Tanzania yakubali ombi la Kenya kuwapatia madaktari 500

Tatizo la hizo hela kwa maisha ya huko Kenya hazina thamani,wanaweza kuishia kula tu,maana ukienda sokoni vitu vinauzwa ghali karibia mara mbili ya bongo.

Uzuri wa hii move ni kwamba baada ya mkataba kuisha watakuja nyumbani wakiwa na uzoefu wa kutosha na serikali haitawarudisha mitaani.na kwa upande wa Kenya mshukuru mmpata madaktari wenye uwezo wa kuongea kiswahili na kiingereza,maana wataweza kufanya kazi katika kila County hadi vijijini bila tatizo lolote kwa wazeee lakini muonyeshe ushirikiano wakati tunawapima tezi dume.

🙂😀
Wabongo kwa uchokozi na maneno tume win, ndo maana majirani wanatuita waswahili...lol
 
..that is interesting.

..lakini ni kweli hatuna pesa za kuwalipa?

..mbona tumeweka order ya madege boeing 787 tena tumelipa cash, halafu unasema hatuna uwezo wa kuajiri madaktari?

..kuna dhahabu, gesi, etc inachimbwa hapa Tz mapato yanakwenda wapi kiasi cha kushindwa kuajiri madaktari?

..majuzi tumeamua kuhamisha serikali toka Dsm kwenda Dodoma. Je pesa za zoezi hilo zimetoka wapi? Kwanini zisitumike kuajiri madaktari na kuwasambaza nchi nzima?
Tuliweza kulipa watumishi hewa kwa miaka, iweje pesa hizo zisielekezwe kwenye ajira za madaktari? Idara ya mahakama ilipewa mabilioni mapema kabisa, pesa zilitoka wapi? Tunagawa mikoa na kuongeza gharama za utawala. Mikoa mipya haina madaktari lakini ina watumishi wa kada nyingine hasa za siasa, pesa zinatoka wapi?
Tulitumia Bilioni 7 za uchaguzi wa Marudio kulee, pesa zilizotoka wapi?
Tume ya uchaguzi ilirudisha bilioni 12 kwasababu hazikutumika, kwanini tunakosa kwa madaktari?
Tuliweza kupanua ukumbi wa bunge kwa mabilioni, za kulipa madaktari zinakosenekaje?
Lini pesa za kulipa wabunge mishahara na allowance zao zilikosekana?
 
Mkuu hivi unategemea mtu kama MK254 akupe majibu ya kina ya swali hilo au ataishia kukucheka na kukukejeri tu

Nimcheke kwa lipi hapo, labda niwe chizi. Huyo jamaa joka kuu huwa tunatofautiana naye kwa mengi lakini kwa hili anauliza maswali ya msingi sana tatizo nyie ving'ang'anizi mkikaririshwa kitu hamuachi. Kuwa na madaktari kitaa waliohitimu taaluma hadi wakaiva ni jambo la aibu hususan kwa nchi inayotumia mabilioni kwa mambo ambayo hayana umuhimu (priority) kwa sasa hivi.
Doctor to patient ratio ya Tanzania ni mbaya sana zaidi ya Kenya, yaani daktari mmoja kwenu anahudumia Watanzania 25,000 hivyo pamoja na kwamba nina furaha kuona mnawatuma hao vijana waje ili kuongeza idadi ya madaktari kwetu, lakini pia inahuzunisha maana huko wanatoka hali ni mbovu.
Ni kama itokee muwe na tatizo la njaa halafu papo hapo mtume mahindi kwa nchi iliyo na shibe zaidi yenu, haileti mantiki.
Kwetu Kenya, msemaji wa ikulu ameeleza wazi kwamba hatuna madaktari kitaa wasiokua na ajira, wameajiriwa wote na kila anayehitimu ananyakuliwa mara moja.

Hao vijana wanaokuja kutokea Tanzania watalipwa mishahara hata zaidi ya madaktari wazoefu huko Bongo.
 
Mkuu kwani mgomo wa Madaktari umekwisha? Nafikiri kuna umuhimu wa madaktari wa Tanzania kuwa support wenzao wa Kenya kama madai yao yana substance - haya mambo ya kusema kama Madaktari wa Kenya wamegoma basi Watanzania wachukue nafasi zao hiyo haipendezi hata kidogo - kwenye mazingira kama hayo hata Madaktari wa Tanzania hawatakua na amani wakiwa nchini Kenya, tusije tukajidanganya hapa. Kama mgomo usingekuwepo alafu Serikali ya Kenya ikaomba Tanzania kupeleka Madaktari kuziba pengo la upungufu wa Madaktari Nchini mwao hilo linge eleweka, lakini siyo kwenye hali ya hivi sasa - hayo ni maoni yangu sina nia mbaya usalama kwanza kwa Madaktari wetu ndiyo jambo la muhimu.

Mgomo umeisha, madaktari wameongezwa hela nyingi sana. Serikali ya Kenya imeomba madaktari zaidi kutoka Tanzania ili kuongeza idadi ya doctors to patient ratio na pia kupunguza adhari za mgomo.
 
Ni common sense tu itakwambia nini kinapaswa kufanyika. Sasa hivi zaidi ya 50% ya mapato ya serikali inatumika kulipa mishahara, usipoongeza mapato ya serikali na kuendelea kuajiri nini kitatokea?

Acheni ushabiki usio na tija, nyie ndio mnafanya harusi kubwa halafu mnalalamika maisha magumu. Kujenga Dodoma na hayo unayosema havina uhusiano wowote. Bado hospitali na zahanaati zinaendelea kujengwa.

Kwa taarifa yako tu, hayo matatizo yapo Afrika nzima na sio Tanzania peke yake. Hao madaktari hata wasingeenda Kenya wangekaa nyumbani tu bila kazi.
Nadhani kuna kitu usichoelewa na hutamwelewa JokaKuu.

Fikra zako zimezama katika kuongeza mapato ndio maana ukaona ni vema kununua Dreamliner kwasababu serikali itapata mapato.

Usichobaini ni impact ya health katika jamii, na gharama katika serikali.

Unawezaje kuiweka thamani ya afya ya mwanadamu katika mahesabu?

Pili, kipi bora kuajiri madktari au kusbiri idadi kubwa ya wagonjwa kulazwa/kufa katika hospitali?

Ukiwatumia madaktari vema, gharama za afya zitapungua kwa kila kipimo, i.e quality of life ita improve,kutakuwa na cost reductions na haya yatapunguza gharama za afya

Kwa maneno mengine utakuwa na health nation lenye ''quality of life'' na kuongeza productivity

Kwa nchi za wenzetu, kuna uwekezaji katika mambo 3 makubwa. Elimu, afya na utafiti

Ukiwa na elimu hutakuwa na bajeti ya kipindu pindu au kuhara

Ukiwa na afya utapunguza gharama za uendeshaji wa hospitali na kuwa taifa lenye afya na uzalishaji

Haya utayafanya ukiwa na uwekezaji katika utaifiti

Sisi tunawekeza katika siasa, halafu tunasema hakuna pesa.

Mikoa imegawanywa kuongeza eneo la utawala na majimbo.

Hilo limeongeza gharama za uendeshaji wa serikali lakini hospitali katika mikoa hazina madaktari kwasababu hakuna pesa za kuwalip! Haa utasemaje hakuna pesa?

Kushindwa kufanya priority si kukosa pesa
 
Mkuu kwani mgomo wa Madaktari umekwisha? Nafikiri kuna umuhimu wa madaktari wa Tanzania kuwa support wenzao wa Kenya kama madai yao yana substance - haya mambo ya kusema kama Madaktari wa Kenya wamegoma basi Watanzania wachukue nafasi zao hiyo haipendezi hata kidogo - kwenye mazingira kama hayo hata Madaktari wa Tanzania hawatakua na amani wakiwa nchini Kenya, tusije tukajidanganya hapa. Kama mgomo usingekuwepo alafu Serikali ya Kenya ikaomba Tanzania kupeleka Madaktari kuziba pengo la upungufu wa Madaktari Nchini mwao hilo linge eleweka, lakini siyo kwenye hali ya hivi sasa - hayo ni maoni yangu sina nia mbaya usalama kwanza kwa Madaktari wetu ndiyo jambo la muhimu.
Bukyanagandi technically mgomo wa madaktari Kenya umeisha, saivi wapo ktk hang over tu ya mgomo wao, after 1months utakuwa umeshasaulika. Hii process ya recruitment ya Tz Drs sio a one week thing, hadi wanakuja kumaliza process zote na kuondoka itakuwa mid April probably, kwa muda huo hang over ya mgomo itakuwa imepungua sana.
 
Nimcheke kwa lipi hapo, labda niwe chizi. Huyo jamaa joka kuu huwa tunatofautiana naye kwa mengi lakini kwa hili anauliza maswali ya msingi sana tatizo nyie ving'ang'anizi mkikaririshwa kitu hamuachi. Kuwa na madaktari kitaa waliohitimu taaluma hadi wakaiva ni jambo la aibu hususan kwa nchi inayotumia mabilioni kwa mambo ambayo hayana umuhimu (priority) kwa sasa hivi.
Doctor to patient ratio ya Tanzania ni mbaya sana zaidi ya Kenya, yaani daktari mmoja kwenu anahudumia Watanzania 25,000 hivyo pamoja na kwamba nina furaha kuona mnawatuma hao vijana waje ili kuongeza idadi ya madaktari kwetu, lakini pia inahuzunisha maana huko wanatoka hali ni mbovu.
Ni kama itokee muwe na tatizo la njaa halafu papo hapo mtume mahindi kwa nchi iliyo na shibe zaidi yenu, haileti mantiki.
Kwetu Kenya, msemaji wa ikulu ameeleza wazi kwamba hatuna madaktari kitaa wasiokua na ajira, wameajiriwa wote na kila anayehitimu ananyakuliwa mara moja.

Hao vijana wanaokuja kutokea Tanzania watalipwa mishahara hata zaidi ya madaktari wazoefu huko Bongo.
Kwanza tuweke facts sawa, Dr to patient ratio Tz si 1:25,000, ukitumia figure hiyo unamaanisha Tz tuna Drs 2000 wanao practise wakati kila mwaka tunazalisha zaidi ya madaktari 1000. Naomba usitumie tena hizo figures.

Kutokana na Naibu waziri wa Afya Tz, wana mpango wa kuajiri madaktari 450 mwaka huu, tukumbuke vilevile hauwezi kuajiri madaktari wengi tu wakati hauna miundo mbinu ya kuwapeleka wakafanyia kazi, ni uamuzi sahihi kuwaruhusu madaktari wetu waende Kenya kwa sasa wakati tuna deal na changamoto.
 
Nadhani kuna kitu usichoelewa na hutamwelewa JokaKuu.

Fikra zako zimezama katika kuongeza mapato ndio maana ukaona ni vema kununua Dreamliner kwasababu serikali itapata mapato.

Usichobaini ni impact ya health katika jamii, na gharama katika serikali.

Unawezaje kuiweka thamani ya afya ya mwanadamu katika mahesabu?

Pili, kipi bora kuajiri madktari au kusbiri idadi kubwa ya wagonjwa kulazwa/kufa katika hospitali?

Ukiwatumia madaktari vema, gharama za afya zitapungua kwa kila kipimo, i.e quality of life ita improve,kutakuwa na cost reductions na haya yatapunguza gharama za afya

Kwa maneno mengine utakuwa na health nation lenye ''quality of life'' na kuongeza productivity

Kwa nchi za wenzetu, kuna uwekezaji katika mambo 3 makubwa. Elimu, afya na utafiti

Ukiwa na elimu hutakuwa na bajeti ya kipindu pindu au kuhara

Ukiwa na afya utapunguza gharama za uendeshaji wa hospitali na kuwa taifa lenye afya na uzalishaji

Haya utayafanya ukiwa na uwekezaji katika utaifiti

Sisi tunawekeza katika siasa, halafu tunasema hakuna pesa.

Mikoa imegawanywa kuongeza eneo la utawala na majimbo.

Hilo limeongeza gharama za uendeshaji wa serikali lakini hospitali katika mikoa hazina madaktari kwasababu hakuna pesa za kuwalip! Haa utasemaje hakuna pesa?

Kushindwa kufanya priority si kukosa pesa

Hayo mambo yote unayosema hayawezekana kama kipato ni kidogo. Namna pekee ya kuongeza ufanisi kwenye afya ni kuongeza gharama za matibabu au kila mwananchi atafute bima ya afya.

Watu wanapata wanachostahili, hawataki kulipa kodi wala kuchangia huduma za afya kwa kiwango kinachotakiwa.

Afya kuwa kipaumbele haimaanishi kuwa mapato yote ya serikali ndio yatumike kwenye afya.
 
Nimcheke kwa lipi hapo, labda niwe chizi. Huyo jamaa joka kuu huwa tunatofautiana naye kwa mengi lakini kwa hili anauliza maswali ya msingi sana tatizo nyie ving'ang'anizi mkikaririshwa kitu hamuachi. Kuwa na madaktari kitaa waliohitimu taaluma hadi wakaiva ni jambo la aibu hususan kwa nchi inayotumia mabilioni kwa mambo ambayo hayana umuhimu (priority) kwa sasa hivi.
Doctor to patient ratio ya Tanzania ni mbaya sana zaidi ya Kenya, yaani daktari mmoja kwenu anahudumia Watanzania 25,000 hivyo pamoja na kwamba nina furaha kuona mnawatuma hao vijana waje ili kuongeza idadi ya madaktari kwetu, lakini pia inahuzunisha maana huko wanatoka hali ni mbovu.
Ni kama itokee muwe na tatizo la njaa halafu papo hapo mtume mahindi kwa nchi iliyo na shibe zaidi yenu, haileti mantiki.
Kwetu Kenya, msemaji wa ikulu ameeleza wazi kwamba hatuna madaktari kitaa wasiokua na ajira, wameajiriwa wote na kila anayehitimu ananyakuliwa mara moja.

Hao vijana wanaokuja kutokea Tanzania watalipwa mishahara hata zaidi ya madaktari wazoefu huko Bongo.

Hizo doctors to patient ratios mnazitoa wapi jamani, mbona kueneza mahabari ya uongo daily. Not every internet sources are real and not all information is in the internet.
 
Ni kweli hii itakuwa ahueni, unajua inauma sana kuona mtu wa taaluma nyeti kama udaktari kakaa mtaani akisubiri ajira kwa mda mrefu

Wacha waende huko wakasaidie ndugu zetu wakenya
Hili ni sawa na kusema umechaguliwa kwenda kuhubiri injiri ndani ya msikiti wa Baghdad
 
Kwanza tuweke facts sawa, Dr to patient ratio Tz si 1:25,000, ukitumia figure hiyo unamaanisha Tz tuna Drs 2000 wanao practise wakati kila mwaka tunazalisha zaidi ya madaktari 1000. Naomba usitumie tena hizo figures.

Kutokana na Naibu waziri wa Afya Tz, wana mpango wa kuajiri madaktari 450 mwaka huu, tukumbuke vilevile hauwezi kuajiri madaktari wengi tu wakati hauna miundo mbinu ya kuwapeleka wakafanyia kazi, ni uamuzi sahihi kuwaruhusu madaktari wetu waende Kenya kwa sasa wakati tuna deal na changamoto.

Kulingana na takwimu za Sikika, mnamo 2012 mlikua na madaktari 2,250 ambapo hapo tunahesabu wote, ikiwemo wale wanafanya kazi kwenye NGOs na mashirika mengine, kwamba waliosalia kuhudumu kwenye mahospitali ya kiserikali walikua wachache.
Anyway nakubaliana na wewe kwamba hauwezi ukaajili madaktari tu bila kuwa na mpango wa kuwaandalia miundo mbinu.
 
Ebu tusaidie hilo chapisho la sikika ulipoona Tz wana 2250 Drs tu (2012). Na hizo takwimu za Kenya, Uganda na Rwanda ni za sikika pia ? Batch ya interns ikimaliza Oct tutakuwa na zaidi ya 2000 Dr mtaani kabla ya kuajiriwa, kusema Tz nzima kuna 2250 Drs wakati Oct tu mtaani kutakuwa na Drs almost 2000 inaonyesha utata wa takwimu zenu na hoja tosha ya kukufanya usitumie hiyo takwimu vingenevyo uwe na nia ovu.
 
Mhh wapumbavu wako fery mbona bongo madaktari hawatutoshi! AAA halafu madaktari wetu mitumbaa? Wanunuliwa kwa being chee Kenyatta kashindwa kuwapandishia dau ndiyo maana kaamua kuchukua mitumba halafu hawa jamaa watazua xenophobia kama ile ya juz juz south
 
IMG_0330.JPG
 
Ila kuna watu wako impartial sana jamani.

Hongera sana mkenya....njoo huku wanyaturu tukupe mke

Hehehe Wanyaturu nawavulia kofia, raha sana. Vipi unapafahamu Singidani, au unafahamu namfua.
Mboyane!!!
 
Back
Top Bottom