Tanzania yalipa Fidia ya Tsh. Bilioni 75 kwa kufuta Leseni ya Kampuni ya Madini

Tatizo hata TISS wanawaza ki ccm kazi kucizia teuzi kupiganania chama badala ya inchi
 
Tunapigwa kijinga tu. Unampa mtu leseni halafu hawekezi au kutekeleza makubaliano hadi unafuta leseni. Halafu anakushitaki arbitration unakubali wewe kulipa usd milion 30? Hii chini ya jpm isingetokea. Sio kwamba angekwenda kinyume na sheria ila team yake ya wanasheria ingewabwaga hao wawekezaji kwani kusingekuepo uhuni wa kupiga hela hivyo.
 
Mkuu acha kutoa sifa ambazo hujui..
Akiwa hai ndege ilidakwa Canada..

Kabudi akaenda kumpiga biti balozi wa Canada.. Wakati mtu anayetudai kafuata taratibu za kusajili kesi mahakama za Canada..

JPM alituma wanasheria.. Tulilambwa billioni 90 na ndege ikaachiwa kimya kimya...
Huwezi kuvunja mikataba kibwege kisha ufikiri utashinda kirahisi..
 
Ni kwa nini haitumiki lugha kuwa "tumeshindwa kesi" na badala yake tunasema "tumeingia makubaliano" ya kulipa?
 
Wakulaumiwa hapa ni TISS sorry to say this
 
Symbion katupiga,IPTL kashatupiga na sasa Winshear kututwanga.Ila siyo bure huyu Mstaafu na genge lake ni lazima wadhibitiwe,tunakoelekea hili taifa litafirisika kama Ugiriki!
 
Ila hii nchi kwa kweli, hapana aisee. Kwamba mtu kapiga 75bn bila kufanya kazi yeyote. Ni mkataba tu kuvunjwa basi.
Hawa viongozi tuliowaamini wana mgao! Wao ndo wanapanga fidia kiasi gani! Unakuta mlalamikaji wala hana neno na alishindwa kwenye kesi ya msingi ya kwanza! Sasa wanamwendea na kumlazimisha aifufue hiyo kesi na atashinda kwa fidia (labda tuseme 1 billion). Hawa watanzania mafisadi wanasema andika fidia billion 75. Wewe tutakupa billion 5 alafu billion 70 ni zetu! Kesi inaendeshwa kimagumashi kimyakimya mara Tanzania imeshindwa kesi na fasta from nowhere muamala wa billion 75 unalipwa!
 
Ni mjinga tu anayeweza kusapoti na kuacha mikataba mibovu.ni bora tuvunje kuliko kukaa na mikataba mibovu.
Unaweza onyesha ubovu wa ule mkataba, na hasa kipengele kilicho pelekea kuvunja?

Na kwa nini tumeshindwa kesi na kupeleke kuwalipa mabilioni ya shillingi?
 
Ni mjinga tu anayeweza kusapoti na kuacha mikataba mibovu.ni bora tuvunje kuliko kukaa na mikataba mibovu.
Fuatilia kwa umakini. Hiyo haihusiani na mikataba.

Hiyo hapo ni Retention license iliyofutwa bila ya kufuata taratibu. Ni sawa mtu uamue kuanzisha shamba, ukafuata taratibu zote, ukaomba hati ukapewapewa, ukalima, kabla ya kuvuna mazao, serikali ikasema imefuta mashamba yote, na yale mashamba yote yaliyokuwa na hati, hati zimefutwa, yamekuwa mashamba ya Serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…