Tanzania yaomba Benki ya Exim China kusaidia fedha za ujenzi wa SGR

Tanzania yaomba Benki ya Exim China kusaidia fedha za ujenzi wa SGR

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), amefanya mkutano kwa njia ya mtandao kutoka jijini Dodoma na Rais wa China Exim Bank, Bw. Ren Shengiun, ambapo wamejadili kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo ikiwemo upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine, DKT. Nchemba, ameiomba Benki hiyo kusaidia upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambao ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele ya nchi kwa sasa.

Kwa upande wa Tanzania Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara hiyo, Bw. Rished Bade na Kamishna Msaidizi wa Usimamizi wa Madeni, Bi. Tiba Kisonga na maafisa wengine wa Wizara.

Wizara ya Fedha
 
Lakini hawa watu wanamatatizo kweli.

Mwigulu juzi tu bungeni amebishana na Mpina na kudai SGR ujenzi wake ni EPC+F

Leo tena serikali ndio inatafuta hela ya mradi (kitu ambacho Mpina alisema) wakakataa mbele ya makamera.

Haiwezekani mtu kuwa mshahaulifu haraka ivyo.
 
Lakini hawa watu wanamatatizo kweli.

Mwigulu juzi tu bungeni amebishana na Mpina na kudai SGR ujenzi wake ni EPC+F

Leo tena serikali ndio inatafuta hela ya mradi (kitu ambacho Mpina alisema) wakakataa mbele ya makamera.

Haiwezekani mtu mkusahulifu haraka ivyo.
Yote na yote bila shaka Dr alipata makofi mengi mengi.Sijui wakiona hili bakuli wataomba makofi yao yarudishwe au vipi.
 
Kila wakilala na kuamka ni maombi maombi tu ... Kwa nini wasiende kwa hawa manabii na makuhani wa ndani?
 
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), amefanya mkutano kwa njia ya mtandao kutoka jijini Dodoma na Rais wa China Exim Bank, Bw. Ren Shengiun, ambapo wamejadili kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo ikiwemo upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine, DKT. Nchemba, ameiomba Benki hiyo kusaidia upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambao ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele ya nchi kwa sasa.

Kwa upande wa Tanzania Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara hiyo, Bw. Rished Bade na Kamishna Msaidizi wa Usimamizi wa Madeni, Bi. Tiba Kisonga na maafisa wengine wa Wizara.

Wizara ya Fedha
If the owners of the natural resources goes around begging, then you should know there's something wrong with their minds...😒
 
Sijui ni nini maana ya kuwa na viongozi kama siku zote wanawaza option rahisirahisi.

China haikujengwa kirahisirahisi kwa kukopakopa na kusaidiwasaidiwa, baadala yake wachina walitoka damu na kufa kuijenga China.
 
Kodi zinazokusanywa ndani hazitoshi kwahiyo wanazikwepa kuziiba, iliziweze kulipa mishahara na viposho vidogo vidogo.
Hawa watawala wanaotembelea magari yenye herufi tu, wizi wanaufanya kwenye hiyo mikopo na mikataba.
 
Aliyerirhi mikoba kutoka Kwa mzalendo he ana uwezo wa kuongoza nchi.pesa zinaliwa tu na wajanja.
 
Wangemaliza SGR Lot 1 na 2 kwanza na treni zifanye kazi kabisa, waanze kukusanya mapato
 
Tumekuwa nchi ya ombaomba kama Matonya ni aibu kubwa na ni kunizairisha.huyu mama si aondoke tu kulinda heshima yake?
Kodi zikiongezwa mnalia Lia wacha wakope tu vizazi vijavyo watalipa
 
Back
Top Bottom