Tanzania yashika Namba 6 Kwa Utawala Bora kusini mwa Jangwa la Sahara

Kwenye ripoti kama hizi, mimi huwa siangalii tu Tanzania imekuwa ya ngapi, huwa naangalia pia ime'score' kiasi gani katika kila 'pillar' iliyotumika katika kupima overall rank. Mfano, kwenye ripoti hii, nchi 120 zilifanyiwa utafiti. Ukifuata idadi ya nchi zilizofanyiwa utafiti ukagawa kwa 2, utapata 60. Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba nchi zilizoshika nafasi 1-60 ni zile zilizofanya vizuri zaidi ya nchi zilizoshika nafasi kuanzia 61-120. Mind you sisi tumeshika nafasi ya 78.

Pillars 7 zilitumika kupima overall ranking. Kwenye leadership & foresight, Tanzania ilishika nafasi ya 40, kwenye robust laws & policies (80), kwenye strong institutions (95), kwenye financial stewardship (57), kwenye attractive market place (77), kwenye global influence & reputation (83) na kwenye helping people rise (86). Kwa hiyo, utaona katika pillars 7, ni pillars 2 tu Tanzania imekuwa kati ya 1-60, na katika pillars 5 imekuwa kati ya 61 na 120. Katika sub-Saharan Afrika, ni nchi 24 tu zilifanyiwa utafiti, na katika hizo, Tanzania imeshika nafasi ya 6, na pengine kama nchi zingefika 50+ tungeshika nafasi ya mbali zaidi.

Kwenye ripoti hii, kwa kulinganisha na ripoti ya mwaka jana, Tanzania imepanda juu kutoka nafasi ya 80 hadi 78.

Lakini pia unaweza kusoma ripoti inayoitwa 'People Power Under Attack 2024', na nyingine ya World Justice & Peace (WJP) Rule of Law Index 2024.

Kwa hizi, ripoti mbili matoleo ya mwaka huu bado hayajatoka.

Hata hivyo, jambo la msingi ni kujilinganisha na top performers na kuona maeneo ambayo inabidi yafanyiwe kazi zaidi. Kwenye ripoti ya Good Government Index 2025, top performer ni Singapore na ime'score' kama ifuatavyo: leadership & foresight ni ya 1, robust laws & policies (9), strong institutions (1), financial stewardship (5), attractive marketplace (1), global influence & reputation (25), na helping people rise (1).

Kwenye ripoti ya WJP Rule of Law Index 2024 katika nchi 142 Tanzania ilishika nafasi ya 96 kati ya nchi 142. Ukichukua 142 kugawa kwa 2 utapata 71. Hivyo, nchi zilizoshika nafasi 1-71 ni good performers kuliko zilizoshika nafasi 72-142.

Anyway, kwenye ripoti hii, katika pillars 8 na kati ya nchi 142, Tanzania ilishika nafasi ya 81 kwenye constraints on government powers, ya 94 kwenye absence of corruption, ya 111 kwenye open government, ya 112 kwenye fundamental rights, ya 80 kwenye order & security, ya 95 kwenye regulatory enforcement, ya 88 kwenye civil justice, na ya 96 kwenye criminal justice. Overall score ni 0.47 kwenye scale ya 0-1.

Top performer katika pillars zote 9 ni Denmark. Ni ya 1 kati ya nchi 142. Ilishika nafasi ya 1 kwenye constraints on government powers, ya 1 kwenye absence of corruption, ya 3 kwenye open government, ya 1 kwenye fundamental rights, ya 3 kwenye order & security, ya 1 kwenye regulatory enforcement, ya 1 kwenye civil justice, na ya 1 kwenye criminal justice. Overall score ni 0.90 kwenye scale ya 0-1.

Ripoti ya People Power Under Attack 2024, nchi 198 zilifanyiwa utafiti, na ziliwekwa kwenye categories 5: 1) Open Space, 2) Narrowed Space, 3) Obstructed Space, 4) Repressed Space, na 5) Closed Space. People Power Under Attack 2024 categorises Tanzania as a country with 'repressed civic space'.
 
Sawa mchambuzi Mimi ni nani Hadi nibishe.

Hata hivyo sampling ilifanyika kisomi ndio maana tuko vizuri
 
Sawa mchambuzi Mimi ni nani Hadi nibishe.

Hata hivyo sampling ilifanyika kisomi ndio maana tuko vizuri
Kwani nimekubishia, kiongozi? Hata mimi ripoti hizi nazitumia kuonyesha maeneo ambayo tumefanya vizuri, na maeneo ambayo hatujafanya vizuri, lakini tunaweza kuyaboresha.
 
Kazi ya Rostam azizi hiyo kugwawa ruzuku
 
Daa tumempita mpaka Rwanda kweli tuko vizuriiiii...... 😀 😎
 
Nasema no
 
Hamuwezi kulazimisha yule raisi wa Malawi apendwe na raia wake ....Yani hata anye almasi aanze kuzigawa nyumba Kwa nyumba...kama wananchi washamkataa washamkataa tu.
 
Hamuwezi kulazimisha yule raisi wa Malawi apendwe na raia wake ....Yani hata anye almasi aanze kuzigawa nyumba Kwa nyumba...kama wananchi washamkataa washamkataa tu.
Nani amekulazimisha? Onyesha nilipoandika wewe Unatakiwa kumpenda?

Unahisi ukiandika hayo ndio itakusaidia wewe kumzuia asiwe Rais ? Mpumbavu Huwa anatafuta kupendwa.
 
Namibia hakuna kisa anawatishia habari za Visa reciprocity Marekani na mataifa makubwa.
Hizi takwimu mara nyingi ni za kupikwa tu.
 
Tanzania ni Nchi Moja salama na nzuri ya kuishi huko kwingine ni jela kama sio jehanamu ndio maana mnapata fursa hata ya kutukana.
Akili huwa mnapeleka wapi?

Wapi Mdude, Soka, Azory, Ben saa8 kwa uchache.

Nani alimuua mzee Kibao mchana kweupe?

Utawala bora mnazungumzia nini wapuuzi wakubwa nyinyi?
 
Akili huwa mnapeleka wapi?

Wapi Mdude, Soka, Azory, Ben saa8 kwa uchache.

Nani alimuua mzee Kibao mchana kweupe?

Utawala bora mnazungumzia nini wapuuzi wakubwa nyinyi?
Waulize Polisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…