Tanzania yashika nafasi ya kwanza kwa usambazaji wa Umeme Vijijini Barani Afrika

Tanzania yashika nafasi ya kwanza kwa usambazaji wa Umeme Vijijini Barani Afrika

Jamani mbona hapa kwetu Morogoro manispaa kabisa mkundi hakuna umeme tunapambana na sola tuu???🙄🙄🙄🙄
 
Mnasemea vijiji gani? Kijijini kwetu mbona hamna Umeme? Hata nguzo tu hamna yaani hata ile dalili tu ya kuwekewa umeme hamna.

Mradi wa REA tu wenyewe umeshindikana kumalizika mmeacha nguzo zimesimama mkaondoka sijui mnatuonaje sisi wananchi.
Kijijini kwenu mtakuwa kwenye idadi ya vijiji 3000 vilivyosalia kuwekewa umeme.
 
Tanzania ilikuwa inashindana na nchi zipi? Je, nchi hizo zilijua kuwa nazo zinashindana na Tanzania katika hili? Msikubali kutumiwa kama propaganda ya chama cha siasa. Nyie ni shirika la serikali.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Tanzania imeshika nafasi ya kwanza barani Afrika kwa kufanikiwa kusambaza umeme nchini kote kwa asilimia 80.

Mhe. Majaliwa aliyasema hayo wakati akielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano kwenye mkutano wa viongozi wa dini kutoka kamati za amani za Mikoa mbalimbali Tanzania bara na Zanzibar, uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

“Leo hii Tanzania ni ya kwanza barani Afrika kwa kusambaza umeme kote nchini hadi vijijini na kufikisha asilimia 80. Kuna nchi ngapi barani Afrika, lakini Tanzania imefanikiwa kuwa ya kwanza. Tumeweza kufikia vijiji 9,112 Tanzania na hadi Aprili 2020 na tumetumia shilingi trilioni 2.27,” amesema.

Akizungumza na viongozi waliohudhuria mkutano huo uliandaliwa ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika ustawi wa amani, uzalendo na kumtanguliza Mungu, Waziri Mkuu amesema ushirikiano mkubwa wanauonesha kwa Serikali, umewezesha kufanya mambo mengi ikiwemo kuimarisha huduma za upatikanaji wa nishati kwa ajili ya ustawi wa Watanzania
 
Jana hii mbichi hata haijakauka watu wa Tanesco wameswekwa ndani na mkuu wa wilaya kwa uzembe.
 
Niulize tu.
Hivi hii serikali Ina calculate percentage namna gani?
Ni muda sasa November mwaka Jana walisema kituo Cha mabasi Mbezi kimekamilika kwa asilimia tisini na ushee. MPAKA LEO MABASI TUNAPANDIA UBUNGO. mkuu wa mkoa na maingineer wake wapo tu.
Mwaka Jana July walisema reli ya Dar Moro SGR imekamilika kwa asilimia themanini. MPAKA LEO BADO HAIJAKAMILIKA.
Barabara ya Kimara Kibaha kitambo tu walisema imekamilika kwa asilimia tisini na ushee.
WEWE MSOMAJI NI SHAHIDI YANGU.
Tangu waseme wamezambaza umeeme kwa asilimia nyingi Ni kitambo sasa. NYOTE NI MASHAHIDI WAUZAJI WA SOLAR WANAENDELEA KUNEEMEKA
 
Kwa tabia zenu naomba msikumbuke vijijini mkasahau mijini..., yaani usambazaji ukawa ni wa miundombinu na sio umeme (yaani tukagawana mgao..)

Fanyeni hima tuongoze Africa kwa gharama ndogo za kutumia umeme wengine oven tumeshabadilisha zimekuwa za kutunzia buibui....
 
Sio kweli nyinyi ni waongo kwa Nini mnakata umeme Kila siku mtaani kwangu
 
Back
Top Bottom