Benki Ya Standard Chatered Yaikopesha Tanzania Sh. Trilioni 3.3 Kujenga Reli Ya Kisasa-SGR
Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa unaohusisha awamu mbili, Kipande cha kwanza kati ya Dar es Salaam na Morogoro (kilomita 300), ambacho kilianza kujengwa Mei 2, 2017 na ilitakiwa kikamilike ifikapo Novemba 2, 2019 kwa gharama ya Sh trilioni 2.7.
wakati kipande cha pili kinachoanzia Morogoro –Makutupora (Manyoni, Singida) (kilomita 422), kilianza kujengwa Februari 26, 2018 na kinatakiwa kikamilike baada ya miezi 36 yaani Februari 25, 2021 kwa gharama ya Sh trilioni 4.4.
Wakati wa uzinduzi wa reli hii, rais Magufuli alisema hii reli ya kisasa inajengwa kwa fedha za ndani.
“Uchumi unakua na ushahidi ni miundombinu tunayojenga, tumebana fedha za mafisadi, tumebana fedha za wapigadili, tumenunua ndege mpya sita, zitakuza utalii, biashara na kulifikisha lori letu linakotaka kwenda.
“Nawaambia siku moja mtaikumbuka awamu ya tano ya kazi, lakini nafahamu katika usafiri wowote unapopakia abiria uhitaji kuwauliza watasimama kuangalia sehemu gani wakati lori linaondoka.
“Wako watakaotazama nyuma, ubavuni, kule lori linakoelekea, kama ukipakia wasukuma wanaweza kuimba kwenye lori.
“Dereva mzuri hutakiwi kusikiliza nyimbo, kuangalia watu walikotazama, angalia unakolipeleka lori ili lifike salama. Kwa hiyo nawahakikishia mimi najiamini ni dereva mzuri na kwenye lori langu limepakia watu wa aina hiyo, wako wanaoimba, wanaopiga stori, wanaotazama nyuma wakati lori linakwenda mbele, walioangalia mbele, ubavuni, lakini lori litafika kule linakokwenda na hili ni lori la maendeleo.
“Na katika kazi tunazofanya, wanaopiga kelele ni wale waliozoea kupiga dili, waendelee, lakini lori litakwenda hadi linakotaka,” alisema Dk. Magufuli.
“Mlinituma nifanye, haya yote ninayofanya kweli ni mabaya? (wananchi wakaitikia mazuri).”
Akauliza tena: “Wangapi wanasema mazuri (wananchi wakanyoosha mikono), … kwahiyo niendelee? (wananchi wakaitikia)
“
Tulionewa sana, tumechezewa sana, tumedharauliwa mno, Tanzania ni tajiri, hatutakiwi kuwa ombaomba. Tuna ubaya gani kwa Mungu, dhahabu zipo, wanyama wapo, lakini sisi ni masikini, ni lazima tujitambue,” alisema rais Magufuli
Alisema Watanzania wanapaswa kujivunia kujenga reli hiyo kwa fedha zao kwani sehemu kubwa ya reli ya kati ilijengwa na wakoloni (Wajerumani na Waingereza) kwa miaka 30 na reli ya Tazara iliyojengwa miaka ya 1970 ambayo ilijengwa kwa ufadhili wa China.
Mwisho wa kumnukuu.
MY TAKE:
Hivi karibuni imeelezwa mvua ndizo zilisababisha mradi usikamilike kwa wakati.
Naomba msitaje neno beberu kwenye mada yangu. Wote tunajenga nchi moja. Kama kuna Mdau kajitokeza kutusaidia mkopo, tuukubali ili tuweze kijikomboa. Hii nchi ilichezewa sana.
1.
Wakati Rais Magufuli anasema "hela zipo" Tanzania yaiomba Benki ya Dunia kusaidia ujenzi wa SGR