sana katika vita dhidi ya rushwa na katika kuwezesha ufanisi Serikalini.

Licha ya kwamba Tanzania ilikuwa haitimizi ahadi zote kwenye Action Plans, lakini kulikuwa na msingi kwamba Nchi yetu inaamini katika Uwazi na Uwajibikaji. Uamuzi wa Serikali kujiondoa OGP unarudisha nchi yetu nyuma. Ni uamuzi ambao haukufikiriwa Sawa sawa.
Uamuzi uko sahihi huo, serikali inabaki na vitu vyenye tija.sasa hivi wanabaki na kitu inaitwa "Peer Review". Na pia serikalo tayari imeanzisha kitu inaitwa data portal kama sikosei taarifa /takwimu zote mhimu unapata kule

So wacha serikali ibaki na vitu vyenye tija.OGP haijawahi kuwa na umuhimu kwa nchi kama Tanzania kwa watanzania wenyewe
 
Democracy kwa Trump, sisi Tanzania hapa kazi tu
.

Watu hawali democracy bali matunda ya kazi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ni kiashilia cha kutamalaki kwa udikteta nchini.

Hawataki kuhojiwa katika maamuzi yao.
Kodi zetu wanazitapanya hovyo vile watakavyo wao.

Wananunua madege na kuanzisha miradi mbalimbali pasipo taratibu za kigavi.
Wana mpaka bajeti za kukamata wazalendo wanao pinga uonevu, wanavunja mikataba ya wawekezaji waliyoingia wao wenyewe na kulipa fidia kwa pesa za walipa kodi.

Tutavumilia maana wametuasa kuishi kama mashetani!
 
Jk hakuwa na Maamuzi Magumu tukasema tunataka Rais Mwenye Maamuzi Magumu
Ndio tulisema na sasa maamuzi magumu tunayafaidi wote ccm na ukawa.

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Back
Top Bottom