Ndg yangu kuongeza ufanisi si kutoza watu au bima au kujenga mortuary
Kuongeza ufanisi katika sekta ya afya ni kupunguza mzigo 'burden' kwa serikali
Sekta ya afya haiingizi na haitaweza kuingiza mapato kama bandari, elewa hilo
Sekta ya afya ni ya kutoa huduma. Hata hivyo, ina mchango mkubwa katika mapato
1. Ukidhibiti maradhi kama communicable diseases unapunguza gharama za uendeshaji wa hospitali na hapo umepunguza mzigo wa serikali na kuelekeza resource kwingine
2. Ukipunguza maradhi, unaongeza productivity kwa wananchi
Kuna njia mbili au tatu, kwanza, prevention, na pili curative.
Yote mawili yanategemea utaalam wa afya ambao ni madaktari na wengine.
Utashangaa nikikuambia kuwa gharama zinazotokana na matibabu ya communicable diseases ni kubwa sana na kimahesabu ukidhibiti hayo, unaweza kununua Dreamliner zako kila mwezi.
Elewa 'qualitative and quantitative analysis' ya healthcare huwezi kui scale na dreamliner, never! Huwezi kupata matokeo ya healthcare kirahisi kama dreamliner kwasababu ni kitu complicated na pengine ndio maana unadhani ni suala la kujenga mortuary nyingi za kuhifadhi maiti na kununua bima!
JokaKuu