Tanzania yapata Mkopo wa Sh. Trilioni 3.3 toka Standard Chartered Bank kwa ajili ujenzi reli ya SGR

Tanzania yapata Mkopo wa Sh. Trilioni 3.3 toka Standard Chartered Bank kwa ajili ujenzi reli ya SGR

Ni wazi huu ni commercial loan (non-concessional loan).. sijui itakuwa Stan Chart ya wapi? Singapore au China? Ila kwa haraka haraka ni kwamba

Interest rate itakuwa ni kubwa sana, unaweza kuta hata ni 12%

Nadhani kuna michezo michafu ya serikali kutengeneza mazingira ya kwenda kukopa kwenye hizi benki za kibiashara badala ya kutafuta cheap funding IMF na World Bank - IDA ambapo interest rate ingeweza kuwa ndogo.

Kwenye hizi mikopo kwenye mabenki ya kibiashara nahisi kuna watu wanakula 10% kubwa sana.

Mtu mwenye akili huwez kuacha kutafuta mikopo ya riba nafuu IMF au World Bank, ukaanza kukimbilia benki za kibiashara.

POOR DECISION, POOR LEADERSHIP!!!!!!!
 
Benki Ya Standard Chatered Yaikopesha Tanzania Sh. Trilioni 3.3 Kujenga Reli Ya Kisasa-SGR

Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa unaohusisha awamu mbili, Kipande cha kwanza kati ya Dar es Salaam na Morogoro (kilomita 300), ambacho kilianza kujengwa Mei 2, 2017 na ilitakiwa kikamilike ifikapo Novemba 2, 2019 kwa gharama ya Sh trilioni 2.7.

wakati kipande cha pili kinachoanzia Morogoro –Makutupora (Manyoni, Singida) (kilomita 422), kilianza kujengwa Februari 26, 2018 na kinatakiwa kikamilike baada ya miezi 36 yaani Februari 25, 2021 kwa gharama ya Sh trilioni 4.4.
John alikuwepo wakat wa kusaini mkopoooo ?
 
Naantombe Mushi,
Hivi hizi bank za biashara huwa zinanufaikaje kukopesha matrion yote hayo kwa just 12% kwa miaka 20 au huwa wanapata upendeleo fulani kutoka serikalini kwa sababu ya hiyo mikopo
 
Hizo habari siyo za kweli kabisa maana tulisha ambiwa kuwa hii reli tunajenga kwa fedha zetu wenyewe figganigga,

In God we Trust
 
Si walisema SGR inajengwa kwa kodi za ndani.....
 
Hivi hizi bank za biashara huwa zinanufaikaje kukopesha matrion yote hayo kwa just 12% kwa miaka 20 au huwa wanapata upendeleo fulani kutoka serikalini kwa sababu ya hiyo mikopo
Ni kwasababu wanakopesha mikopo ya dola, ambapo unakuta cost of funding kwa dola ni kama 2.5% kwa mwaka kwa sasa hivi, so hapo kama wanatupa kwa asilimia 12% ina maana wenyewe wanatengeneza pesa nzuri sanaaa.

Kuna margin karibu 9% watakuwa wanatengeneza ambayo kwa huo mkopo ni pesa nying sana

Na ujue kwamba huko mbeleni kama itatokea labda USA wakapandisha interest rate, ina maana cost of funding itaongezeka so hata hilo deni letu pia riba zitakuwa zinaongezeka, ambayo kwetu sisi ndo tutakuwa tunaumia maana interest zitakuwa kubwa sana. Ndo mana nchi kuwa na mikopo mingi sana ya dola sio kitu kizuri. Its a disaster.
 
Back
Top Bottom