Tetesi: Tanzania yaondolewa kwenye mradi wa kimataifa kuhusu nishati endelevu kikwazo kikiwa ni sheria ya takwimu

Tetesi: Tanzania yaondolewa kwenye mradi wa kimataifa kuhusu nishati endelevu kikwazo kikiwa ni sheria ya takwimu

We unajifanya unaakili na kujua kuitafsiri sheria ya takwimu kuliko serikali yetu tukufu iliyotunga hiyo sheria?
Naomba nikujulishe kuwa mie sijifanyi nina akili, kiukweli wewe una akili zaidi yangu! Mie kazi yangu ni kusema ukweli na Kwa bahati nzuri sheria ya takwimu naijua sana kuliko wewe na ndugu zangu wapinzani wa kila jambo ingawa akili yangu ndogo kuliko mtoto aliyezaliwa leo
 
Naomba nikujulishe kuwa mie sijifanyi nina akili, kiukweli wewe una akili zaidi yangu! Mie kazi yangu ni kusema ukweli na Kwa bahati nzuri sheria ya takwimu naijua sana kuliko wewe na ndugu zangu wapinzani wa kila jambo ingawa akili yangu ndogo kuliko mtoto aliyezaliwa leo
Kwa hiyo hao wanaoipinga hawajaielewa sheria au?
 
...NB: Siwezi kuweka source kwa kuogopa kuichongea hiyo taasisi ya kimataifa na watu walio kwenye wizara walioridhia Tanzania kuondolewa kwenye huo mradi.
Udaku wa namna hii ndio makamanda wanaupenda. Yaani hide my ID please. Bila source, ha ha ha.
 
Endeleeni kumsifia huyu mtu, hadi nchi itakapovurugika ila msije kusema hatukuwambia.
 
Utasikia chadema ndio walio sababisha
 
Weka link acha uoga wa kipuuzi.
Hili sio suala la link ni habari kutoka jikoni ambako na mie nipo. Huo ni mradi wa kitengo cha World Bank ambao ulikuwa unahitaji Tanzania kutoa statistics ambazo haijapitishwa na serikali. Hilo ndio nitakueleza. Kama unataka nenda ofisi za World Bank kawaulize wakupe habari zaidi.
 
Kwa hiyo taarifa hii ni siri?
Nani mna/wanamuogopa hadi waogope kutoa taarifa hadharani?
Weka link acha ubabaishaji wa kipuuzi.
 
Tanzania imeondolewa katika mradi wa kimataifa unaohusu mambo ya nishaji endelevu (sustainable energy management) sababu ikiwa ni matatizo ambayo wafadhiri wa mradi wanaona watapambana nayo kutokana na sheria ya Tanzania ya takwimu.

Mradi huo unahusu pia kuzifanyia upembuzi taarifa na takwimu zinazotolewa na serikali nishai, na pale zinapoonekana zina makosa kutumia njia nyingine zutakazoonyesha nini kinapaswa kuwa kweli (interpolation/extrapolation methods). Wafadhiri wa mradi huo walielezwa kwamba sheria ya Tanzania kuhusu takwimu haitawaruhusu kutoa maoni mbadala juu ya takwimu za Tanzania, hata kama zinaonekana kuwa hazisemi kweli.

Zaidi ya hilo, wataalamu hao walikabiliana na tatizo la Tanzania kuhudhuria mikutano na semina za mradi huo pale ambapo zilifanyika nje ya Tanzania, kutokana na ugumu wa Watanzania kupata ruhusa ya kutoka nje ya nchi.

Hatimaye wafadhiri wa mradi huo, baada ya majadiliano na wahusika wa mradi upande wa Tanzania, waliamua kuiondoa Tanzania kwenye huo mradi.

NB: Siwezi kuweka source kwa kuogopa kuichongea hiyo taasisi ya kimataifa na watu walio kwenye wizara walioridhia Tanzania kuondolewa kwenye huo mradi.
Nadhani siyo kuchongea. Ni kweli tupu. Sheria zingine zilitungwa bila kushirikisha wadau, yaani hapakuwa na ignorance of corporate veil. Hilo ni tatizo ambalo litatusumbua sana. Lingine la safari ni kweli, kibali mtu unatakiwa kuomba 14 days kabla ya safari, na mara nyingi safari huwa ghafla, ingawa kuna dharula na inafanya kazi kwa masharti
 
Pamoja na kuwa sina haja ya kubishana nawe Synthesizer ila Sheria ya Takwimu haikatazi kuksoa takwimu za NBS! Wala haikatazi kuchukua takwimu kwa matumizi ya taasisi au mtu binafsi! Ni kawaida wadau kukosoa kwa data takwimu rasmi kama 10 fundamental principle of official statistics. Tatizo ni watu wankurupuka na kutangaza takwimu zisizo na uhalisia kwa kutumia sample ambayo si representative of the population.

Hivi unajua kukosoa takwimu zilizotolewa na serikali ni kosa kwa sasa au haupo Tanzania. Kwa taarifa yako Zitto anakabiliwa na kesi hiyo, shauri yako
 
Swafiiii sana walahi
Tutakuwa kama Norway
 
Hiyo mijitu ni mijizi tu, tupa kule walahi
 
Back
Top Bottom