Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
Nimekuelewa mkuu..asante kwa mchango wako mzuri.
..nakubaliana na wewe kwamba serikali yetu kushindwa kuajiri madaktari ni uzembe.
..natofautiana na wewe kuhusu suala la kuhamia Dodoma.
..kama tunataka Central corridor na Dodoma ziendelee basi tulenge kwenye sekta ya uchumi ambayo inashirikisha wananchi wengi wa maeneo hayo.
..kwa mfano, tungeweza kuwekeza ktk sekta ya zabibu na uzalishaji wa wine/mvinyo. Au, tungeweza kuwekeza ktk sekta ya mifugo kwa kuanzisha viwanda vya ngozi na kusindika nyama. Nakumbuka zamani kulikuwa na nyama toka Kongwa Dodoma, ukienda bucha unanunua kongwa steak.
..kwa hiyo maoni yangu, kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa Dodoma na Central corridor ni njia bora zaidi ya kujenga uchumi wa eneo hilo na kuinua kipato cha wananchi kuliko kujenga ikulu na kupeleka makao makuu ya wizara za serikali.
NB:
..nimeangalia miji mikuu kama Washington DC, Berlin,Ottawa, Moscow, New Delhi, yote haiko katikati ya nchi zao. Kwa hiyo dhana kwamba mji mkuu ukiwa katikati ya nchi tunapeleka serikali/huduma karibu na wananchi inawezekana haina mashiko sana.
point yako ya mwisho ni kweli kabisa kwa sababu hata mimi niliona kuwa dodoma itahitajika kutumia nguvu nyingi ili kuisukuma kimaendeleo ukilinganisha na mikoa mingine kutokana na uchache wa rasilimali kulinganisha na mikoa mingineyo kama mwanza
Makao makuu yakiwekwa dodoma ni dhahiri kuwa watu wengi watahamia zaidi na hivyo kutengeneza soko kwa bidhaa zozote zitakazozalishwa na hii itakuwa na impact kubwa kwa wakazi wa mji huo kutokana na kukua kwa mzunguko wa pesa...
Ongezeko la watu huvutia uwekezaji na hupelekea eneo husika kukua, uwekezaji unaouhitaji waweza kufanywa na sekta binafsi kama eneo lenyewe litaonesha uwepo wa mazingira stahiki ya faida kutengenezwa...
Naliongelea hili kwa kuwa mimi nimeshakaa dodoma na hata sasa huwa ni mpitaji hivyo, nimeona hali ya muamko wa kiuchumi kutokana na hamisho hilo la makao makuu
Kwa sasa construction kwa dodoma ni kubwa sana na uwekezaji unaonekana kukua sana...
central corridor ni lazma itakua kwa uharaka kwa kutegemea serikali na sekta binafsi