Tanzania yakopa Benki ya Dunia tsh 2.7 trilioni kwa ajili ya Elimu, Barabara na Mawasiliano!

Tatizo SGR inakula pesa kama mchwa, hizo barabara ilikuwa kuwalewesha tu msijue ukweli, barabara zinajengwa toka enzi za Nyerere.
Uko sahihi. Wengi tunaangalia tunapoangukia na tunasahau kuangalia tulipojikwaa.
Miradi mikubwa inayoendelea iliyoanzishwa siku za nyuma na kwa pamoja inaikamua Serikali. Na zege limeshakorogwa, jamvi lazima liishe.
Mama anapitia mitihani mizito kwakweli.
 
Isitoshe Kikwete anahusika na nini humo wakati Deni la Taifa limepaishwa na yule chizi.
 
Mabeberu wanashirikiana na CCM kuinunua Tanzania yetu si bure kwa mikopo hii ya kila kukicha.
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kutoka Benki ya Dunia (WB).
Tumeambiwa ni za Elimu ila hawakawii zingine kupelekwa kwenye madaraja na reli.....na zingine nyumbani.
 
Wakope kwa ajili ya maendeleo na kuimarisha miundo mbinu wezeshi. Kama hivi mgao wa umeme ni kwa nadra na tunaona kiko kinachofanyika katika umeme. Mpaka 2025 tugonge trillioni 100 na ushee ndio nitaona Mama'Rais yuko makini kujenga miundo mbinu ya kuinua uchumi na kuboresha maisha.

Tufike pahala awamu zinazofuta ziwe na kazi ya kusimamia maendeleo na kulipa madeni. Na pasitokee tena Rais katika Taifa
hili eti baada ya kuchaguliwa tu mawazo ni kwenda kutembea na kukoga jamaa zake. Tuwe na Rais ambaye kabla ya kufikiria kugombea na kuingia madarakani aanze kukuna kichwa jinsi ya kusimamia maendeleo yaliyoko na kulipa madeni.
 
Hizo hela hata kwenye elimu hazitoenda, zitaenda kwenye bwawa na reli. Hawana hela za kujengea lakin wanajifanya "wanajenga kwa fedha za ndani". Nyingine zitaingia kwenye mifuko ya viongozi wa CCM
 
Bwana madelu anaupiga mwingi sana na sasahivi naona na kauso kanawaka sijui kaanza na yeye michezo ile ya wacongo ya kitaulo, mkopo na tozo zooote kazi yake ni moja , haya bana hongereni sana kwa kuwafahamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…