Tanzania yakopa Benki ya Dunia tsh 2.7 trilioni kwa ajili ya Elimu, Barabara na Mawasiliano!

Tanzania yakopa Benki ya Dunia tsh 2.7 trilioni kwa ajili ya Elimu, Barabara na Mawasiliano!

..wakati huohuo tumetumia trillion 2 CASH kununua ndege toka kwa mabeberu.

..vilevile shirika la ndege limekuwa likipata HASARA kila mwaka.
Tunakusanya Cash tunawapelekea kulipia ndege. Baadaye wanazirudisha kama mkopo ili kugharamia huduma za jamii.
Nadhani tungekusanya ili kutatua changamoto za kijamii na kugharamia shughuli za maendeleo.

Tungekopa tunapopungukiwa na kuongezea kwenye miradi mikakati ya uwekezaji.

Inatia huruma kwamba huduma za afya na elimu kuwa tegemezi kwa fedha za mikopo. Hilo neno masharti nafuu ni lugha tu lakini mkopo ni mkopo tu.
 
Wape na dondoo (minutes) za kikao tulichokubaliana!
Dondoo sio lazima mkuu,uzuri wa tozo zinatuunganisha Watanzania bila kujali chama,dini au kipato!
Asante tozo
 
Mikopo kila uchao lakini tija ya maana wala haionekani.Tunachoshuhudia ni utitiri wa 'mashangingi' barabarani,wizi na anasa za waheshimiwa utadhani wapo ulimwengu mwingine.Ni ajabu kabisa nchi hii mpaka leo tunahangaika na madawati na matundu ya vyoo lakini tazama magari ya hao wanaoitwa viongozi wanavyoishi.Hivi Watz nani katuroga?
 
Hizo hizo ndio wanategemea wazitumie kununulia wapinzani maanake wanafahamu siku zinavyozidi kwenda ndio bei inazidi kupanda.
 
Back
Top Bottom