Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kijijini kwenu mtakuwa kwenye idadi ya vijiji 3000 vilivyosalia kuwekewa umeme.Mnasemea vijiji gani? Kijijini kwetu mbona hamna Umeme? Hata nguzo tu hamna yaani hata ile dalili tu ya kuwekewa umeme hamna.
Mradi wa REA tu wenyewe umeshindikana kumalizika mmeacha nguzo zimesimama mkaondoka sijui mnatuonaje sisi wananchi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Tanzania imeshika nafasi ya kwanza barani Afrika kwa kufanikiwa kusambaza umeme nchini kote kwa asilimia 80.
Mhe. Majaliwa aliyasema hayo wakati akielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano kwenye mkutano wa viongozi wa dini kutoka kamati za amani za Mikoa mbalimbali Tanzania bara na Zanzibar, uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
“Leo hii Tanzania ni ya kwanza barani Afrika kwa kusambaza umeme kote nchini hadi vijijini na kufikisha asilimia 80. Kuna nchi ngapi barani Afrika, lakini Tanzania imefanikiwa kuwa ya kwanza. Tumeweza kufikia vijiji 9,112 Tanzania na hadi Aprili 2020 na tumetumia shilingi trilioni 2.27,” amesema.
Akizungumza na viongozi waliohudhuria mkutano huo uliandaliwa ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika ustawi wa amani, uzalendo na kumtanguliza Mungu, Waziri Mkuu amesema ushirikiano mkubwa wanauonesha kwa Serikali, umewezesha kufanya mambo mengi ikiwemo kuimarisha huduma za upatikanaji wa nishati kwa ajili ya ustawi wa Watanzania
Ila awamu hii kwenye suala la umeme kdg wamejitahidi tuwape pongeziMgao wa umeme utaisha lini wazee?
Ila awamu hii kwenye suala la umeme kdg wamejitahidi tuwape pongezi
Ova